Kuachwa kuachwa
Kuachwa ni shughuli pevu
Mbaya zaidi kwa yule uliye mpenda
Wewe una geuka mwana mashairi
Pluss presha na kuponda
Yeye Yuko bize, Wana mgonga
Nimpate vipi mi sijui
Nina imani mapenzi hayajui
Nitapata ugonjwa wa moyo
Kwa sababu ya mawazo
Ninavyo jua maisha yake
Hajawahi kuwa na boyfriend
Ila ni mimi wa kwanza
Na ninashindwa kumpata
Kwa ishara naonekana nampenda
Yeye eti mi namzingua
Eti kama angilikua anasikia
Basi ukweli wangu angeujua
Kwa ishara naoneka nampenda
Yeye eti mi namzingua
Eti kama angelikua anasikia
Basi ukweli wangu angeujua
Ningemzowea rafiki yake
Basi mi ningemtuma
Ningezitambua ishara zake
Kwake mi ningefika
Ningemzowea rafiki yake
Basi ningemtuma
Ningezitambua ishara zake
Kwake mi ningefika
Sicilia ninampenda
(Binti kiziwi)
Moyo wangu wamtaka
(Binti kiziwi)
Sicilia nateseka juu yake
(Yeye binti Kiziwi)
Sicilia ninampenda
(Binti kiziwi)
Moyo wangu wamtaka
(Binti kiziwi)
Kichwa kinauma mawazo
(Kwake binti kiziwi)
Nashangaa pale napomkuta
Akiwa na wenzake wanaongea
Huwa najiuliza mimi
Wanaongea naye vipi
Nashangaa pale napomuita
Nahisi huwa anakataa
Sijui ndio hasikii
Au mapozi au mapozi naye
Afadhari angejua kusoma
Hata hatari ujumbe ningempa
Eti kama ningejua ishara
Basi kwake ningefika mimi
Afadhari angejua kusoma
Hata bonge ujumbe ningempa
Eti kama ningejua inshara
Basi kwake ningefika baby