Sehemu nne za kunasa wateja mtandaoni 2021

Badmantebwe

New Member
Sep 23, 2017
3
18
kama unafanya biashara yoyote basi wateja ni muhimu kwako, makala hii inakupa sehemu nne za kupata wateja mtandaoni na mbinu za kunasa wateja kwenye vyanzo hivyo
Hii ni kwa wafanyabiashara,wamiliki wa blogs na wamiliki wa mitandao(tovuti)

makala hii inakupa vyanzo vinne vya kupata watembeleaji na wateja mtandaoni na mbinu za kunasa watembeleaji kutoka vyanzo husikia.
Vyanzo vyenyewe ni kama vifuatavyo

1. Google search
2. Facebook
3. Youtube
4. Instagram


GOOGLE SEARCH: Ni mfumo wa kutafutia taarifa fulani mtandaoni, google ndiyo tovuti inayoongoza kwa kutembelewa zaidi ya mara bilioni 40 kila mwezi.

1-p-g-300x225.png
google inakuwezesha kunasa wateja na watembeleaji wwanaotafuta huduma au bidhaa yako
hapa Tanzania google ndiyo inayoongoza kutembelewa zaidi kwavile watu wanatumia google kutafuta taarifa na kuuliza maswali.

Google inafanyaje kazi:google inafanyakazi kwa mtindo wa kuchukua taarifa toka kwenye blogs na tovuti za watu kisha kumletea hizo taarifa mtu anayezitafuta.
Kazi ya google ni kukuonesha taarifa unayoitafuta inapatikana wapi mtandaoni mfano ukitafuta neno “gari nzuri “basi google itachakata tovuti na blog zote zinazohusu magari kisha itaziletea ambazo zina majibu ya kitu ulichotafuta.

Namna ya kupata watembeleaji toka google
Njia ya bure

, unaweza kupata watembeleaji bure toka google iwapo kama google itaonesha blog au tovuti yako juu kwenye majibu, kwa mfano blog yako ni ya mziki mtu akienda kutafuta nyimbo Fulani ambayo ipo kwenye blog yako basi google wakiweka blog yako juu kwenye search result basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata watembeleaji wengi.

JE, NIFANYAJE ILI BLOG YANGU ITOKEE KWENYE GOOGLE?

Ili blog yako itokee kwenye google yakupasa ufanye SEO (search engine optimization) ambacho ni kitendo cha kufanya blog yako iendane na matakwa ya google
Namna ya kufanya SEO ( kwa ufupi)
1. Wasilisha blog yako kwenye google search console.
2. Wasilisha sitemap yako kwenye search console
3. Andika post nyingi (zaidi ya ishirini)
4. Hakikisha blog yako inafunguka haraka (speed)
5. Hakikisha unaweka tags na meta description kwenye kila post
6. Hakikisha link zinafunguka vizuri na blog iko active muda wote.
7. Andika post ndefu zinazovutia wasomaji
8. Unganisha blog yako na site za google

9.hakikisha blog zingine zinalink blog yako (backlinks) ili upande ngazi kwenye google

NJIA YA KULIPIA: kupitia google adwords (huduma ya matangazo ya google) inakuwezesha kupata watembeleaji toka google kwa vile google ukilipia kwenye adwords basi google wataiweka blog yako juu pale mtu anapo search neon husika ambalo pia linahusiana na blog yako, google watakukata pesa yako kulingana na idadi ya watemebelaji ( wateja utakaopata)

ANGALIZO!: kupata watembeleaji toka google kunahitaji hatua za msingi zilizoelezwa hapo juu lakini huchukua muda mrefu mpaka blog yako ianze kuonekana google.

FACEBOOK: huu ni mtandao wa pili kutembelewa zaidi Tanzania, hivyo ni fursa kubwa ya kupata watembeleaji kwa ajili ya blog yako au wateja kwa ajili ya biashara yako. Facebook ni mtandao wa kijamii ambao watu hutumia kuchapisha na kusambaza picha na video zao kwa watu wao wa karibu na dunia kwa ujumla.
Mbinu ya kupata watembeleaji kupitia facebook.

1-p-f-300x229.png
facebook inakuwezesha kunasa wateja na watembeleaji kwa gharama nafuu
Njia ya bure: njia hii inakuonesha namna gani unaweza kupata watembeleaji kwa urahisi na bure kabisa kutoka facebook , njia hii utatumia vikundi na kurasa za facebook.
1. Jiunge vikundi vya kutosha vinavyoendana na aina ya blog au biashara yako mfano kama blog yako ni ya mziki basi jiunge makundi ya mziki na wasanii au kama unauza urembo basi jiunge makundi (magroup) ya urembo
2. Follow (like) kurasa nyingi zinazoendana na blog yako
3. Post kwenye vikundi: kuipromote blog / website yako huku ukiambatanisha link yako
4. Sambaza post zako kwenye facebook groups
5. Comment na reply comment kwenye posts facebook pages.

Njia ya kulipa: ili u promote biashara na blog yako facebook inatakiwa uwe na page ya biashara ambayo utaitumia kwa kulipia (ku boost) post zako ziwafikie watu wengi, kwahiyo kupitia page yako ya facebook utaweza kulipia ili tangazo au post yako husikia kuruhusu blog na biashara yako iwafikie watu wengi.
 
Back
Top Bottom