Sendeka amesimama kuhesabiwa kuhusu Tanganyika


Hoja yako hapo kwenye nyekundu kwa kifupi ni RASILIMALI. Huwezi ukazungumzia rasilimali kama katiba haijakaa vizuri na katiba ina historia yake. Na mojawapo ya historia ya Katiba ya Tanzania ni suala la muungano ambalo halijakaa vizuri. Juzi juzi jamaa wamenusa mafuta huko Zenj wakasema hilo litolewe kwenye mambo ya muungano maana rasilimali hiyo ya mafuta itawafaidia wazenj tu. Mimi naamini matazizo ya watanzania siyo hayo uliyoyaorodhesha hapo juu pekee. Ni pamoja na misingi ya utawala ambayo ni ya kikatiba ambayo inawafanya watawala wetu wawe miungu watu wakijigawia mali zetu wapendavyo nasi tukiendelea kukosa hayo mambo muhimu uliyoyaorodhesha.
 
Hongera mh. Sendeka, huu ni wakati muafaka wa kuelezana ukweli, siasa za vitisho vina mwisho, lazima tuwe na serikali yetu kamili Tanganyika hao wanaopigania muungano kwa maslahi binafsi zao zipo ukingoni, hawana cha kuwaeleza wananchi zaidi kusifia muungano ambao hauna maana yoyote ile kwa watanzania wa kawaida, wazinazibar wengi wanadhana ya kuwa watanganyika tunanufaika na muungano, binafsi sijui nimenufaika nini hadi sasa hawajui kama tumewabeba kwa muda mrefu bila ridhaa yetu, muungano nia yake kubwa ilikuwa ni kuleta umoja kamili kati yetu kama wao hawautaki tunawalazimisha nini?
Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Reactions: Ame
Kwa mbali naiona Mamlaka ya Watu wa Pemba inanukia chini ya P.L.O(Pemba Liberatio Organization).
Sijui kama Jamhuri ya Watu wa Unguja itawavumilia hawa P.L.O.
 
Tupo pamoja.

Kuanza kulipia makaratasi na document upya ni kasheshe.......

Kama UNGUJA hawataki Muungano na Pemba wanataka, basi fukuza Unguja na walete Wapemba hapa.....

Tanzania is here to stay hata kama haitakuwa Jamhuri ya MUUNGANO na ibaki Jamhuri ya Tanzania....
Hapa hatudai Tanganyika, tunataka muungano uvunjwe
 


Tangia tumekuwa na huu Muungano tumefaidika na kitu gani. Hebu tupime kati ya Faida na hasara tulizopata hadi sasa kisha tuamue keundelea ma kuuvunjilia mbali
 
Hapa hatudai Tanganyika, tunataka muungano uvunjwe
muungano uvuvnjwe na tanzania indelee kuwa tz na capital yake dom. visiwa tunavyo vingi ie mafia, ukerewe
kwa hivo kama visiwa viwili vinata kutoka tz viache vitoke
 
muungano uvuvnjwe na tanzania indelee kuwa tz na capital yake dom. visiwa tunavyo vingi ie mafia, ukerewe
kwa hivo kama visiwa viwili vinata kutoka tz viache vitoke

Unafahamu mipaka ya Zanzibar inaishia wapi wewe?
 
Unafahamu mipaka ya Zanzibar inaishia wapi wewe?

Hebu niambie inaishia wapi sifahamu lakini sio zile habari 10 mile strip ya coast ambayo sultan aliachiwa atawale na mkoloni! Sisi tunachotaka ni Tanganyika yetu muungano utavunjika, utabaki sisi hatutaki kujua tunataka Tanganyika yetu irudi. Mungu ibariki Jamhuri ya watu wa Tanganyika
 

Tropical your just a joke,yaani Wazanzibar waishi wapendavyo na wabara waishi kwa hofu ndani ya muungano ,how?
 
Viva Ole Sendeka,watu wako tuko nyuma yako tukikusuport!lazima tuwe nchi tuachane na choko choko za muungano,hazina msaada
 
Hongera Sendeka umesema yaliyoko moyoni mwako sio kufuta upepo.

MOD. TUWEKEE KURA YA MAONI HAPA KUHUSU HUU MUUNGANO WETU
 
hahaa!

ivi unajua uwa najiulizaga kila nikitizama vituko, midomo na sharubu za sendeka.

ivi atumii majani kweli?

Ole Sendeka (Mzee Sendeka) havuti wala kuitumia bangi a.k.a. ngambo kali a.k.a. majani.

Ila wewe inaonyesha unatumia bangi kama si sembe ya afghani. Kwasababu ni mvivu wa kuelewa na mgumu wa kujifunza tena mzito wa kujikosoa/kuliona kosa lako. Ila ni hodari wa ubishi. Hebu angalia kiswahili chako kilivyo kibovu na uj**** wa kushindwa kuandika maneno vizuri. [wana-jF ingie kwenye profile yake halafu angalia kiswahili alichotumia kilivyo kibovu)
 
we lazima mwaka huu mbivu na mbichi za utanganyika na uzanzibar zijulikane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ