Seneta John McCain apatikana na saratani ya ubongo

Seneta John McCain apatikana na saratani ya ubongo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,610
Seneta wa chama cha Republican John McCain amepatikana na saratani ya ubongo na anatafuta matibabu kulingana na duru za offisi yake.

Matibabu hayo huenda yakashirikisha matumizi ya dawa ama mionzi kulingana na daktari wake. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 80 yuko katika hali nzuri akiendelea kupata afueni nyumbani. Uvumbe huo ulipatikana wakati wa upasuaji wa kuondoa damu ilioganda juu ya jicho lake la kushoto.

McCain ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita nchini Vietnam pia alitumikia miaka mitano jela. Seneta huyo aliyehudumu kwa mihula sita na kuwa mgombea wa urais wa chama cha Republican 2008 alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Phoenix katika jimbo la Arizona siku ya Ijumaa.

Uchunguzi wa tishu ulibaini kwamba uvimbe wa ubongo unaojulikana kama glioblastoma ulisababisha damu hiyo kuganda kulingana na taarifa ya kliniki hiyo ya Mayo. Madaktari wa Seneta huyo wanasema kuwa anaendelea kupona kutoka kwa upasuaji huo na afya yake iko shwari, iliongezea.

Matibabu yake yatashirikisha utumiaji wa dawa na mionzi. Glioblastoma ni uvimbe mbaya wa ubongo na huongezeka kutokana na umri wa mtu ukiwaathiri wanaume wengi zaidi ya wanawake.

Bwana McCain ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya sineti kuhusu hudumu za jeshi alikuwa katika hali nzuri huku akiendelea kupona nyumbani na familia yake, afisi yake ilisema.



Chanzo: bbc swahili
 
Senator wa Republican ambaye alishawahi Kugombea Urais pia wa Marekani Senator Mc Cain amekutwa na Ugonjwa wa Cancer ya Ubongo aina ya Tumors ambayo Madaktari Wanasema ni Cancer ambayo ni aggressive zaidi



Baada ya Taarifa hizo Viongozi mbalimbali walimtakia mapambano mema.

Wakuu tutunze Afya Zetu Mara nyingi Best wishes za Cancer huwa kama Umekufa hivi unaweza Kuona wamarekani wanatoa picha zake za Utotoni, Pia alikua mwanajeshi huu Jamaa.

Mi namtakia mapambano mema.

Rais Bill Clinton


Rais Obama
DFJXX4BXoAAWLdS.jpg


Hillary Clinton
DFJXX4CXcAAzFXB.jpg



Makamu wa Rais Wa Obama Joe Birden
DFJXX4AXUAUSboF.jpg


Secretary Hillary Clinton
DFJXX4CXcAAzFXB.jpg


TAARIFA KUTOKA OFISI YA MC CAIN
DFIyr-YXYAAlACV.jpg

​
 
Ugonjwa uliomuondoa mamayangu wa kambo huo.
Ajitahidi kuomba sana mana safari si mbali nayo Alipo
 
Kuna Aina Za tumor ya Ubongo Vijana Wa KCMC, MUHAS wanajua hili na HKL na KLF upo kusahihisha Lugha.
Mimi mwenyewe ni mmoja Kati ya hao vijana wa MUHAS na hamna kitu kama hicho ulichosema.
Anyways kwa kukusaidia.
Cancer ni aina ya tumor,
Tumors zipo aina mbili
1. Benign: hizi hazijasambaa kutoka sehemu zilipoanzia
2. Malignant: hizi ndizo zinaitwa cancers kwamba zimesambaa kutoka pale zilipoanzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
John McCain wakati wa vita ya vietnam na Usa alitekwa na wanajeshi wa kivietnam wakamuweka kwenye shimo refu mpaka alipokuja kuokolewa na wenzake akili zote akawa ameziacha shimoni(in putin voice)
 
Ugonjwa uliomuondoa mamayangu wa kambo huo.
Ajitahidi kuomba sana mana safari si mbali nayo Alipo
Mama yako aliondoka mapema zaidi kutokana na aina ya matibabu
 
Mimi mwenyewe ni mmoja Kati ya hao vijana wa MUHAS na hamna kitu kama hicho ulichosema.
Anyways kwa kukusaidia.
Cancer ni aina ya tumor,
Tumors zipo aina mbili
1. Benign: hizi hazijasambaa kutoka sehemu zilipoanzia
2. Malignant: hizi ndizo zinaitwa cancers kwamba zimesambaa kutoka pale zilipoanzia

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndiye Ulimboka Dr.
Sema ndio!
 
John McCain wakati wa vita ya vietnam na Usa alitekwa na wanajeshi wa kivietnam wakamuweka kwenye shimo refu mpaka alipokuja kuokolewa na wenzake akili zote akawa ameziacha shimoni(in putin voice)

Mkuu hakuna aliye kuja kumuokoa McCain alipo tekwa huko VietNam - aliachiwa na WavietNam baada ya vita kumalizika.
 
Back
Top Bottom