Sendeka awavaa wanaokingia kifua vigogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sendeka awavaa wanaokingia kifua vigogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 24, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,440
  Trophy Points: 280
  Sendeka awavaa wanaokingia kifua vigogo

  2008-12-24 12:38:07
  Na Simon Mhina

  Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, amesema kamwe hakuna kigogo nchini atakayekamatwa na nchi kutikisika.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Sendeka alisema madai hayo yanatolewa na wapambe wa baadhi ya vigogo kwa lengo la kujijengea `kinga`.

  Sendeka alisema hakuna mtu anayeweza kutikisa nchi kama Tanzania ambayo inaongozwa na sheria, huku ikiwa na vyombo thabiti vya dola; serikali, bunge na mahakama.

  ``Nashangaa wanaosema eti fulani akikamatwa na kufikishwa mahakamani nchi itatikisika, hakuna wa kutikisa nchi.

  Wanaotoa madai hayo ni wapambe wa vigogo ambao wanadhani wapo hatarini kufikishwa mahakamani,``alisema.

  Mbunge huyo alisema kama kuna mtu ambaye akiguswa nchi inaweza kutikisika ni Rais.

  Alikuwa akitoa maoni yake juu ya mjadala unaoendelea, ambao ulianzishwa na wanasiasa na wanasheria, wakitaka Rais mstaafu Benjamin Mkapa aondolewe kinga ili aweze kuburuzwa mahakamani.

  Sendeka alisema kimsingi yeye hakubaliani na wazo la kumuondolea kinga Mkapa kwa sababu kuu mbili;
  mosi, wanaosema apokonywe kinga hawajawa na ujasiri wa kutaja waziwazi makosa yake.

  ``Wengi wanasema aunganishwe na fulani aunganishwe na yule, lakini hawasemi, kuwa wanataka yeye kama Mkapa asomewe shtaka gani?`` alihoji.

  Pili, alisema kumfikisha mahakamani rais mstaafu, linaweza kuwa jambo ambalo halina maslahi kwa hatima ya taifa.


  Alisema kutangaza kwamba mtu fulani akikamatwa nchi itatikisika, ni sawa na kumdhalilisha rais aliyeko madarakani kuonekana serikali yake ni legelege.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,440
  Trophy Points: 280
  Huyu Sendeka naye ni msanii. Hivi hajui kweli ni makosa gani yanayozungumzwa na Watanzania ambayo Mkapa aliyafanya kuifisadi Tanzania!? :confused:
   
 3. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huo tayari ni uoga. Yaani kumfikisha Mkapa mbele ya sheria ni jambo ambalo halitakuwa na maslahi kwa Taifa???????? Hizi ni ishara za kubweka kwa mbwa, akisikia harufu ya simba anafyata mkia. Hainiingii akilini hata kidogo Sendeka anapodai kuwa kumfikisha Mkapa hakuna maslahi kwa Taifa. Sasa kama ni hivyo kwa nini Jeetu Patel, Mgonja, Mramba, Yona na wengine wamepelekwa mbele ya sheria? Si kwamba Mkapa alikuwa hajui kinachoendelea kwenye EPA na UPUPU mwingine waliofanya wakiwa madarakani, alikuwa anajua hizo deals zote. Hapa suala si maslahi ya Taifa bali ni KATIBA. Sheria lazima ichukuwe mkondo. Sendeka acha kubweka na kupulizia, amua uwe MOTO au BARIDI. Huwezi kuwa vuguvugu.
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,544
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Bubu kama ulijuwa ni usanii basi na kichwa cha habari ungebadilisha na useme Sendeke awa kigeu geu.
  Huyu si mlisema ni mzalendo? Angalia anavyojichanganya. Eti hakuna maslahi kwa Taifa kurudisha mali za umma?
  Nasema ni kigeugeu kwasababu anadaiwa kuwavaa wanaowatetea vigogo....Yeye anamtetea nani?
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,440
  Trophy Points: 280
  Yeye anamtetea fisadi mkubwa kuliko wote aliyeshiriki kwenye kila ufisadi nchini kuanzia EPA, ununuzi wa rada, magari, helicopters za jeshi na ndege ya Rais, ukwapuzi wa nyumba za serikali, mikataba fake ya uchimbaji dhahabu, ukwapuzi wa Kiwira, Net Group, Mkataba wa kifisadi wa miaka 20 aliosaini na TANESCO wenye thamani ya shilingi bilioni 340.
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,544
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana BAK...Tungeomba basi na kichwa cha habari kibadilishwe ili kiendane na maudhui...Hapa JF ni lazima tufanye tofauti na "CRUMMY" press kama anavyopenda kusema Kuhani.
  Unakumbuka nilipokuwa nikianzisha thread kipindi cha nyuma na kuipatia heading inayostahili kuendana na habari yenyewe.
  Once again nashukuru sana na ningeshukuru zaidi kama heading ingebadilishwa ili tusipotoshe washabiki na wapenzi wa JF simply kwasababu NIPASHE imefanya hivyo.
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Rasis Mstaafu MH Mkapa ni lazima afikishwe Mahakani kujibu tuhuma za Ubadhirirfu wa Fedha na mali ya Umma akiwa Mtendaji mkuu wa serikali ya Tanzania.

  Hatua ya kumfikisha Ben Mahakamani ni muhimu sana kwa sababu itafungua ukurasa mpya katika Historia ya Tanzania kwamba,wakati wowte ule katika ngazi yeyote ile, hakuna mtu au kikundi cha watu kilicho juu ya sheria.

  Kuna vijiraka vya marekebisho ya sheria vinavyo mlinda Rais Mstaafu lakini havina nguvu ya kuzuia asifikishwe mahakamani kwa makosa ya Jinai alo fanya kama Ben chini ya kivuli cha Urais, au kama Rais huku akijua wazi kwamba anavunja sheria za nchi.

  Rais mstaafu Ben analindwa zaidi na watu wanajipendekeza kwa kutegemea neema fulani kisiasa na kiserikali kuliko sheria ndani ya katiba ya JMT.
  Kundi hili la watu wanaojipendekeza kwa kujifanya wanamlinda Rais kwa nguvu zao zote ndio nguvu kubwa iliyo kaa katikati yetu sisi wananchi na mtuhumiwa wetu namba moja katika Ufisadi MH Ben Mkapa na Mkewe Anna.

  Huyu MH Mbunge Sendeka amefikia hatua ya kumkingia kifua Ben kwa kusema" Kufikisha MH Ben Mahakamani hakuna faida yeyote kitaifa??!!" hii si kwa sababu hajui faida ila ni kwa sababu yeye pia anaamini kwamba nchi itatikisika Ben Mkapa akifikishwa Mahakamani.
  Ili kuonyesha kwamba hatupati nafasi ya kumuinamisha na kumfanya ameze maneno yake mwenyewe kwamba hakuna mtu anaweza kutikisa misingi ya nchi ya Tanzania kwa kufikishwa mahakamani, MH Sendeka ameamua kutumia neno "Maslahi".

  Sielewi vizuri anamaanisha nini kwa kusema hakuna Maslahi!

  MH Kikwete mwenyewe, pamoja na Urais wake hayuko juu ya sheria hata kidogo. Ujuha wa wabunge wetu utokanao na unafiki wa kujikomba ili wajikweze na kunufaisha hamu zao chafu za uroho wa madaraka,dhurma, unyang'anyi, fedha na mali wasiyo itolea jasho, ndivyo vitu vinavyowaziba macho na kudumisha utaratibu wa kumlinda Rais pale afanyapo kosa la jinai.
  Aidha kwa sababu wao ni kizazi kilicho uzao wa Rushwa inayogharamiwa na fedha itokanayo na Ufisadi, na ni watu wanaojali maslahi ya kivikundi kuliko maslahi ya taifa.
  Aidha kwa sababu wengi wa Wabunge wetu ni watu wa hovyo kimaadili, watu wasio jali familia zao, watu wawekao fedha mahali pa mahusiano ya kimwili na kiroho na wake na watoto wao, watu wanaojali miili yao tu na kutojali nafsi na roho zao, watu waziachao roho zao zikiwa uchi katika jukwaa la dharau na manyanyaso makuu, watu wamchao Ibilisi wazi wazi tena kwa gharama kubwa na kumdhihaki Mungu kwa fedha zao za sadaka.
  Wabunge wetu ni sawa na askari wa kukodiwa" Mamruk" wanao pambana vikali kwa faidha ya fedha na siyo utu wao wala utu wa mtu mwingine yeyote.

  Sijui kuna Maslahi gani kumfikisha Yona Mahakamani na kumwacha Mkapa?

  Sijui kuna Maslahi gani ya kumfikisha Mwizi wa kuku kule Kunduchi na kumwacha Mwizi wa Mali ya Umma na mbadhirifu namba moja MH Ben?
  Sijui kuna MAslahi gani MH Sendeka kuchukua muda wake na pumzi yake Kumtetea Mtuhumiwa wa wizi na kiongozi mkuu wa Mafisadi aliye mlinzi wao pia??

  Mslahi? Maslahi au Maskhara?
   
 8. T

  Tofty JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ole Sendeka is such an hypocrite as it's clear from what he is saying that he is one of those "wapambe wa vigogo" ambaye anaongea kwa lengo la kuwakingia kifua hao mafisadi. For once i hope someone from the ruling party would actually mean what he/she is saying when they speak up against mafisadi instead of playing us all for a fool!!!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kundi la mashujaa wa CCM limeanza kuwa kama kinyonga sasa .Kaanza yeye bado kilango na Mwekyembe .EPA na Kagoda ndiyo imeweka serikali iliyo madarakani ni pamoja na wabunge wengi was CCM .Kila jimbo lilikuwa linapewa pesa za kuhakikisha CCM inarudi na wabunge wengi.Sendeka alipewa ngapi ndiyo hatujui labda alipewa milioni kama wengine wachache ambao baadaye wamelia lia kwamba wenzao walipewa 5m na kuendelea wengine 1m.Nasema EPA na Kagoda si JK wala Msekwa na Sitta wako salama hapana.
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapa JF Sendeka alikuwa anajulikana kama "mpiganaji" haya sasa mambo hadharani wengine tuliyaona haya siku nyingi....
   
 11. M

  Mutu JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa ki ungwana kwa kuwa yeye katoa hoja ya kuwa hakuna mtu naye sema makosa ya Ben wazi basi swala ni wanaotaka afikishwe mahakamani wamkumbushe tu makosa yake,thats it! Unajua alichoongea kama mtu hajui makosa ya Ben ni point kubwa sana na analamba hizo point kwa watu milioni nyingi Tz ,sasa atokee mtu ajibu na yeye kwa media .
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Duh! sasa hii noma kidogo I mean labda nimtafute mkulu kwanza kujua hasa kilichojiri maana this is not him kabisa something is not right hapa!

  - Masilahi ya taifa yanaanzia na kuishia hapa, yaani kwenye kumburuza Mkapa Kisutu, sasa kwa nini kina Mramba na Yona wasiachiwe if that is the case? Kwani hawa hawana hela za kutulipa fidia taifa hizo Biilioni 11 tu wanazodaiwa kutuletea hasara ili yaishe tu?

  Tunataka watinge Kisutu na na kulala Rumande Keko, ili kuimarisha utawala wa kuheshimu sheria, na huwezi fanikiwa kwenye hilo bila ya kumfikisha waliyekua wakishirkiana naye yaani kiongozi wao in crime Mkapa, hawa kina Yona na Mramba, ni samaki wadogo sana tunataka the big fish na hatuwezi kukatishwa tamaa na haya maneno ya kutokuwepo kwa masilahi kwa sababu ni pure nonesense na pathetic! Kamata Mkapa buruza Kisutu kama kuna mbunge asiyeona masilahi kwenye hilo akae pembeni sisi tutaendelea mbele mpaka kieleweke, lakini do not give us this masilahi nonesense!
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mutu hakuna cha mtu kujitokeza umesha jitokeza tayari kwenye JF sasa nenda kwenye magazeti au wewe si mtu unataka mtu ajitokeze ?Watu wa JF bwana .Mkiambiwa siasa LIVE ni ngumu mnasema oh Lunyungu nachonga haya .
   
 14. share

  share JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Ili kumtetea Mkapa, kwa madudu anayosakamwa nayo, itabidi uwe na akili kama ya mwendawazimu.
   
 15. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Naomba kutofautiana na wewe nyuzi 180.

  Dai analotoa Mbunge kwamba Tunao dai MH Mkapa afikishwe Mahakamani tumkumbushe makaosa ya mkapa ni suala linalo mdidimiza, kumdharirisha na kumbomoa MH Sendeka.
  MH Sendeka asile H/W yake hapa ili afanyiwe na kupata alama chee.

  Huyu ni mjumbe katika Baraza la kutunga sheria.
  Huyu ni mtu wa watu.
  Huyu ni muwakilishi wa matatizo kero na unyonge wote walio nao wananchi wa Tanzania bila kujali jimbo lake au nani alimteua.
  Sidhani kama ni haki (sheria) kwa mtunga sheria kuja hapa jamvini na hoja hafifu namna hiyo ya kudai kwamba hajui kulikoni.

  MH Sendeka Rejea maelezo ya Kina ya Mbunge wa Moshi vijijini.
  Hata kama ulikuwa umelala fofo pale Bungeni au ulikuwa inajivinjari mitaani wakati wenzio wako Bungeni au ulikuwa na udhuru wowote ule wa maana, ulitakiwa kujua kiacho msibu MH Mkapa badala na kuja na hoja ilo via kiasi hicho.
  Maswali ya nini kinamsibu Mzee Mkapa kiasi kwamba sisi vijana tunataka sheria ichukue Mkondo na kumkumba Babu huyu asiye na huruma hata chembe, babu aliyetetewa wakati wa uchaguzi wa 1995 kwa nguvu zote na Marehemu MWalimu Nyerere kwamba ni mtu safi, kumbe wapi bwana ilikuwa ni nidhamu ya woga na kujipendekeza kwingi kwa ndiyo mzee nyingi,
  yalitakiwa yaulizwe na MH Mbunge siku ile Mbunge wa Moshi Vijijini alipo mtolea uvivu MH Mkapa na Jiko lake pale Bungeni.

  Vinginevyo asituvurugie nia na hamu yetu ya kuwafikisha mafisadi wote mbele ya sheria bila kujali Umri, heshima vyeo,mvi na vipara vyao.

  Tunaheshimu Mvi za mtu kwa kutegemea hekima na busara kutoka kinywani mwake na katika matendo yake. Lakini nathubutu kusema siku hizi kuna baadhi ya mvi zisizostahili heshima hata kidogo, na ukweli usiopingika kwamba vichwa na viwiliwili vilivyobeba mvi hizo kamwe havitakiwi kubaki mitaani na kuvuta hewa safi ya Muumba bure, mahali pao pa kupumzika mpaka uhai uwatoke ni jela tu.

  Hoja ya MH Sendeka inaturudisha nyuma, aidha inatuingiza kwenye mviringo wa hoja unaotulazimu kueleza jambo hilo hilo kila mara.

  Hatuwezi kutekwa kirahisi namna hiyo, hatuwezi kupelekwa alijojo kirahisi namna hiyo. Hii si hoja ya kutufanya tudhani mbunge hajui kulikoni.
  Hizi ni njama za makusudi za kuvuruga uzito wa hoja kwa kutumia dhamana yake kama mbunge na nafasi yake katika jamii na heshima kwa wanao mheshimu ili kwa mara nyingine tena kutufanya wajinga na punda wa dobi.
  Mbunge anajua kinachoendelea ila anajipamba kisiasa ili kujenga hoja itakayo mpa shibe ya kifisadi huko mbeleni kwa kuupa joto ufisadi.

  MH Sendeka hapa hatuko kona zile za Pikadili kule Landani ambako inasemekana watu hutembea kisengerenyuma.

  Usitizingue na wala usitutengulie udhu wetu kwenye hii hoja.

  Hoja hafifu kama hizi kwa kawaida huwa zinawagharimu wote wanaozitoa. Iko siku ambayo haiko mbali kuanzia leo MH Sendeka utameza Maneno yako yote ulosema ikiwa ni pamoja na karatasi iloandikiwa au Wbsite nzima.

  It is extremely expensive.
   
 16. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  WakuuJF
  Yatakuja Masendeka mengi sana mwaka 2009/2010. Tujifunze kuyazoea, kutokukubali yatupotezee mwelekeo. La sivyo tutaanza kujadili Masendeka tuuuu tukasahau wezi na viranja wao ANBEN
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,544
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Humu ndani mnamponda Sendeka..Huko nje(heading) Inamfagilia kuwa kawavaa wanaowatetea vigogo...Ni sawa na kuyakataa mapepo na kumtetea shetani mwenyewe..Ndivyo haswa alivyofanya Sendeka...
   
 18. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa.

  Siyo kila anayepambana na pepo anawafukuza pepo, wengine huingia mkataba wa kifisadi na mapepo na kukugeuza saver ya kudispatch data kwenye terminal nyingine.
  Wacha wamvagilie wanavyotaka wao huko nje lakini sisi tunajua yeye ni mmoja wao kwa sababu kauri yake na za mafisadi zinashabihiana.

  Nyani wa JF anauawa hapahapa JF huko nje wataweka tanga muda ukifika.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,544
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Vichwa vya habari does matter Madilu especially kwenye jamii yetu ya wabongo...Unajuwa tena si kila mwananchi ana uwezo wa kusoma katikati ya mistari kwahiyo heading inaweza ikawa imebeba ujumbe halisi.
  Sasa hapa kuna mada imeletwa ya kumfagilia Sendeka..Ukiingia na kusoma habari yenyewe ni tofauti...Kabla hata hatujaanza ku argue kama ni kivipi kina Mramba wawe na makosa na Mkapa asiwe nayo, tuanze kwanza kujiuliza ni kivipi amewavaa wanaowakingia vigogo kifua...Kwasababu si tuna akili timamu?
  Ama si sawa na kuona mtu anayejidai anajuwa kusoma na huku gazeti kageuza upside down? Ama macho yangu?
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hili la Mkapa litawaendesha watu mbio, ukweli upo wazi lakini siku zote watu wanakuwa wagumu kuukubali. Na Ole ndio kesha toa msimamo wake kuhusu hilo. Mimi nitaheshimu mawazo yake kwani bado yapo sahihi kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
   
Loading...