Sehemu ya pili Resistori: Jifunze electronis, umeme online

Sehemu ya pili Resistori: Jifunze electronis, umeme online

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,640
JIFUNZE KUHUSU RESISTOR​
Resistor ambapo katika saketi huwa na alama ya "R" ni kifaa cha umeme ambacho kinafanya kazi ya kupunguza mtiliriko wa umeme katika saketi ya umeme.
Resistor hutumika pia kupitisha kiwango maalumu cha voltage kinacho ingia katika vifaa hai kama vile transistor.
Kazi kuu ya resistor katika saketi ni "kukinza" au "resist" ndipo ikapatikana jina kikinzani au resistor,kazi yake kuu ni kukinza mtiririko wa electrons katika saketi.
Resistor ni kifaa "mfu" (passive) ambacho hakizalishi nguvu wala hakiongezi nguvu.Kifaa hiki hupunguza nguvu ya umeme kwa kuibadilisha kuwa joto,kifaa hiki kina miguu miwili sehemu ya kuingilia umeme na sehemu ya kutokea umeme.
Mguu wowote unaweza kuingiza au kutoa umeme, kifaa hiki kinaweza kufungwa mfatano au sambamba na saketi ya umeme.
Mwonekano wa resistor ya kawaida.
res38a.jpg

Na alama za resistor katika saketi ya umeme huonekana hivi.
res6.gif

UHUSIANO OULIOPO KATI YA CURRENT NA RESISTANCE​
Mtiririko wa umeme(current) mara zote katika saketi ya umeme huwa kinyume ukinzani (resistance)
Ukinzani ukiongezeka current inapungua,ukinzani ukipungua current inaongezeka (Current through a resistor is inversely proportional to its resistance.)
UHUSIANO OULIOPO KATI YA VOLTAGE NA RESISTANCE​
Msukumo wa umeme(voltage) mara zote katika saketi ya umeme huongezeka ama kupungua kutokana na kuongezeka ama kupungua kwa ukinzani(resistance).
Voltage ikiongezeka ukinzani utaongezeka voltage ikipungua ukinzani utapungua.( Resistance is directly proportional to the voltage across it).
AINA ZA RESISTOR​
Resistor zipo za aina nyingi utofauti huu katika aina hizi umetokana na aina ya madini yalio tumika kuitengeneza rsesistor husika.hivyo utofauti huu hauathiri chochote sheria ya OHM.
1. Carbon Composition Resistor – Imetengenezwa kwa carbon dust au graphite paste, hutumika katika vifaa vinavyotumia nguvu kidogo.Na resistor hiyo ni kama hii.
res39a.jpg

Hivi ndivyo ilivyo tengenezwa kwa ndani
res1.gif

2. Film or Cermet Resistor – Imetengenezwa kwa conductive metal oxide paste, Hutumika katika vifaa ambavyo vinatumia nguvu kidogo sana.

res40a.jpg

Hivi ndivyo ilivyo tengenezwa kwa ndani
res2.gif


3. Wire-wound Resistor – Hutengenezwa kwa wire na cover la chuma kwa ajili ya kupooza joto, Hutumika katika vifaa vinavyotumia nguvu kubwa.
res41a.jpg

Hivi ndivyo ilivyo tengenezwa kwa ndani

res3.gif

4. Semiconductor Resistor – Imeundwa kwa thin film technology,hubandikwa katika sakafu ya saketi.Ni resistor ndogo sana kiumbo.
index.jpegooooooooo.jpeg





VIPIMO VYA RESISTOR​
Resistor inapimwa katika kipimo cha OHM kuanzia 0Ω hadi 1000000Ω

1kilo ohms = 1000 Ohms
1000 kilo ohms = 1mega ohms
1Mega ohms = 1000000 ohms

RANGI ZA RESISTOR​
Ukinzani wa resistor unatambuliwa kutokana na rangi zake.rangi hizi husimama kuwakilisha thamani Fulani ya ukinzani.
capture-20150709-225932.png




Kuna resistor zina idadi ya rangi nne,tano na nyingine sita.


capture-20150709-235014.png


​
NAMNA YA KUTAMBUA THAMANI YA RESISTOR YENYE RANGI NNE​
Thamani ya rangi ya kwanza inaandikwa kama ilivyo.Mfamo Nyekundu itakua 2
Thamani ya rangi ya pili inaandikwa kama ilivyo.mfano Njano itakuwa 4
Thamani ya rangi ya tatu inatumika kama zidishio mfano kama rangi ya tatu itakua nyekundu,na thamani ya nyekundu ni 2,hivyo mbili itageuka kuwa sifuri mbili yaani 00.
Thamani ya rangi ya nne ni fedha vumilivu itakuwa 10%

Hivyo resistor hii itakuwa hivi 242=2400 Ohms na uvumilivu 10%

Ambapo itaandikwa 2400Ω 10% ili kuibadilisha iwe katika kipimo cha Kilo-Ohm itabidi uigawanye kwa 1000,hivyo resistor hiyo hapo juu itaandikwa hivi.

2.4kΩ 10%
NAMNA YA KUTAMBUA THAMANI YA RESISTOR YENYE RANGI TANO​
-Thamani ya rangi ya kwanza inaandikwa kama ilivyo.Mfamo Nyekundu itakua 2

-Thamani ya rangi ya pili inaandikwa kama ilivyo.mfano Njano itakuwa 4

-Thamani ya rangi ya tatu inatumika kama zidishio mfano kama rangi ya tatu itakua nyekundu,na thamani ya nyekundu ni 2,hivyo mbili itageuka kuwa sifuri mbili yaani 00.

-Thamani ya rangi ya nne pia inatumika kama zidishio mfano kama rangi ya nne itakua chungwa,na thamani ya chungwa ni 3,hivyo tatu itageuka kuwa sifuri tatu yaani 000.


Thamani ya rangi ya tano ni fedha vumilivu itakuwa 10%

Hivyo resistor hii itakuwa hivi 242=2400000 Ohms na uvumilivu 10%

Ambapo itaandikwa 2400000Ω 10% ili kuibadilisha iwe katika kipimo cha Kilo-Ohm itabidi uigawanye kwa 1000,hivyo resistor hiyo hapo juu itaandikwa hivi.

2400kΩ 10%
NAMNA YA KUTAMBUA THAMANI YA RESISTOR YENYE RANGI SITA​
Resistor yenye rangi sita usomaji wake ni sawa na ile yenye rangi tano,tofauti yake ile langi ya sita huelezea temperature cofficience.kama itakavyo onekana katika chart.

Waweza kuwasiliana na mimi 0657-115587


CHANZO: Electronic Darasa
 
Back
Top Bottom