Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,484
- 40,012
hili ni mojawapo ya maswali ambayo bado sijapata majibu yake kwa hakika. Mara nyingi tumeona jinsi sekta binafsi (makampuni kadha wa kadha na watu binafsi) wakiunga mkono chama tawala aidha kwa kukichangia au kwa kujiunga nacho au kushiriki katika miradi yake bila hofu yoyote ile wakiamini ni haki yao ya kidemokrasia.
Tumeona makampuni yakitoa misaada kwa wabunge wa chama tawala bila wasiwasi wowote wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo wanatimiza jukumuu lao la kiraia (civic duty).
Hivyo utaona kampuni kama Zain inaenda kutoa misaada ya vitabu kwa mbunge wa CCM huko Mbozi, au kampuni nyingine ikitoa misaada inayohusisha wanasiasa wa chama tawala.
Lakini kitu kimoja kinachokosekana sana ni makampuni makubwa na yenye ujiko kuunga mkono upinzani au jitihada za wapinzani. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikiangalia kuona kampuni kama Zain, Vodacom, IPP, Quality Group n.k zikienda kwenye majimbo ya wapinzani na wakisimama pamoja na wabunge wa upinzani kutoa misaada ya aina mbalimbali au kudhamini shughuli zao.
Sijaona kama CUF wakiandaa kongamano lao pale Arusha kampuni kama TBL itakuwa tayari kuzamini, au kampuni kama NSSF kujitangaza pale kibiashara au kuvutia wanachama zaidi.
Hivyo naanza kujiuliza kuna ubaya gani kwa makampuni makubwa kuonekana na wapinzani kama kwa kufanya hivyo kutatangaza makampuni hayo, kuwapatia wateja wengi na kuonesha kuwa hazina mlengo fulani wa kisiasa?
Je kampuni binafsi au mtu binafsi mwenye uwezo wa kifedha au kibiashara akionekana anaunga mkono chama cha upinzani waziwazi kuna tatizo gani katika utawala wakati tunajua wafanyabiashara wengi wakubwa tu wamekuwa wakiunga mkono CCM pasipo kificho?
Je ni kwanini hakuna wafanyabiashara wakubwa ambao wamejitokeza kujiunga na chama chochote cha upinzani kwa wazi (ukiondoa wachache ambao wamefanya hivyo hadi hivi sasa).
Kimsingi ninachouliza ni kuwa; je ni wazo zuri kwa sekta binafsi kuonekana wanasupport, kufagilia au kwa namna ya wazi kabisa kuunga mkono juhudi za upinzani kuibwaga CCM?