Security guards na umuhimu wao

Security guards na umuhimu wao

Tata ya bana

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2018
Posts
304
Reaction score
369
Je ushawaza unapita getini kuingia kazini kwako unampita mlinzi kama mti,unamuona kama hajasoma vile,ila kampuni ikifa ni yeye pekee atabaki pale.vilevile maslahi yao ni ya ovyo sana.hebu tudiscuss umuhimu wao
 
Kuna Makamguni Mengine Ya Ulinzi Wako Smart Sana Na Zana Zao Ni Imara. Makampuni Mengine Yanaokoteza Walinzi Na Kuwalipa Mshahara Wa Hovyo Sana, Walinzi Wamevaa Sare Zimechakaa.
 
Wana sifa sana hawa wakujitolea,nawachukia kinyama
Unachuki na walinzi kwani ukifuata taratibu au uwe kwako watakufuata?

Hatuna kawaida ya kuheshimu walinzi wanajeshi na polisi wanaogopwa kwa kuwa wanatoa vichapo mchakato wa kumtia hatiani ni mrefu.
 
Kadri unavokuwa na elimu ndogo basi ndivo na kazi yako itakuwa ya kudharaulika(za kuajiliwa).
Walinzi n watu muhimu tatzo nao wanakuwaga wakorofi na hawana ubinadamu kabisa mda mwingine.
Unamzuia mtu getini chuoni na anawahi mtihani kisa hajabeba id.
 
Hivi unaweza kutoa hela benki ukiwa huna ATM card?
Moja ya kazi yao ni kusimamia usalama wa shule kama umesahau ID yako rudi ukaichukuwe.
 
Kampuni za ulinzi zina changamoto hasa hizi za ndani,kuna jamaa yangu alipewa kazi,akapewa na shati LA kampuni akaambiwa akatafute suruali nyeusi na boot nyeusi.salary 140000.nimkashauri akauze mtumba kuliko hii kazi.nilimchangia 20000.ss ana kitambi
 
Nakumbuka kipindi kile nimemaliza chuo sina dili, nipo mtaani nacheza draft na karata tu... Nimetuma maombi hadi nikachoka. Jamaa yangu akaniambia kuna kazi fresh tu nipeleke vyeti, nikaulamba na vyeti vyangu mkononi huyo hadi Knight support pale Victoria. Kufika nikapigwa pigwa maswali ila nikaambiwa sababu sijawahi pitia mafunzo yoyote ya kijeshi au mgambo inabidi nianze kama mlinzi then baada ya miezi mitatu narudishwa ofisini kwenye professional yangu

Nikawaza weeee nikaona haina noma, mwanaume nikachapa mazoezi you wiki tatu mfululizo kama nipo jeshini vile, baada ya kumaliza wakati wa mkataba naona 150,000 kula, nauli juu yako na eneo la kazi nimepangiwa kabisa. Nikafumba macho na degree yangu nikasema liwalo na liwe elimu kitu gani. Ila Mungu acha aitwe Mungu tu kabla sijatia sahihi na kuripoti kituo cha kazi, simu ikaita naitwa kazini shirika moja hivi safiiii... Weeee furaha yake acha tu, ungekuta na mie mlinzi sehemu fulani

Hadi leo huwa sidharau walinzi, baada ya kubaini mie na elimu yangu nilikua naenda kushika kirungu then probably wapo wasomi walinzi ila sababu ya ukosefu wa ajira wamejishikiza huko.

Unaweza mdharau mlinzi leo sababu hujui elimu yake halafu kesho unamkuta ofisi safiiii anapigwa kiyoyozi ukahisi uchawi au kawekwa kindugu kumbe sio

Respect kwa wana wote wapambanaji

Nikaw
 
Aisee

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Hawa watu wana thamami na ni muhimu kuliko tunavyodhani.
I've made it a habit sio tu kazini kwangu hata kwenye ofisi za watu nikiingia getini nikamkuta mlinzi ninamsalimia (kwa umri wake either shkamoo au habari) kisha nampa pole kwa kazi na nikiwa natoka nahakikisha kumuaga "kazi njema, jioni njema".
Walinzi ni moja kati ya watu wanaodharauliwa sana sehemu za kazi lakini ukifikiria kua na yeye ni baba /mama wa familia yuko hapo kutafuta riziki alishe, asomeshe au auguze familia basi ni vema kumchukulia kama yule unaemkuta ndani anazunguka kwenye kiyoyozi.
After all maisha yao yapo hatarini kwasabu lolote likitokea yeye ndio yupo front line. Kazi kubwaaaa na risky kwa mshahara mdogo pengine ndo per diem yako kwa siku.
Kuna sehemu nilikua nafanya kazi na moja ya majukumu yangu ilikua kusimamia junior staff (walinzi wakiwepo). Nilianzisha utaratibu wa kuhakikisha jioni walinzi wanapatiwa birika ya kuchemshia chai, mkate, sukari, maziwa, majani etc... kutokana na mazingira ya kazi baridi na kutokua na nafasi ya kwenda kula akiwa lindoni. Naweza kusema ni kitu kidg lakini ni moja kati ya vitu vilivyoniwekea heshima .
Je utapoteza dakika ngapi au sh.ngapi kumsalimia na kumtakia kazi njema????
 
This is what we call a matured mind, a very high level of maturity... In life we depend each other so we have to respect each other despite of the educational and financial gaps we have, that's how life is
 
inavyosemekana wamiliki wa kampuni wana sign pesa nzuri sana kwa kila mlinzi kwa makampuni wanayokubaliana kulinda,si chini ya 800k maana yanapigwa mahesabu ya vitu mbalimbali,ila sasa inaposhuka mpaka kufikia 140k hapo ndio havieleweki.
 
Hawa watu wana thamami na ni muhimu kuliko tunavyodhani.
I've made it a habit sio tu kazini kwangu hata kwenye ofisi za watu nikiingia getini nikamkuta mlinzi ninamsalimia (kwa umri wake either shkamoo au habari) kisha nampa pole kwa kazi na nikiwa natoka nahakikisha kumuaga "kazi njema, jioni njema".
Walinzi ni moja kati ya watu wanaodharauliwa sana sehemu za kazi lakini ukifikiria kua na yeye ni baba /mama wa familia yuko hapo kutafuta riziki alishe, asomeshe au auguze familia basi ni vema kumchukulia kama yule unaemkuta ndani anazunguka kwenye kiyoyozi.
After all maisha yao yapo hatarini kwasabu lolote likitokea yeye ndio yupo front line. Kazi kubwaaaa na risky kwa mshahara mdogo pengine ndo per diem yako kwa siku.
Kuna sehemu nilikua nafanya kazi na moja ya majukumu yangu ilikua kusimamia junior staff (walinzi wakiwepo). Nilianzisha utaratibu wa kuhakikisha jioni walinzi wanapatiwa birika ya kuchemshia chai, mkate, sukari, maziwa, majani etc... kutokana na mazingira ya kazi baridi na kutokua na nafasi ya kwenda kula akiwa lindoni. Naweza kusema ni kitu kidg lakini ni moja kati ya vitu vilivyoniwekea heshima .
Je utapoteza dakika ngapi au sh.ngapi kumsalimia na kumtakia kazi njema????
Hongera yako mkuu.
 
Back
Top Bottom