Semi Final 2, CECAFA: Zanzibar Heroes yaifunga Uganda goli 2 - 1! Sasa kukutana na Kenya katika mchezo wa fainali

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,471
4,424
Kabumbu lishaanza kupata joto katika dimba la Moi, mjini Kisumu. Ni nusu fainali ya pili kila timu ikisaka kuingia fainali.

Dakika ya 5:
Uganda 0-0 Zanzibar

Dakika ya 25:
Uganda 0-1 Zanzibar

Abdul-Azizi Makame anaitanguliza Zanzibar baada ya kumalizia mpira wa kona.

Dakika ya 30:
Uganda 1-1 Zanzibar

Nsibambi Derrick anaisawazishia Uganda. Mechi ni kali kwelikweli, itazame kupitia Azam Sports 2

Bao la kusawazisha la Uganda likipatikana dakika sita baada ya Zanzibar kutangulia

HT: Uganda 1-1 Zanzibar


58': Uganda 1-2 Zanzibar

Mohamed Issa Banka anaiandikia Zanzibar bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Ibrahim Ahmada kuangushwa ndani ya boks. Wakati huo Uganda wako pungufu baada ya Nsubuga Joseph aliyefanya kitendo hicho kutolewa nje kwa kadi nyekundu.


Mchezo wa nusu fainali kati ya Zanzibar heroes na Uganda unaendelea na ubao mpaka sasa hivi unasomeka, Zanzibar heroes 2-1 Uganda

FULL TIME
Zanzibar heroes 2-1 Uganda
 
Timu ya Taifa ya Zanzibar Leo imefankiwa kuibwaga Timu ya Taifa ya Uganda kwa magoli 2:1 katika muendelezo wa Mashindano ya CECAFA kwenye hatua ya nusu Fainali yanayoendele nchini Kenya
 
3ee2974561e5f62c56b54e7f08c7f062.jpg
Timu ya Zanzibar heroes imelipa kisasi cha Novemba 24, 2015 pale walipofungwa 4-0 na Uganda.

Leo hii Zanzibar heroes imeungana na Kenya kucheza fainali Jumapili baada ya kuichapa Uganda mabao mawili kwa moja katika patashika ya nusu fainali ya michuano ya CECAFA2017

Zanzibar heroes ndo ilikuwa timu ya kwanza kuandisha bao kunako dakika ya 21' lililofungwa na Abdul - Azizi Makame baada ya Ibrahim Ahmada kuwakosakosa na kusababisha kona.

Uganda walisawazisha bao hilo dakika 6 na Nsibambi Derrick, baada ya Zanzibar kutangulia kufunga, sare hiyo ya 1-1 ilidumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Mohamed Issa Banka dakika ya 58 aliiandikia Zanzibar bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Ibrahim Ahmada kuangushwa ndani ya ndani ya 18 na Nsubugu Joseph ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Hadi kufikia dakika 90 za mtanange huo wa nusu fainali ya michuano ya CECAFA2017 Zanzibar heroes 2-1 Uganda na kufanikiwa kutinga fainali.
 
Mwakilishi pekee wa Tanzania aliebaki katika mashindano ya CECAFA, Zanzibar heroes leo amefanikiwa kuuangusha mbuyu mwengine wa soka Afrika Mashariki, The Cranes ya Uganda na kutinga fainali, ambapo sasa ataikabili timu ya taifa ya Kenya ili kuamua mbabe wa soka Afrika Mashariki.
Awali watandaza kabumbu hao wa visiwani waliichakaza kwa vipigo miamba ya soka ya
-Amavubi-Rwanda
-Kili stars - Tanzania bara
na kupoteza dhidi ya Libya
Katika mechi za makundi, Zanzibar heroes walitoka sare na timu ya taifa ya Kenya ambayo wataumana tena katika mechi ya fainali
Kila la heri Zanzibar heroes !!
 
Back
Top Bottom