Uso wa nyoka
JF-Expert Member
- Mar 17, 2014
- 4,791
- 2,381
Hizo za Canada hazina ushahidi lakini zenu mlizotuibia zina ushahidi kwani hamjui kuiba mnaacha tracess nyuma; hongo zenu zote mlizopata kutoka kwa WACHINA kupitia dalali wenu Shimbo zinajulikana zilikofichwa!!!
Sisi kina nani? Hakuna traces wala kilichoibiwa, unazungumza kwa kudhani na huna ushahidi wowote ulionao kuthibitisha uhalali wa tuhuma zako dhidi yake, kwa sababu katika hali ya kawaida ungeuweka huo ushahidi kusupport hizo kauli kama ambavyo wengi wanafanya humu jukwaani pale wanapomtuhumu mtu. Kuna watu wamewahi kutaja akaunti za benki, kiasi cha fedha katika akaunti, mikataba iliyosainiwa, namba ya hundi na kiasi cha fedha kilicholipwa na vitu kama hivyo. Sasa wewe unaposhindwa kuweka hadharani vitu kama hivyo, sioni sababu ya kuendelea kumshutumu mtu kwa sababu hakuna kinachothibitisha kuwa unachokisema kina ukweli. Ungekuwa unao ushahidi ukauweka hadharani, sidhani kama swala la kupinga shutuma zako dhidi yake lingekuwa na nguvu na kusema eti hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi yake si swala la msingi kwa sababu hakuna ulichowahi kukitolea uthibitisho.