Zitto Kabwe: Salamu nyingi kutoka kwa Mhe. Mbowe na Matiko, nimewaona leo gerezani Segerea

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
"Salamu nyingi kutoka kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe na dada yetu Esther Matiko nimewaona leo gerezani Segerea na wapo na ari kubwa ya kuendelea na mapambano ya kulinda Demokrasia ya nchi yetu.

Nimemueleza juhudi tunazochukua dhidi ya muswada kandamizi wa Vyama. Amefarijika sana.

Mwenyekiti Freeman Mbowe na Mbunge Esther Matiko, wanatusihi kuendelea na mshikamano dhidi ya kukandamizaji wa haki, uonevu na utawala wa imla.

Nikiwa pamoja na Ado Shaibu, tumewahakikishia viongozi wenzetu kuendeleza mshikamano mpaka tushinde udikteta, ukatili na ukandamizaji nchini".

Ameandika Mhe. Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Twitter.
 
Asante mkuu Mungu atawalinda na hila zote
 
Back
Top Bottom