Seif na Mbowe wakipikwa chungu kimoja wanaiva

Baraghash

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Posts
2,713
Reaction score
1,790
Ukiwafuatilia wanasiasa hawa wawili kwa ukaribu utagundua kuwa wanafanana sana kiasi ambacho kama hata wakipikwa chungu kimoja basi bado watabaki na ladha ileile ya kulika.

1 Wote wanayoyahubiri hawawezi kuyatekeleza - Kutojiamini
2.Wote ni vigeugeu,leo wanasema hili kesho wanasema lile kuhusu kitu hichohicho - Unafiki
3.Wote wana maamuzi ya kukurupuka- hawasikilizi ushauri - toka bungeni/ susia uchaguzi. Leo yanawatafuna

Kule Zanzibar jeshi la polisi limeshamuelewa Maalim Seif na hawapati taabu ya kumdhibiti wala polisi hawahitaji kufanya mazoezi ya kijeshi mitaani kila siku. Wanamuacha kupayuka tu. The barking dog doesn't bite!

Huku bara jeshi la polisi bado halijamsoma, laiti kama wangemjua MBOWE kuwa kama ni Mun'gunye, nje gumu ndani laini, wasingejitia hasara nchi nzima ya kujiandaa na UKUTA wakijua kuwa umesimamishwa kwa nyasi tupu na kupambwa kwa kuzungushiwa vitambaa vya bendera .

Mbowe sasa anatafuta sababu nyepesi ya kufuta mikutano ya hadhara na maandamano ikiwa tu jeshi la polisi litacheza karata zake vizuri.
 
Sio kweli kabisa, wanafanana kwa sababu wote wako upinzani tu
 
Lengo la ccm ni kukiua chama cha cuf ili mdai ya seif kuporwa ushindi yakose nguvu kama chama kikifa na znz itaanza kupokea misaada
 
Mbowe na Maalim Seif wanafanana kwasababu uongozi wao ni upinzani wakweli sio wa kutumwa na ccm kama Lipumba.
 
Huyo mfuasi wa lipumba hana lolote.

hii thread ya kinafiki namwandishi wake mnafiki.
 
Hebu thibitisha Unafiki, ukurupukaji, kutokujiamini na kukataaushauri kwa Mbowe
1 Wote wanayoyahubiri hawawezi kuyatekeleza - Kutojiamini - Maandamano ya Sept anaya pigia chapuo za kiaina ili yasifanyike na hayafanyiki
2.Ni kigeugeu,leo anasema hili kesho anasema lile kuhusu kitu hichohicho - Unafiki leo huyu fisadi kesho msafi
3.Wote wana maamuzi ya kukurupuka- hawasikilizi ushauri - toka bungeni/ susia vikao Sasa analilia suluhu
4. kumsaliti Katibu mkuu wake mkuu,mbachao,Dk Willibrod Slaa kwa msala upitao
5 Ameufanya uongozi mzima wa chadema uwe kama kambare, wote wana masharubu.
 
Ni sawa na serikali ya ccm na raisi jinsi wanavyotoa matamko ya kupishana.ZAA WATOTO ULIKUWA NI UTANI.

WAMACHINGA.HATUKUMUELEWA RAIS....swissme
 
Ukiwafuatilia wanasiasa hawa wawili kwa ukaribu utagundua kuwa wanafanana sana kiasi ambacho kama hata wakipikwa chungu kimoja basi bado watabaki na ladha ileile ya kulika.

1 Wote wanayoyahubiri hawawezi kuyatekeleza - Kutojiamini
2.Wote ni vigeugeu,leo wanasema hili kesho wanasema lile kuhusu kitu hichohicho - Unafiki
3.Wote wana maamuzi ya kukurupuka- hawasikilizi ushauri - toka bungeni/ susia uchaguzi. Leo yanawatafuna

Kule Zanzibar jeshi la polisi limeshamuelewa Maalim Seif na hawapati taabu ya kumdhibiti wala polisi hawahitaji kufanya mazoezi ya kijeshi mitaani kila siku. Wanamuacha kupayuka tu. The barking dog doesn't bite!

Huku bara jeshi la polisi bado halijamsoma, laiti kama wangemjua MBOWE kuwa kama ni Mun'gunye, nje gumu ndani laini, wasingejitia hasara nchi nzima ya kujiandaa na UKUTA wakijua kuwa umesimamishwa kwa nyasi tupu na kupambwa kwa kuzungushiwa vitambaa vya bendera .

Mbowe sasa anatafuta sababu nyepesi ya kufuta mikutano ya hadhara na maandamano ikiwa tu jeshi la polisi litacheza karata zake vizuri.
usituletee giza kwenye mwanga wetu wewe.
 
Hoja za kutafuta kiki upuuzi mtupu; msifie JPM utapata kiki na ukuu wa kata.
 
1 Wote wanayoyahubiri hawawezi kuyatekeleza - Kutojiamini - Maandamano ya Sept anaya pigia chapuo za kiaina ili yasifanyike na hayafanyiki
2.Ni kigeugeu,leo anasema hili kesho anasema lile kuhusu kitu hichohicho - Unafiki leo huyu fisadi kesho msafi
3.Wote wana maamuzi ya kukurupuka- hawasikilizi ushauri - toka bungeni/ susia vikao Sasa analilia suluhu
4. kumsaliti Katibu mkuu wake mkuu,mbachao,Dk Willibrod Slaa kwa msala upitao
5 Ameufanya uongozi mzima wa chadema uwe kama kambare, wote wana masharubu.

Hamna cha maana unachoongea zaidi ya kukariri na kufata mkumbo tu, acha dhana kaka uwe na fact

Hayo yote unayoyasema hapo hajaamua Mbowe bali chama kiliamua kwa vikao vyao rasmi
 
Kwanini tuandikie mate wakati wino upo! Tarehe 01 Sept sio mbali. Mbowe atakuja na kisababu hafifu cha kuahirisha mikutano. Hapo ndipo utakaposadiki utafakari wangu.
 
Kaka shirikisha ubongo wako basi kwa unachokiandika, kwa nini unamtenga Mbowe na Chama?, Kauli anayoitoa mbowe inakuwa iko na baraka za Prof Safari, Prof Baregu, Tindu Lisi, Mwalim Salim, Mnyika nk, kwa kifupi ni kauli ya chama
 
Kaka shirikisha ubongo wako basi kwa unachokiandika, kwa nini unamtenga Mbowe na Chama?,
Nimeipenda; waswahili wanasema, mla kuku wa mwenziwe miguu humuelekea.Kama kauli yako ni sahihi wakati wa kumkaribisha Lowassa mbona Mbowe, hata Katibu mkuu wa chama chake Dr.Slaa,hakumuhusisha mbali na hao uliowataja?
 
Kaka wewe uko Dunia gani? katibu mkuu ndio alileta proposal ya kumkaribisha Lowassa ndani ya Chama, alikuja kutofautiana na wenzie kwenye jinsi ya kumpokea huyo Lowassa, majority walikubali na tulichokioma na kutangaziwa

So hayakuwa maamuzi ya Mbowe yalikuwa ya chama na yeye Mbowe kama Mwenyekiti alikuwa msemaji wa hayo maazimio
 
Back
Top Bottom