Sema kweli katika upendo na mwenzi wako.

Jpinduzi

Senior Member
Feb 26, 2011
136
68
Imekuwa kama kawaida kusema uongo baina ya wapendanao pasipo kujali madhara yake!Basi uvueni uongo mkaseme kweli kila mtu na jirani yake....tushike kweli katika upendo na kukua.Jirani wa kwanza ni mume au mke wako.Ili ndoa idumu na kukua na pia kuendelea vizuri sema kweli katika upendo wa mwenzi wako.Kusema kweli katika upendo,kunasaidia kuondoa jazba,ghazabu ,hasira na hatimaye mabishano na magomvi yanayozaliwa na hayo.Uchungu wote na ghazabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu pamoja na kila namna ya ubaya(EFE 4:31). Jiepushe na mabishano,ubishi katika ndoa huleta uchungu na kujenga chuki baina yenu pia na jamii yako.
 
Hivi vitu hufundishwi humu jf, unafundishwa kwenu, hapa ni kukumbushana tu.

Asante mtoa thuredi
 
Inategemea!kuna mida na wakati inakulazimu kusema uongo walau kunusuru ndoa/uhusiano!but not all time unatakiwa uwe hivyo!uongo ni muhimu pia kudumisha mapenzi.
 
Imekuwa kama kawaida kusema uongo baina ya wapendanao pasipo kujali madhara yake!Basi uvueni uongo mkaseme kweli kila mtu na jirani yake....tushike kweli katika upendo na kukua.Jirani wa kwanza ni mume au mke wako.Ili ndoa idumu na kukua na pia kuendelea vizuri sema kweli katika upendo wa mwenzi wako.Kusema kweli katika upendo,kunasaidia kuondoa jazba,ghazabu ,hasira na hatimaye mabishano na magomvi yanayozaliwa na hayo.Uchungu wote na ghazabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu pamoja na kila namna ya ubaya(EFE 4:31). Jiepushe na mabishano,ubishi katika ndoa huleta uchungu na kujenga chuki baina yenu pia na jamii yako.
haleeluyaah!!
 
Back
Top Bottom