Ni maskini ukimlinganisha na Mramba.
Sawa ndio maana Mramba yuko mahakamani hivi sasa na karibu atapata kifungo cha muda mrefu!!! Hawezi kupona hii kesi!
Ni maskini ukimlinganisha na Mramba.
Karim Wade, mtoto was rais wa zamani wa Senegal, Abdoulaye Wade kawekwa lupango miaka 6 kwa ufisadi. Uhalifu huo ulifanyika chini ya mwavuli wa, na kulindwa na baba yake wakati akiwa madarakani. Hili ni fundisho kwa jamaa fulani hapa kwetu pia.
Hata ukimtetea vipi huyu kijana ndio njia anayotumia baba yake kuliibia Taifa hivyo sintashangaa kama yatakuja kumpata kama yaliyompata huyo wa Senegal!!! Atie maji nywele zake wakati wenzie wananyolewa!!
Kama unao ushahidi kuwa Baba yake anaiibia Tanzania kupitia mtoto wake, uweke hadharani ili na sisi tuushuhudie lakini kama unazungumza kwa kuhisi, kudhani na kutegemea maneno ya kijiweni, utakuwa unakosea sana kwa sababu ni uonevu wa dhahiri.
Ridhiwani ni kijana mwenye maadili, angekuwa mwingine kwenye nafasi hiyo, wengi mngeugua kwa msongo wa mawazo.
Kuna kesi alifungua dhidi ya wananchi fulani kwamba walimkashifu kwa kusema kuwa amejilimikizia mali kwa mgongo wa baba yake,ile kesi iliishia wapi? Angekuwa na maadili asingetuhumiwa!!
Hiyo haitoshi kujustify tuhuma dhidi yake, kuna kusameheana, kupuuza na sababu nyingi za kuifanya kesi isiendelee, labda wewe utuelezee kuwa iliishaje hadi mhitimishe kuwa ni kwa sababu tuhuma dhidi yake zilikuwa za kweli.
Aliogopa kuendelea na kesi ile kwani mambo mengi ambayo wananchi walikuwa hawayajui juu ya ufisadi wake yangeibuliwa mahakamani!!
Alitamka hivyo? Alimwambia nani? Ni mambo gani hayo, hebu yatoe hapa tuamini kuwa unachokizungumza kina ukweli na uyasupport na ushahidi.
Maswali yako yanaonesha kuwa wewe kama alivyo yeye ni mwanasheria uchwara!! Yeye ndio aliyeshitaki na kama yeye ndio aggrieved party halafu hafuatilii kesi yake maana yake yale yaliyosemwa juu yake na wale aliowashitaki ni kweli hivyo anaona afadhali akae kimya yaishe!!
Unachekesha sana! Unataka kuniambia kuwa haiwezekani mtu akasamehe au kupuuzia pamoja na kuwa yeye ndie mlalamikaji? Au huna ushahidi kuthibitisha tuhuma zako dhidi yake? Kudhani ndiko kunakowafanya wengi muumize wengine huku mkifunika makosa yenu kwa visingizio vingi. Tafadhali, nakuomba uulete ushahidi kuthibitisha tuhuma zako dhidi yake ili unisaidie na mimi kuuelewa ubaya aliowafanyia Watanzania kiasi cha kubebeshwa lawama zote hizi!
Una uhakika kuwa endapo aggrieved party asipofuatilia kesi yake inajustify tuhuma dhidi yake bila ushahidi wa nyongeza?
Ushahidi wa nyongeza ungetolewa mahakamani na huo ndio uliomfanya akaenda kufuta/kutofuatilia kesi!!! Baba yake akitoka madarakani kila kitu kitawekwa hadharani; hivi sasa kuuweka hadaharani ni kupoteza wakati kwani hawatamshuhurikia!!! Angojee muziki kama anaoucheza mtoto wa Rais wa zamani wa Senegal!!
Hao unaosema wanampenda ni kwa sababu ya madaraka ya baba yake hata huyo mtoto wa aliyekuwa Rais wa Senegal alikuwa si mbunge tu bali waziri na alikuwa na wapambe wengi tu!! Hao unaosema wanaompenda sasa ni waganga njaa tu ambao hufuata mahala penye chakula sio watu wa kuwaamini sana!!
Wewe unaemchukia bila sababu za msingi ndio wa kuogopwa zaidi kwa sababu hao unaosema ni waganga njaa, huna ushahidi kuwa anawalisha, Ridhiwani hawezi kumlisha kila mkaazi wa Chalinze.
Nasubiri huo ushahidi wa mabilioni aliyoiba ili na mimi nijiridhishe juu ya uhalali wa tuhuma dhidi yake.
Ushahidi wa kukuridhisha juu ya wizi wao utaupaya baada ya utawala wao kufikia ukomo wake; kwa sasa kuutoa itakuwa tunacheza KIDUKU ngoma ya kikwere!!!!
Haisaidii, kutokuutoa sasa ni ushahidi wa wazi kuwa hamna huo ushahidi. Sioni utofauti wa kuutoa sasa na kuutoa baadae kama nia yenu ni ya dhati na si kumtungia hadithi kwa sababu mnadhani ndivyo au mnahisi ndivyo alivyo kwa vile tu ni mtoto wa Rais.
Hata kama unasema haisaidii basi msaidie nduguyo angalau kwa kumshauri kuwa aanze kutia maji nywele wakati wenzie wananyolewa!! Kwani wakina Makongolo baba yao hakuwa Rais na mbona hawana tuhuma?
Hawana Tuhuma? Hebu fuatilia kuhusiana na familia ya Nyerere na fedha walizodaiwa kustash Canada, nani amethibitisha hilo mpaka leo?