Selfika na JF: Snap it. Show it

Asante Mwenyezi Mungu kwa kutupa siku nyingine tena nzuri

Tunawaombea wenye shida mbali mbali za kimwili na za kiroho pia
Ugonjwa na taabu
Wasafirio nchi kavu, angani na baharini
Yatima, wajane na wasiojiweza pia
Nyoosha mkono wako wa baraka,nyoosha mkojo wako wa ulinzi ukatuongoze kutubariki na kutulinda katika mema yote... Aaamen
 
Amen!!🙏
Mungu ni mwema!
 
Amen
 
Traders exhibition!!
Sure!
Siku kuu hii mpaka inakuwa ya wafanyabiashara kwa kweli tumetoka mbali.
-7 july kuzaliwa kwa tanu 1954, hapa ndipo ilizaliwa saba saba.

-1963 Saba Saba ikawa public holiday baada ya Tanganyika kuingia rasmi mfumo wa chama kimoja.

-1967 TANU inatangaza itikadi ya ujamaa kama siasa rasmi hapa Saba saba ikawa siku ya wakulima na wafanyakazi.
-1977 CCm inazaliwa kwa muungano wa TANU na ASP saba saba inabadilishwa inakuwa siku ya wakulima.

-1992 mfumo wa vyama vingi unaingia na Tanzania inafuta siku kuu ya saba saba, 1993 inaanzishwa nane nane kama siku kuu ya wakulima.

-1994 kunatokea sintofahamu mara baada ya baadhi ya wafanya kazi kutofika kazini kwa kuendelea kusheherekea siku ya saba saba.

-Baadae serikali inairudisha tena saba saba kama siku kuu ya wafanya biashara.

Tumetoka mbali sana kwa kweli.
 
Mnooo!!
Asee Uko vizure pilot ✌️!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…