Sensa 2012: Yanayojiri

Mie najiandaa kubandika bango langu la "Nyumba hii ni ya waislam hatuhesabiwi" ili huyo kalani wenu asijisumbue kufika hata uwani kwangu.
 
Hakuna kitu kama hicho!
Ni maneno tu ya wanasiasa kujikosha.
Kuongea leo wakati a na uhakika kuwa hakuna kitakachobadilika ni upopompo!
 
Akili zake zimeifadhiwa kwenye masoz za mwili wake
 
Mimi nimejipanga kutoa DATA za uongo! Na hawana namna ya ku-verify! RIP sensa!
 
kama hiyo kauli imetoka kwa kiongozi basi Tz kuna tatizo kubwa kuliko tunavyofikiria.
 
Leo sifungiii mbwa ndani ole wao Sasa waingie! SENSA kwa maendeleo ya Taifa my foot! Mbona hayo maendeleo siyaoni
 
Leo nimetulia home nikisubiri kuhesabiwa kama Serikari (iwe dhaifu au imara) ilivyo tutangazia regardless msimamamo wangu wa kisiasa wala ki-IMANI.... ya Kaisari mpe Kaisari.... ya Mungu mpe Mungu.....
 
Imefika saa 8:30 usiku mhudumu wa hoteli amekuja kuginga mlango wa chumba changu, akaniambia nitoke nje kuna watu wa sensa wananihitaji, nikawaambia kwa muda huu siwezi kutoka waje asubuhi, nikakomea mlango nikarudi kulala, inawezekana hawakuridhika na majibu yangu mhudumu akarudi tena kugonga mlango tena mara hii kwa nguvu kweli sikuweza kufungua, nikaona hali iko hivyo kwa vyumba vya jirani wanagongewa hawafungui, si mmoja wa waliogoma lakini kwa style na muda wenyewe nililazimika kutotoa ushirikiano, niliwaambia warudi asubuhi mpaka muda huu nimeamka sijaona dalili kama kweli wanaweza kurudi kuja kutuhesabu tena, wewe ni zipi changamoto zimekupata kwa zoezi hili la sensa lililoanza saa 6:01 usiku?
 
Hata wakati wa utawala wa mfalme Herode walifanya sensa na kila mtu alihesabiwa katika mji aliozaliwa. Mie na familia yangu tutahesabiwa. Ili msiniulize sababu ya sensa wakati wa mfalme Herode maana sikumbuki mpaka nisome hiyo aya
 
kama hiyo kauli imetoka kwa kiongozi basi Tz kuna tatizo kubwa kuliko tunavyofikiria.

Tena kuna zaidi ya matatizo, just imagine kwa mwaka huu 2012 kunafanyika zoezi la vitambusho na sensa. Kwa viongozi/watendaji wenye akili wangefikiria ku-merge ili fedha nyingine zikanunulie watoto wetu madawati huko shuleni. Ni aibu nchi hii yenye miti kila kona kukosa madawati
 
hivi wateja waliolala bilila lodge wamehesabiwa?
 
Hapa kahama bado kabisa nasikia sikia itachukua mda maana hata makarani wana malalamiko kuhusu posho zao
 
Mimi tayari nimehesabiwa, lakini la kushangaza kwa sababu ya umbo langu nimehesabiwa kama watu wawili. Madai yao ni kwamba kama serikali inakadiria mipango chakula kwa ajili ya kulisha kila mtanzania, mimi nitahitaji double!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…