Sehemu gani ya nchi hii nitapata shughuli za vibaru?

Asante kwa kushare mkuu, vp hawahitaji uzoefu wowote kwa shughuli hiyo?
Hawahitaji uzoefu, nguvu ndio mtaji wako mkubwa pia hakikisha husumbuliwi na matatizo ya kifua maana kg25 kupanda nazo kileleni sio kazi ndogo ukizingatia kadri unavyokwenda juu hewa inakua nzito kidogo.
 
Unaweza kwenda moshi/Kilimanjaro ukifika pale moshi mjini ulizia ofisi za Ahsante tours ukifika waombe kazi ya uportal upandishe watalii mlimani lakini hata ukifika pale moshi ulizia unapoweza kupata connection ya maporta then kajichanganye najua utapata hela ya kula uanze maisha mdogo Mdogo baada ya mda ujichanganye na maeneo ya Arusha najua channel zitakua zimefunguka.
Portal=Porter(s)
Kiswahili wanaitwa wapagazi
Kiswahili kisicho rasmi wagumu
 
Nenda Lindi au mtwara kuna kazi za kulimia mikorosho ukimaliza vipo vbarua vya kuokota korosho na kama afya iko poa nenda TPA mtwara kuna vibarua vya kubeba magunia ya korosho
 
Nenda Lindi au mtwara kuna kazi za kulimia mikorosho ukimaliza vipo vbarua vya kuokota korosho na kama afya iko poa nenda TPA mtwara kuna vibarua vya kubeba magunia ya korosho
Shukrani kwa taarifa mkuu
 
Kuna kambi kubwa inajengwa na kilosa wanajenga ya waturuki kwa ajili ya wafanyakazi wa reli ya standard gauge. Iko poa na wageni wanaingia kilosa kufata ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kambi kubwa inajengwa na kilosa wanajenga ya waturuki kwa ajili ya wafanyakazi wa reli ya standard gauge. Iko poa na wageni wanaingia kilosa kufata ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu bila shaka una uenyeji maeneo hayo, tafadhali tujulishe mpk sasa aina ya vibarua ipatikanayo hapo ili tusijefunga safari tukakosa nauli za kurudi.
 
Back
Top Bottom