Mkandara,
Unaweza kuwa sahihi kwamba RA hata angepelekewa polisi bado angekataa kuhojiwa lakini pia huwezi kujua ukweli bila kujaribu.
Kwa mhusika mkuu kama inavyoonyesha sasa kwenye baadhi ya taarifa, mimi naamini ingekuwa busara kuomba amri ya bunge kumhoji RA baada ya kukataa kuitikia ombi la kwanza.
Sio kwasababu akina RA hawafuati sheria basi na sisi tunaojifanya ni waumini sheria tuamue kupambana nao kwa kukiuka sheria hizo hizo.
Ushahidi wa kiapo wa RA ungelikuwa muhimu mno.
Lakini kikubwa zaidi ifike mahali tuachane na mambo ya Richmond na kusonga mbele. Kama tumeshindwa kuwafunga wahalifu ni bora tukakubali ukweli huo. Lakini kama kuna njia zingine za kuwawajibisha basi zifanyike haraka. Tumepoteza muda mrefu mno kujadili jambo moja huku wananchi wanaendelea kuteseka kwa matatizo mbalimbali. Maamuzi ya wanasiasa wanawajibika wakati wa kura. Kama JK ameshindwa kumshughulikia RA basi kilichobaki ni kumshitaki kwa wapiga kura mwaka 2010. Huu mduara imefika mahali imekuwa sanaa, inafurahisha macho na masikio yetu lakini haumwongezei tija Mtanzania wa kawaida.
hivi hii nchi ina vyama vya upinzani kweli? au wapo tu wanatolea macho hela za ruzuku ndio maana kila mtu anakuja na chama chake kila siku? kuwa na chama cha siasa umekua mtaji sasa badala kuja kupigania mabadiriko ndani ya nchi.kila kitu kipo wazi no actions.vyama vya upinzani vina uwezo wa kumpa changa moto raisi mpaka hatua zichukuliwe na hapo sisi wananchi tutapata nguvu ya kuwaunga mkono.lakini huu mchezo wa kila siku mambo yanafanyika na tunapiga gumzo tu na siku zinakwenda ndio maana tunafuga viongozi wa ajabu mpaka leo.majina yale yale serikalini yanazunguka tu.
kama raisi anaogopa kuchukua hatua baada kupewa ushaidi kwanini aliangaika kuomba tume iundwe ya kufanya uchunguzi?
hii kazi inatakiwa ifanywe na serikali baada ya kupewa report na maamuzi ya bunge sasa lawama zozote ni vizuri ukazipeleka kunako husika, serikali kwa kushindwa kutumia madaraka, nguvu na haki za kufanya hivyo. serikali ina takukuru, usalama wa taifa, polisi na mahakama. ukiwa kiongozi mzuri sema ukaletewa report na takukuru iliyo na ulakini utamrudishia aliye kuletea pamoja na point unazo taka zifuatiliwe. hivyo mapungufu yote yapo juu ya serikali.Nemesis,
Hapana, mimi niliridhishwa sana na report ya Mwakyembe na hata ukiangalia mijadala yote ya huko nyuma utaona hilo. Tatizo langu kwasasa ni hizi taarifa mpya zinazotoka na ambazo mimi naziita ni missed opportunity kwasababu laiti zingefuatiliwa zaidi huenda tungekuwa tumeukata mzizi wa fitina wa akina RA kimoja.
Kama RA ndiye kweli pesa zililipwa kwake na mpaka hata kufuatilia hizo pesa hazina, mbona ingekuwa busara kumhoji na kupata ushahidi wake kisha kupendekeza apelekwe mahakamani? Matatizo mengi tunayokumbana nayo sasa ni kwasababu ya hiyo missed opportunity.
Kuna jamaa aliwahi kusema wakati mzuri wa kulinda sheria ni pale zinapomuokoa mbaya wako. Unapo deal na watu ambao kwa njia moja ama nyingine kunaweza kuwa na tofauti zenu, inabidi kuwa makini kuhakikisha wanapewa kila opportunity ya kujitetea. Hata mimi naamini wakati mzuri wa kuitetea sheria ni pale inapomuokoa mbaya wako.
Mtanzania, yote hayo nakubaliana nawe. Hata hivyo kuna jambo moja ambalo naona umeliruka... nalo ni nia ya hawa wahujumu uchumi. Lengo lao kubwa hivi sasa ni kujisafisha kwa hayo maovu kwa uwezo na mbinu zozote wanazoweza. Na kibaya zaidi ni nia yao ya kujisafisha kwa lengo la kuwaharibia wote waliowafichua na kuwaanika hadharani. Maelezo ya Mh. Selleli yanaonesha nia yao hii. Tumeshindwa kuwafikisha lupango, sawa, lakini kamwe tusiwaruhusu waonekane ni kondoo weupe machoni pa jamii.
SteveD,
Aliyehukumiwa atajisafisha vipi kama hakuna kukata rufaa? Lowassa na RA wamehukumiwa, hata mijadala ya Richmond ikiisha sidhani kama wana nafasi ya kujisafisha. Labda sisi wananchi wenyewe tuamue tu kwamba tumewasamehe.
Mimi kusema wacha twende mbele ni kwa pande zote mbili wakiwemo hao watuhumiwa. Walikuwa na miaka mitatu ya kujitetea na kama hawajasafishika sidhani kama itasaidia kitu hata kama huu mjadala ukijadiliwa miaka 10.
Hili suala lote linaangukia kwa rais maana bunge hata lifanye nini, haliwezi kuilazimisha serikali kufuata mapendekezo yao yote. Labda waamue kupiga kura ya kutoikuwa na imani na serikali na kuitisha uchaguzi mwingine kitu ambacho nina wasiwasi kama wabunge wana guts hizo.
Mkuu wangu historia ya maovu haina muda, tutavieleza hata vijukuu vyetu na itaendelea hivyo hivyo kujadili mabaya ya Ufisadi kuliko kuyakubali yaishe..kwa kila hatua na kila atakayekumbuka jambo.. Hata wale walioficha mwanzoni kwa hofu ya Utawala, tutayapokea mawazo yao.Mimi kusema wacha twende mbele ni kwa pande zote mbili wakiwemo hao watuhumiwa. Walikuwa na miaka mitatu ya kujitetea na kama hawajasafishika sidhani kama itasaidia kitu hata kama huu mjadala ukijadiliwa miaka 10.
SteveD,
Mkuu wangu mimi huwa siachi vitu vikielea hadi ijulikane. Wayahudi walikuwa watumwa miaka zaidi ya 1000 huko Soiuth Kutawaliwa zaidi ya miaka 500 lakini wazo la kujikomboa lilikuwepo kila siku yan maisha yao pamoja na kwamba mambo mengine yaliendelea. Kusema tusahau ni kukubali kushindwa na hatuwezi kusogea mbele hata kidogo...Mawazo ya Mtanzania ni mawazo ya mkata tamaa ambaye anaona botra liende ndio kilichobakia.
tatizo lako ni gharama gani badala ya kuangalia maradha gani yanatokea... Ndio hayo ya samaki Sangara..Mkuu Ya Chiluba yaligharimu UsD 13m lakini wameponyesha billioni nyingine...unatazama karibu sana mkuu wangu.Mkandara,
Kwenye management kuna kitu kinaitwa SATISFICING, ni uamuzi wako kufukuzia optimum ambayo haikamatiki au kukubali adequacy ambayo ni achievable. Ukiniuliza mimi nitachagua the later, hata kama utaniita ni mkata tamaa.
Tumeona ya akina Chiluba dola $13m kutumika kufukuzia case ya laki tano. Nikipewa chaguo, nitazitumia hizo $13m kujenga shule au hospitali kuliko kumfukuzia mtu mmoja ambaye hata sina uhakika wa kumfunga.
Nadhani itafikia wakati inabidi tuchague watu wa kuwajibu au kuwaelimisha.
Bob, angalia wewe na Bubu ataka kusema msije mkawa mnapoteza muda wenu bure. Angalia unajadiliana na nani.
Mkuu FMES,
Nikija kwenye point yako, nitashukuru ukinitafutia paragraph inayoongelea masuala ya pesa za Richmond kuingia kwenye account za kampuni za RA na yeye mwenyewe kufuatilia hizo pesa hazina. Mimi sijaiona na nitakuwa happy kusahihishwa kwa facts.
Mkandara,
Kwenye management kuna kitu kinaitwa SATISFICING, ni uamuzi wako kufukuzia optimum ambayo haikamatiki au kukubali adequacy ambayo ni achievable. Ukiniuliza mimi nitachagua the later, hata kama utaniita ni mkata tamaa.
Tumeona ya akina Chiluba dola $13m kutumika kufukuzia case ya laki tano. Nikipewa chaguo, nitazitumia hizo $13m kujenga shule au hospitali kuliko kumfukuzia mtu mmoja ambaye hata sina uhakika wa kumfunga.
Mkandara,tatizo lako ni gharama gani badala ya kuangalia maradha gani yanatokea... Ndio hayo ya samaki Sangara..Mkuu Ya Chiluba yaligharimu UsD 13m lakini wameponyesha billioni nyingine...unatazama karibu sana mkuu wangu.
Well thats You kwa sababu nijuavyo mimi upo upande wa makaburu (CCM)hivyo ni vigumu sana kwako kuelewa harakati na machungu ya wananchi..
Nemesis,
Kama RA ndiye kweli pesa zililipwa kwake na mpaka hata kufuatilia hizo pesa hazina, mbona ingekuwa busara kumhoji na kupata ushahidi wake kisha kupendekeza apelekwe mahakamani? Matatizo mengi tunayokumbana nayo sasa ni kwasababu ya hiyo missed opportunity.
inabidi kuwa makini kuhakikisha wanapewa kila opportunity ya kujitetea. Hata mimi naamini wakati mzuri wa kuitetea sheria ni pale inapomuokoa mbaya wako.
lowasa haku-hukumiwa report ilisema ajipime mwenyewe kama mtu mwenye busara na kiongozi wa serikali.SteveD,
Aliyehukumiwa atajisafisha vipi kama hakuna kukata rufaa? Lowassa na RA wamehukumiwa, hata mijadala ya Richmond ikiisha sidhani kama wana nafasi ya kujisafisha. Labda sisi wananchi wenyewe tuamue tu kwamba tumewasamehe.
Mimi kusema wacha twende mbele ni kwa pande zote mbili wakiwemo hao watuhumiwa. Walikuwa na miaka mitatu ya kujitetea na kama hawajasafishika sidhani kama itasaidia kitu hata kama huu mjadala ukijadiliwa miaka 10.
Hili suala lote linaangukia kwa rais maana bunge hata lifanye nini, haliwezi kuilazimisha serikali kufuata mapendekezo yao yote. Labda waamue kupiga kura ya kutoikuwa na imani na serikali na kuitisha uchaguzi mwingine kitu ambacho nina wasiwasi kama wabunge wana guts hizo.
Mtanzania, hapa ndipo hapo academic management ya kikampuni au kibiashara inatofautiana na management katika mambo ya siasa. Kwenye siasa na uongozi kitaifa kuna sovereignty, usawa, haki, freedom na uzalendo. Mambo haya hayanunuliki au kuwa mambo ya pick and mix kwa ajili ya kumaximize profit. Hapana mkuu. Naikubali kabisa technique hii as applied in management books lakini si katika kutunza hadhi ya Taifa. Ukifata hiyo kwenye siasa, utauzwa na kuishia kuwa mtumwa.
Kwa mfano wako wa Chilluba, je ungelipenda tuwafungulie wahalifu kutoka jela kwa vile tunaweza kusave pesa nyingi? Katika hili mimi nachoose kuwa masikini jeuri lakini haki inakuwa imetendeka.
Mkuu haya unazungumza kwenye nchi yenye SHERIA. Hatufanani katu ni mbingu na ardhi.SteveD,
Hapana, sio kwenye makampuni tu bali hata serikali. Mfano ni hapa UK kwenye money for peerages na Blair. Kulikuwa na ushahidi lakini prosecutor akaona uwezo wa kushinda ni mdogo, akaamua kuiachia case.
Hicho ndio ninachoongelea mimi, ni tofauti na kuwaachia wahalifu ambao wamehukumiwa au kutumia pesa nyingi kumhukumu na kumfunga mhalifu. Kama unaona uwezo wa kumfunga ni mdogo, ni bora kutumia hizo pesa kwenye mambo ya maana.
Kama tumekubali suala la akina RA mwamuzi ni JK, ifike mahali tumwachie yeye na sisi wananchi tutoe hukumu yetu 2010.