Nakumbuka kipindi kile nimemaliza chuo sina dili, nipo mtaani nacheza draft na karata tu... Nimetuma maombi hadi nikachoka. Jamaa yangu akaniambia kuna kazi fresh tu nipeleke vyeti, nikaulamba na vyeti vyangu mkononi huyo hadi Knight support pale Victoria. Kufika nikapigwa pigwa maswali ila nikaambiwa sababu sijawahi pitia mafunzo yoyote ya kijeshi au mgambo inabidi nianze kama mlinzi then baada ya miezi mitatu narudishwa ofisini kwenye professional yangu
Nikawaza weeee nikaona haina noma, mwanaume nikachapa mazoezi you wiki tatu mfululizo kama nipo jeshini vile, baada ya kumaliza wakati wa mkataba naona 150,000 kula, nauli juu yako na eneo la kazi nimepangiwa kabisa. Nikafumba macho na degree yangu nikasema liwalo na liwe elimu kitu gani. Ila Mungu acha aitwe Mungu tu kabla sijatia sahihi na kuripoti kituo cha kazi, simu ikaita naitwa kazini shirika moja hivi safiiii... Weeee furaha yake acha tu, ungekuta na mie mlinzi sehemu fulani
Hadi leo huwa sidharau walinzi, baada ya kubaini mie na elimu yangu nilikua naenda kushika kirungu then probably wapo wasomi walinzi ila sababu ya ukosefu wa ajira wamejishikiza huko.
Unaweza mdharau mlinzi leo sababu hujui elimu yake halafu kesho unamkuta ofisi safiiii anapigwa kiyoyozi ukahisi uchawi au kawekwa kindugu kumbe sio
Respect kwa wana wote wapambanaji
Nikaw