Senene kuongezwa kwenye orodha ya vyakula vinavyotolewa kwenye ndege katika safari za kimataifa nchini Uganda.

😋😋😋mate yamenijaa hatari, mwezi ujao nitakuwepo huko nitawala sawasawa
 

Wadudu wana protein x 3 zaidi ya nyama
IMG_3351.png

IMG_3350.jpg

IMG_3348.jpg

Na mishkaki kwa raha zangu
 
Yani mimi nilivyo mdudu siwezi kula hata kidogo.

Ukikaangiwa na uyoga bila na nyanya na vitunguu wakapondwa huwezi kujua
Mimi nakumbuka utotoni nilikula kwa sababu Jirani zetu walikuwa wanakaanga sana nikajaribu kumbikumbi
Ila ulikuwa utoto sijala tena kwa kusema ukweli

Natania tu
 
Baada ya kusambaa kwa video inayomuonesha mchuuzi wa Senene aliyekuwa akiuza bidhaa zake ndani ya Ndege ya Shirika la Ndege la Uganda, Shirika hilo limesema linafikiria kuongeza Senene (Nsenene) katika orodha ya vyakula ndani ya ndege katika safari za kimataifa zinazofanywa na ndege zake.

Awali, video hiyo ilizua hisia tofauti kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wakijiuliza, mchuuzi huyo aliweza vipi kupenyeza na bidhaa hiyo katika uwanja wa ndege na kufanikiwa kuiza, huku wengine wakimpongeza kwa ‘ujasiri’ wake.

Shirika la Ndege la Uganda limekiri kuwa Wasafiri wa ndege hiyo, aina ya Airbus A330 iliyokuwa ikitoka Uwanja wa Entebbe kwenda Dubai Novemba 26, 2021, walionekana kufurahia bidhaa hiyo, na kuwa wamejifunza kutokana na tukio hilo. Shirika hilo limesema litatumia fursa hiyo kukuza utamaduni wa vyakula vya asili vya Uganda duniani.

ATCL hii ni FURSA kwenu ichangamukieni pia.

Chanzo; Jamii forum App

UGANDA: Shirika la Ndege la #Uganda limetangaza kuongeza Senene katika orodha ya Vyakula vinavyotolewa kwenye Ndege katika safari zake za Kimataifa

Hatua hiyo imekuja baada ya Wasafiri kufurahia Senene waliokuwa wanauzwa na mchuuzi ktk Ndege

Soma Uganda Airways kuongeza Senene katika orodha ya vyakula ndani ya ndege baada ya video ya mchuuzi kusambaa mitandaoni

#JFLeo https://t.co/WnGErA7mkC
View attachment 2026099
Waki rasmisha hiyo nsenene kwenye flights zao inabidi wamlipe royalty huyo msela kwa kuchukua idea yake.pia wawaombe radhi wafanyakazi
 
Back
Top Bottom