CCMDiwani wa Sekei ni Chama gani?
Anaitwa nani?
Nimetoka kibaruani hapa sasa hivi naambiwa kuna mchango wa lazima tshs 20,000 kuchangia sijui shule tena nikajulishwa kuwa sasa hivi imebadirika imekuwa elfu 70, kitu kilichonisikitisha zaidi nimeambiwa kwamba wale wote waliokutwa majumbani mwao leo hawana hiyo hela wamebebewa vitu vyao kama tv,deki n.k kufidia mchango wa lazima wa elfu 20,000 .Naomba kama kuna kiongozi yeyote wa serikali alitolee ufafanuzi hili maana mbaya zaidi wapangaji ndio walioipata adha hii
Diwani wa Sekei mi wa CHADEMA anaitwa Mheshimiwa Deus Kessy. Ila eneo linalolalamikiwa halipo kata ya Sekei bali kata ya Kiutu.Diwani wa Sekei ni Chama gani?
wewe usizungumze vitu usivyovijua mimi sina utaahira wa ubongo hadi nije kuropoka jambo lisilona ukweli kama umetumwa uje ukanushe ni bora ukaja sekei kuanzia maeneo ya idara ya maji na sehemu za muungano ufanye upate majibu maana ni familia nyingi zimekutwa na balaa hiloPamoja na kwamba kuna vitu umedanganya ili kuongeza chumvi na hivyo kutimiza dhamira yako, nakujulisha hakuna mchango wa namna hiyo bila wananchi wenyewe kupitisha kwenye vikao vyao.
Nakushauri uliza mikutano uliyokuwa unaitwa na kuingia mitini iliamua nini?
Huu ni uoga kiwango cha professor!!! Na ndio watanzania wengi walivyo.Kwani maeneo hayo ulipo hakuna viongozi wa SERIKALI au wa kwenu wapo humu JF?
Huu ni uoga kiwango cha professor!!! Na ndio watanzania wengi walivyo.Kwani maeneo hayo ulipo hakuna viongozi wa SERIKALI au wa kwenu wapo humu JF?
Diwani wa kata ya kiutu anaitwa nani na ni chama gani?Diwani wa Sekei mi wa CHADEMA anaitwa Mheshimiwa Deus Kessy. Ila eneo linalolalamikiwa halipo kata ya Sekei bali kata ya Kiutu.
Mchango huu ni wa halali kabisa kuchangia maendeleo na vikao vya tangu mwaka Jana 2017 vilishaamua mchango uwepo. Mwenyekiti wa kijijini Sekei mheshimiwa Daniel Sambu Sagiraki amefanya kazi kubwa kuhamasisha maendeleo haya.
Tuwaunge mkono viongozi na kama hukutoa 20,000 ndani ya muda uliowekwa basi lipa tu hio elfu 70 na faini.
Na ujifunze kuhudhuria vikao/mikutano ya kijiji