Sema ukweli wako, ukiona Tsh. 50 mbele yako unaiokota au utaipita kama hujaiona?

Naokota kuanzia 5000 chini ya 5000 siokoti. Zaidi ya mara 3 nimekuwa nikikuta 1000, 2000 imedondoshwa, kama tupo wawili namuonesha mwenzangu aokote, kama nipo peke yangu na kuna mtu nyuma yangu nitamwambia aiokote...Basi tu ni kiformula nilichojiwekea mwenyewe.
hivi nyie wenzangu mna mioyo ya aina gani et?

Hadi Buku unaacha? tuwe tunatembea wote Pyaar
 
kwangu ni tofauti kama niko kwenye daladala nikiona 50, 100, nk nampa konda. mtaani nikiona hiyo pesa namwacha niliye nae aokote kama niko mwenyewe siokoti. mara kibao tu natoka kwenda zoezi jioni barabarani naona 100, 200 nk wala sihangaiki nazo. juzi nikiwa zoezi asubuhi njiani niliokota simu hizi ndogo, kwa kweli hiyo niliokota japo kuna mwana nimemwachia pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
simu umemwachia mwana au umemuazima atumie kisha akurudishie mkuu?
 
Nmecheka hapo ulipofika kwenye 5000 na 10000 nilijua utaendelea ku flow

kama ulivyoanza mwanzo,mimi nakuombea wiki hii ukutane nazo uje utupe

mrejesho ila kwanini huokoti hizo coin zingine,unajiskiaje ukiokota au unajionaje?

Huwa sijiskii tu amani kufanya hivo.
 
Kwa nini nisiokote, sema wewe unabahati maana wengine hata hizo hamsini siku hizi hatuzioni.
 
Kuna 50 moja imeanguka chumbani karibu na mlangoni toka juzi Mimi na wife tunaipita tuu.. hata watoto wakija kusalimia asubuhi wanaipita tuu.. sijui kwa nn. Sa HV nimeona huu Uzi Niko mbali na home nikaikumbuka.
 
Jana nilienda mahali na rafiki angu mmoja hivi,sasa tulipofika huko tulipoenda wakati nmeshuka tu kwenye gari chini nikaona sh.50 "nikaiokota" kisha nikwamwambia mwanangu, "ndugu yangu leo siku yangu itakua safi sana nimeokota hela" akaniuliza sh.ngapi? nikamjibu sh.50..

akanicheka kwa dharau,si unajua ile cheko kisha akaniambia "hebu nione hiyo 50" nikampa alipoishika akairusha mbali kbsa yani aliitupa kisha akaniambia "acha wenye shida nayo waiokote wewe unabania riziki za watu"..

kusema la ukweli sikupenda nilinuna nikamwambia mwanangu naomba sh 50 yangu,akaniambia chukua 5000 akanipa noti ya 5000 kwakweli nilichukua ile 5000 ila bado moyoni mwangu nilikua nawaza ile sh.50 yangu iliyotupwa.

Hii si mara yangu ya kwanza mimi kuokota sh.50 na sh.100 kusema ukweli tokea moyoni mimi nikiziona hizi coin huwa naziokota kisha natia mfukoni,siwazi mara mbili wewe nichukulie utavyoncukulia ila ndio hvyo...

Haya leo sema ukweli na wewe ukiona sh.50 utaiokota au huikoti? au ilishawahi kuku kuta upo kwenye dala dala mtu anakwambia "kaka umedondosha hela yako" kuangalia chini unakuta n sh 50,halafu ile 50 si yako unajua kbsa hii si yangu,Huwa unafanyaje? unaichukua au huichukui?

Natamani watu mseme ukweli tu leo...


Mimi naokota na ninaitia mfukoni, lakini kama ni ndani ya daladala na nimeambiwa nimeangusha ela na hiyo ela siyo yangu basi nitasema hiyo sio ela yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom