Sehemu gani ya kuangalia Cinema Mbeya?!

ha ha ha!!! cinemax mbeya hakuna, ila kuna vibanda umiza video show. nenda kwa Eria video show pale kwenye soko la mwambene, chonicho video show kule uyole, paskari video show uyole, juma video show uyole na kule mwenge video show
 
wachawi sana ho jamaa wana nyungo kila nyumba
ume-generalize sana, Mbeya kuna watumishi wa Mungu kama mashehe na Mapdri nao waweza kua wachawi?, ni nani huyo ambaye amewahi kufanikiwa kukagua nyungo majumba yote Mbeya?.
 
Nimefika Mbeya kikazi sasa kesho nataka pata nafasi kuangalia fate of the furious,je kuna sehemu naweza pata huduma hiyo?
Mbeya hakuna hiyo. Ila unaweza tumia muda huo kwa kufanya utalii wa ndani, kwa kupanda mlima Loleza, kwenda tazama kimondo, kwenda tazama ziwa ngozi, kwenda Ngonga Beach Kyela au Matema beach, kwenda tembelea mipaka ya Kasumulu au Tunduma, kwenda kitulo, kwenda hifadhi ndogo ya wanyama Ifisi, kwenda uporoto Kuona kilimo cha viazi mviringo nk... Wasalim sana Mbeya mkuu.
 
Back
Top Bottom