Sehemu gani ya karibu naweza kusajilia line ya Safaricom

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
[SUP]Wadau kama mnavyojua kizazi hiki kimesheheni fursa kibao za mtandaoni ikiambatanishwa na urahisi wa kutuma na kupokea pesa.[/SUP]

[SUP]Ila kwa bahati mbaya Tanzania tupo nyuma sana yani kwa lugha nyepesi bado tumelala usingizi mzito.[/SUP]

[SUP]Huenda makampuni mengi yalikuwa tayari kuanzisha mifumo rahisi na salama ya kupokea pesa ukiwa humu nchini lakini bado kuna longolongo nyingi sana huko BOT wao wakiwa wana uhakika wa kupokea mishahara minono ila huku mtaani wametuwekea vikwazo sana kwa kutoweza kupokea pesa kutoka nje ya nchi.[/SUP]

[SUP]Leo hii Paypal naweza kusema ndio imekuwa kama M-Pesa ya dunia, ni salama na rahisi kutumika lakini hadi leo hii 2020 Tanzania imeshindwa kutupia jicho katika hii ishu.[/SUP]

[SUP]Wenzetu Kenya naona walishaamka, Mtandao wa simu wa safari com unaruhusu kufanya miamala na kupokea pesa kwa njia nyingi sana ila kwa chache zinazokubalika sana ni Paypal na Skrill.[/SUP]

[SUP]Sasa naombeni tujuzane ndugu zangu ni sehemu gani naweza kupata line ya safaricom kihalali kabisa bila zile janja janja za kusajiliwa na vitambulisho feki, majina feki, n.k[/SUP]


[SUP]Nawasilisha[/SUP]
 
Back
Top Bottom