Sehemu kubwa ya ongezeko la mshahara kwa wafanyazi kurudi serikalini kwa njia ya tozo benki

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Kama kweli waziri wa fedha amesaini kuanza kutumika kwa tozo kwa miamala ya kuweka au kutoa fedha ATM na benki, kwa mtazamo mwingine ni kuwa fedha ya ongezeko la mshahara sehemu kubwa kama sio yote itarudi serikalini kama tozo, kwa sababu ulipaji mishahara hasa wa wafanyakazi wa serikalini lazima upitie benki.

Kwa vyovyote vile mfanyakazi arudishe fedha hiyo kama tozo ya kutolea, hizi ni failure kwa wizara na inaleta malalamiko ya wananchi. Watu bado wanajiuliza inakuwaje TRA inajinasibu kukusanya kwa kuvunja rekodi, halafu bado vyanzo kama hivi vinaanzishwa inashangaza.
 
winnie-the-pooh-pooh.gif
 
ongezeko la mshahara sehemu kubwa kama sio yote itarudi serikalini kama tozo kwa sababu ulipaji mishahara hasa wa wafanyakazi wa serikali lazima upitie benki.
Hivi serikali itakapokuwa inatumia mishahara ya watumishi wake kupitia benki nayo itakatwa ama makato yatakuwa kwa mtumishi.

Nauliza hivi kwa sababu serikali haimiliki Benki ambazo watumishi Karibu wote wanapokelea mishahara!!!
 
Solution hiyo hapo
 

Attachments

  • BINANCE PAY KWA WATANZANIA WOTE1.pdf
    402.9 KB · Views: 7
Magufuli aliwahi kusema 'nikipandisha mishahara kutatokea kupanda kwa gharama za maisha' haya sasa mwanamama Mwakatozo anaonyesha kwa vitendo.
 
Kaka kwakweli ,NI aibu Kwa taifa,linalojinadi Lina wajali watu wake. Huwezi kumkata mfanyakazi Payee,,halafu uende ukamkate tena TOZO. Kwakweli Mwiliguru alisema tuhamie Kongo,tukampuuzia. Alimaanisha.
 
Hata masurufu ndio hivyo hivyo.
Ukisafiri kikazi mara nyingi unaambia ujilipie nauli ukifika huko utarudishiwa nauli yako baada ya kuonyesha tiketi na risiti za taxi.
Ukifika unapewa nauli yako ya kuendea, yakurudia mpaka urudi utume tiketi ndio ulipwe kwa njia ya tigo pesa/mpesa/Airtel mone etc.
Gharama za kutolea hawakutilii
 
Mwigulu hana ubunifu wowote wa Kuona vyanzo tele wa kupata pesa nje ya kodi, tozo na kukopa.
 
Back
Top Bottom