Seif Sharif Hamad: Leo Nilifika Gereza la Segerea Kuwajulia Hali Mhe. Freeman Mbowe na Esther Matiko Wako Imara sana na Hawatarudi Nyuma

Leo tarehe 29 Desemba, 2018 nilifika gereza la Segerea kwenda kuwatembelea na kuwafariji Mhe. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, na Mhe. Esther Matiko, Mbunge. Nimewakuta wote wawili wako imara na hawana wasiwasi kuwa haki itaishinda dhulma inayotendwa na watawala dhidi yao.

Nimeitumia fursa ya kuonana na Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Esther Matiko kuwaeleza kuhusu #AzimiolaZanzibar na mikakati ya vyama sita vya siasa kurudisha demokrasia Tanzania. Mhe. Mbowe amenambia yuko pamoja na sisi na akitoka tu gerezani ataungana nasi kuendeleza atakapopakutia.



View attachment 980465
Wewe Sharrif gani wewe? Hatujakusikia hata siku moja kuwatembelea Masheikh wa Zanzibar waliorundikwa segerea huko bila sababu.

Eti leo unamtembelea Mbowe. Khaa, Mpemba na Wachagga wapi na wapi?

Mnafik tu huna lolote.
 
Chanzo cha mauaji ya Akwilina ni maandamano ya CHADEMA, hiyo ndio source kuu.. Risasi ilipigwa kuwatawanya waandamanaji wasio na kibali yaani maandamano haramu yalio ongozwa na akina Mbowe na Co.. na katika kuwatawanya risasi ilimpata Akwilina sbb ya maandamano yasiyo na kibali.. So Mbowe anatakiwa kujibu hilo na kasema gerezani yuko imara sana kuliko alivyokuwa uraiani.. Sasa kumbe nia yake ilikuwa kuwa aende gerezani, na kheri akae huko huko miaka yote ili awe imara zaidi... Alime mboga mboga na kukamua ng'ombe magereza.. Merry Xmass & Happy New Year 2019
Ahaa kumbe risasi hutumika kutawanya maandamano? Ina maana hujui kisheria, kikatiba na kimataifa ni vitu gani hutumika kutawanya maandamano? Je walipoandamana walikuwa na silaha mpaka itumike risasi ya moto? Jivikene uziwi ila haya yakiendelea mtego wa panya utawahusu waliomo na wasiokuwemo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom