Sema ukweli mara zote, utapendwa

Sema ukweli mara zote, utapendwa

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,231
SEMA UKWELI MARA ZOTE, UTAPENDWA
Maneno ya ukweli hayabembelezi...
Na maneno yanayobembeleza sio ya kweli...
Hivyo ni wajibu kwako kuchagua, unataka kutoa maneno ya kubembeleza au unataka kutoa maneno ya kweli?
Ukitoa maneno ya kweli, watu hawatapendezwa, na wanaweza kukuchukia, ila ni kwa muda tu. Baadaye wataelewa, kwa sababu ukweli huwa haujifichi kwa muda mrefu. Baada ya muda utafahamika na wewe utakuwa umesaidia.
Ukitoa maneno ya kubembeleza, watu watafurahia na wanaweza kukupenda, ila ni kwa muda tu. Baadaye ukweli utafahamika, na hapa watu watakuchukia kwa sababu hukuwaambia ukweli tangu mwanzo, huenda wangechukua hatua mapema, na mambo yasingekuwa mabaya.
Japo hufanyi ili kupendwa au kuchukiwa na watu, japo huhitaji kujali kama ni nani anakupenda au kukuchukia, mara zote sema ukweli, hata kama ni mchungu kiasi gani, hakuna kilicho bora zaidi ya ukweli. Mery Christmas and happy new year.
 
Back
Top Bottom