Second selection Kidato cha Tano 2015/2016

Second selection Kidato cha Tano 2015/2016

ALU255

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
2,089
Reaction score
2,125
1.0. UTEUZI KIDATO CHA 5 – AWAMU YA PILI 2015
Ufaulu wa watahiniwa Kidato cha Nne kwa mwaka 2014 kuanzia daraja la Distinction hadi Credit yaani GPA ya 5.0 hadi 1.6 ni watahiniwa 73,754 wakiwemo wasichana 27,680 na wavulana 46,074 sawa na asilimia 37.48 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 ni jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wavulana 31,700 na wasichana 23,303. Aidha, wanafunzi waliochaguliwa na kujiunga na vyuo vya Ufundi ni 479 wakiwemo wavulana 332 na wasichana 147.

Matokeo ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2015 yalitangazwa tarehe 30/6/2015. Wanafunzi wote walitakiwa kuripoti shuleni kuanzia tarehe 18/7/2015. Tarehe ya mwisho ya kuripoti ilikuwa ni tarehe 31/7/2015.

Hata hivyo kulitokea maombi mengi ya kubadili shule/tahasusi. Maombi hayo yalishughulikiwa kwa kuzingatia kutojaza baadhi ya shule na nyingine kuwa wazi. Baada ya mabadiliko haya bado kulikuwa na maombi mengine ambayo yalihusu kubadili shule/tahasusi ndani ya Mkoa au Halmashauri. OWM-TAMISEMI iliwaandikia barua Makatibu Tawala wa Mikoa kushughulikia maombi yaliyoko ndani ya mikoa yao.

2.0 .HALI ILIVYO HADI SASA
Hadi sasa jumla ya wanafunzi 8,945 wameshapatiwa fursa ya masomo ambapo jumla ya wanafunzi 8,822 wamepangiwa kusomea ualimu UDOM. Kati yao wanafunzi 7,042 watasoma SCIENCE, MATHEMATICS AND ICT(Dip, Ed SMICT) na wanafunzi 1,780 watasoma Ordinary Diploma in Primary Teacher Education (ODPE). Aidha jumla ya wanafunzi 123 wamechaguliwa kujiunga na shule mpya ya serikali ya St. Peter's Liuli iliyopo Halmashauri ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma iliyopata usajili Julai 2015. Wanafunzi hawa ni wa tahasusi za HGL na HKL. Bado wanafunzi 9,806 hawajapata fursa ya kuchaguliwa.

OWM TAMISEMI imewaandikia barua Makatibu Tawala wa mikoa ya kuwataka kuwasilisha idadi ya wanafunzi ambao hawajaripoti kwenye shule zilizoko kwenye mikoa yao kwa kila tahasusi. Tayari baadhi ya mikoa imeanza kuwasilisha taarifa za wanafunzi wasioripoti. Baada ya kupokea taarifa hizi kutoka mikoa yote, second selection kwa wanafunzi waliobakia itafanyika tarehe 30/8/2015 - 2/9/2015. Watakaochaguliwa watatangazwa pamoja na tarehe ya kuripoti shuleni. Utaratibu utawekwa wa kufidia siku ambazo hawakusoma kwa kutumia siku za mapumziko mafupi (mid term) na muda mwingine muafaka.
 
iv mbona walisema kuwa ili m2 uweze kwenda 5 lazma uwe na C3 na kuendelea so vp hawa wenzetu waliopata daraja la PASS coz unakuta m2 ana C4 NA D3 inakuaje hapo?
 
iv mbona walisema kuwa ili m2 uweze kwenda 5 lazma uwe na C3 na kuendelea so vp hawa wenzetu waliopata daraja la PASS coz unakuta m2 ana C4 NA D3 inakuaje hapo?

hiyo inawezekana kwa private ila kwa gvt uwe kuanzia C3 na uwe umepata daraja credit hadi distinction
 
Nauliza kuwa 1.5 wenye wameachwa kabisa kujiunga na chuo chochote cha serikari mfano mimi bios c chem c geog c phy d afya chuo siendi
 
Nauliza kuwa 1.5 wenye wameachwa kabisa kujiunga na chuo chochote cha serikari mfano mimi bios c chem c geog c phy d afya chuo siendi

hapo chuo cha afya unaenda lakini mpaka u apply au ulijaza chuo 1st katika selform?
 
serikali imeshughulika na wale waliopata kuanzia 1.6 so below hapo watafute private

me nilidownload information zao zilizohusu upangaji wa wanafunzi kidato cha tano walieza kuwa wataanza na madaraja ya credit mpaka dinstriction..
Then nikaona wameandika tena kuwa unatakiwa uwe na C3 "bila kujali daraja"(umeelewaje hayo maneno) alilopata mwanafunzi na vipaumbele vitatolewa kwa wenye shida maalumu.,kwa wanafunzi wa hisabati na technologia pamoja na michepuo ya sayance... Ndio hayo 2 mkuu
 
nafasi zinatolewa kwa ushindani yani kuanzia gpa kubwa hadi ndogo so inategemea na nafasi zilizopo kama wenye gpa kubwa watakuwa wameisha ina maana hapo watafuata hata wenye pass ambao comb balanced kama zitakuwepo nafasi
 
kuna tetesi kuwa baadhi ya waliochaguliwa special diploma udom kuchaguliwa kidato cha tano coz zipo baadhi ya shule zinahitaji wanafunzi wa sayansi na hesabu
 
Back
Top Bottom