Zimmermann
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 4,051
- 3,615
Kwa uzoefu wangu humu ndani, kwenye hicho kipengele cha mwisho Mkandara angekujibu: Msiwalazimishe waislam wafanye kama wakristu(kusign MoU). Huku ni kuhalalisha dhambi ileile wanayofanya wakristu. Kinachotakiwa ni serikali kujitoa kwenye makubaliano na vyombo vya dini, ijenge shule nyingi, hospitali na kutoa huduma nyingine za jamii vizuri.Kaka, toka nimejiunga na JF, nimekufahamu kama mtu ambaye yuko objective, sijawahi kushawishika kuhoji msimamo wako ktk masuala mbali mbali, wala sitaanza leo.
Nimesoma post zako ktk hii thread, sikushawishika kuhoji kwasababu nilielewa mantiki yako hata kama siamini unachokisema kwa 100%. Maoni yangu niliyaelekeza kwa Ritz kutokana na msimamo wake.
Nikirudi ktk hoja zako; nani mwenye jukumu la kutoa takwimu? Kwa mujibu wa JK, NBS pekee ndio wenye mamlaka ya kutoa takwimu. Serikali ina uwezo wa kumuzuia mtu au taasisi yoyote kutoa takwimu ikiwemo mimi na wewe hapa kwenye mtandao?Kuna ugumu kidogo..
Hakuna mahali ktk post yangu niliposema kipengele cha dini kisiwekwe. Wacha kiwekwe tu, pamoja na vipengele vingine kama kabila, sexual orientation, n.k. Nisichopenda ni kuona hii ndo inafanywa kuwa "ishu" ya liwalo na liwe! Ushauri: Rais ni msikivu, viongozi wa kiislamu wakaongee naye. Ukimpa rais ultimatum unamfanya awe defensive. Hao wanaopata ruzuku ktk afya na elimu nao waligomea sensa? Hizi harakati na "fujo" ndizo zinafanya uislam uwe na image mbaya.
Viongozi wa kislamu wamefikia wapi ktk kudai mkataba na serikali toka Rais atamke akiwa dodoma kwamba hawajaomba wakati "wenzao" waliomba?
Mkuu,hiyo ni nyumba ya familia ambayo nimeijenga mimi.Huenda kule weekend tu.Karibu kwangu Mikocheni B Mkuu...Sijui ni option pia, na ipo kwenye dodoso. Au wewe ulitakaje, wakufuate ulipoenda?
Kubwa zima halioni aibu kusema linakaa kwa kakaake. Akili za kula bure bwana
Ndugu Job K, Utafiti wa kuwa Mtoto/watoto wa kijijini hana/hawana ujasiri wa kujieleza kuliko wa mjini wewe umeufanyia wapi?
Hayo ya lugha mbona wengine hatukuulizwa? Mtaalam wa sensa atusaidie kwa hili...kwanza kuna maswali mengine nadhani huwa wanajitungia wenyewe hapo hapo. halafu sometimes wanaboa, eti kama mimi aliniuliza elimu yangu nikamwambia chuo kikuu, badae akaniuliza naongea lugha ngapi nikamwambia mbili na ya kwetu ya tatu. akaniuliza hizo mbili ni kiingereza na kiswahili? nikamjibu ndiyo, akaniambia ni kweli au unanidanganya? nikamwambia nakudanganya sijui kiingereza (manake niliboreka) sasa sijui alijaza nini. Haya Mr. hakuwepo, akamuona mtoto mmoja mwingine alikuwa kalala, eti baba yake ni mtanzania, nikamwambia ndio, mbona huyo mtoto kama shombe? na wakati mtoto ni mweusi (mimi ni mweupe sana) bora angekuwa amefuata hata huo weupe wangu, nikamwambia kalete DNA test na mtafute babake uwapime! In short mambo ya kuboa yalikuwa mengi. nitakesha nikiyaandika.
nimepatwa na mshangao!
Hii sensa ya mwaka huu kweli tutapata takwimu sahihi? Hebu naomba mnaoshiriki ku-sensisha watu mnisaidie! Hivi mlielekezwa kwamba msipokuta watu wazima hata watoto wanaweza ku-sensiwa? Nyumbani kwangu binti yangu wa miaka 7 amejibu maswali ya sensa - big up my daughter - una akili kama mpaka watu wa sensa wanaridhika na majibu yako?!!.
Sasa najiuliza kama na huko vijijini ndo hali itakuwa hii tutapata takwimu sahihi kweli? Angalau mtoto wa mjini unaweza kusema ana ujasiri wa kujieleza sasa huko vijijini wataweza? Nahitimisha kwa kusema "sensa hii ni bure kabisa" ninazidiwa na sensa zinazofanywa kwa wakimbizi. Bora tusiwe na zoezi hili linalokula pesa yetu na kutupa takwimu za hovyo!
Hayo ya lugha mbona wengine hatukuulizwa? Mtaalam wa sensa atusaidie kwa hili...
Ndugu Job K, Utafiti wa kuwa Mtoto/watoto wa kijijini hana/hawana ujasiri wa kujieleza kuliko wa mjini wewe umeufanyia wapi?
Mkuu wangu paragraph yako ya kwanza inajieleza vizuri sana na jibu lake linapatikaa paragraph ya pili.. Unaposema shule ya St Sebastin ni ya Wakristu ina maana tayari serikali imewapa kibali hawa wenye shule hiyo (kwakristu) kujihusisha ktk shughuli za maendeleo. Ni kutokuwa na takwimu hizi ndio maana muafaka wa Muo Uliundwa, ni kutokana na takwimu hizi ndio maana mnawakatalia waislaam kujiunga na OIC ama hata kuwarudishia shule zao kama mlivyorudishiwa wakristu na hata kuwa sehemu ya serikali ktk kuendesha shughuli za Elimu na Afya. Wewe nambie imekuwaje leo serikali imeingia muafaka na dini ya Kikristu kuendesha Elimu na Afya ikiwa huamini ktk utengano wa kiimani?.. Je hizi sio shughuli za maendeleo ambazo mnaiweza sensa hii...Hatuogopi, ila hatuoni sababu.
Mimi nafikiri sensa inafanywa na serikali, na inafanywa kwa makusudi maalum. Kuwatambua wananchi wake, idadi, shughuli zao za uchumi, hali za afya na uzazi n.k. Kwa kila kipengele hapo, serikali imelenga kupata takwimu zake kwa sababu fulani. Na ni kwa sababu hiyo serikali inaingia gharama za kuhesabu watu na kujua taarifa zao. Sasa ni yepi yatakuwa makusudi ya serikali kutaka kuwajua watu kwa dini zao? (Hili la kwanza)
Kwenye suala la umiliki wa wa shule mkuu huo utakuwa ubishi wa kitoto. Hivi shule ya St. Sebastian inakuwa inahusiana vipi na serikali ikiwa wewe umeshasema ni ya taasisi ya dini? Manake unaposema kama mtakubali nashindwa kuelewa unalenga nini. Kwani ukishajua idadi ya waislamu na wakristo kutakuwa na tofauti ipi ya umiliki wa kitu ambacho si chako?
Halafu hebu tuje wenye uislamu wenyewe: Hivi leo ikitulazimu kuwatambua waislamu, kipi kitakuwa kigezo? Watu wataitwa na kutabulika kuwa waislamu kwa kanzu na ndevu au kwa majina yao?
Nauliza hivi kwa kuwa juzi tu, hapa hapa JF kulizuka matusi na kashfa nyingi juu ya Mufti wenu wenyewe kiasi cha wengine kumuita KAFIR yeye pamoja na ma-kadhi aliowachagua mkiwashutumu kuwa ni vibaraka wa serikali. Kwa mujibu wa maelezo yenu, mtu yeyote mwenye kupinga maendeleo ya Uislamu ni KAFIR.
Sasa ikiwa baadhi yenu mlishapanga kugomea sensa, na hilo likachukuliwa (miongoni mwenu) kuwa ndio jambo jema kwa uislamu, ina maana wote wanaounga mkono sensa ni makafir. Rais wa nchi, viongozi wa BAKWATA na vyama vingine vya dini yenu na Watanzania wote ni makafir. Je, ingekuwa ndio wewe Mkuu Mkandara umepewa jukumu la kuwahesabu Waislamu na kupata idadi yao, wanaounga mkono sensa utawahesabu kama waislamu au sio waislamu?
Ndugu kuna watu wazima tena siyo watoto maeneo ya vijijini bado wapo katika hali ya woga nakutoelewa kinachoendelea.
Akifika mgeni watu wanamshangaa au kumkimbia kwa hofu, sembuse watoto ukamuulize maswali akujibu THUBUTUUUUUUUUUUUU!!!!!!!
Tunaomba wahusika na kuhesabu watu (SENSA) watumie busara na siyo ili kutimiza wajibu wa kuzunguka mitaani) Hapa mnaweza kutupa wasiwasi hata kuweza kujaza takwimu zauongo katika makaratasi ya sensa. Na mwisho wa siku kwenda kukinga mshiko!!!!
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Nimepatwa na mshangao!
Hii Sensa ya mwaka huu kweli tutapata takwimu sahihi? Hebu naomba mnaoshiriki Ku-sensisha watu mnisaidie! Hivi mlielekezwa kwamba msipokuta watu wazima hata watoto wanaweza ku-sensiwa? Nyumbani kwangu binti yangu wa miaka 7 amejibu maswali ya Sensa - Big up my daughter - una akili kama mpaka watu wa sensa wanaridhika na majibu yako?!!.
Sasa najiuliza kama na huko vijijini ndo hali itakuwa hii tutapata takwimu sahihi kweli? Angalau mtoto wa mjini unaweza kusema ana ujasiri wa kujieleza sasa huko vijijini wataweza? Nahitimisha kwa kusema "SENSA HII NI BURE KABISA" ninazidiwa na sensa zinazofanywa kwa Wakimbizi. Bora tusiwe na zoezi hili linalokula pesa yetu na kutupa takwimu za hovyo!