Searching a School for my Children | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Searching a School for my Children

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Modereta, Aug 29, 2008.

 1. Modereta

  Modereta Senior Member

  #1
  Aug 29, 2008
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  i have school going children, i am trying to find a school with a system that creates a " balanced human being" where children through this school shall become "interllectually creative and responsible citizen. This will enable
  them to enter into the society not as passive spectators but as conscious sensitive citizen, ready to tackle the challenges of our times by taking an active part in the transformation of our world. May be i am too ambitious or unrealistic
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mod,
  Inategemea wako shule gani. Kama ni kwenye msingi na O-Level basi wapeleke shule za kawaidia tu. Nafikiri hizi huwa zinasaidia watoto wawe WATANZANIA kweli kwa kuijua reality ya maisha yetu. Labda kama watoto hao ni watoto wa MAFISADI basi unasema kuwa all in all wataenda kwa wenzao USA, Canada, UK nk. Wakirudi kutoka huko, watafungua makampuni yao au kuwa maboss wa makampuni ya baba zao na wataishi maisha tofauti kabisa na Watanzania wengine.
  Mtoto kuwa na akili sana inategemea vitu vingi. Anaweza kuwa wa kwanza miaka yote na akifika chuo kikuu anakuwa amechoka kama RONADINHO na hapo anakuwa Kibonde. Ndiyo maana utaona kijana katokea Secondary za vichochoroni na akifika UDSM anaanza kuamka na kuwa UNTOUCHABLE. Watu wanasema kuwa watu wengine akili zao zinaamka wakiwa wakubwa. Ila ukweli utabaki palepale kuwa MSINGI mbaya wa elimu utaharibu JENGO zima la elimu la kijana. Hivyo, ni vema KU-BALANCE katika uchaguzi. Nilishasikia sijui wapi shule moja watoto walipata A za Kiingereza na masomo mengine wakafeli saaana. Nafikiri kama uwezo upo, waende shule nzuri na si NZURI SANA. Na jinsi wanavyopanda basi waanze kupatiwa shule nzuri zaidi. Si vibaya kama shule hiyo kidogo fimbo zinatembezwa mara MADHAMBI ya kijana yanapozidi kuongezeka yaani anapigwa YELLOW CARD. Ila hii inategemea MUONO wa MZAZI.
   
 3. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Fanya yafuatayo:
  1.Fika ofisi ya Kata au manispaa,kwa kawaida wanadisplay matokeo ya mitihani ya shule zote zilizosajiliwa kwenye kata husika au wilaya/manispaa.
  Waandikishe kwenye zile zilizoongoza.
  2.Kama unauwezo ifikapo level ya sekondari,then peleka seminari kwa o-level tu.
  3.Akifanikiwa kufika form 4 maana yake ni kuwa uwezekano wa kufaulu kwenda form 6 ni mkubwa,since amesoma seminari.
  4.Then mwache aendelee sekondari ya serikali asibaki seminari.Hii itasaidia kwenye maombi ya mkopo wa elimu ya juu kwani mikopo inapotolewa wanaangalia historia ya shule alizosoma mwombaji.Kama alisoma shule za kulipia, it implies kuwa mzazi/mlezi anauwezo hence mkopo unakuwa mgumu kupatikana.
  5.Mwisho ndugu yangu,shule za kawaida ni nzuri at least NI WAKWELIi.Mwanao akirudi nyumbani na sifuri lake ,wanamwongezea na masikio.Akirudi na 70% or 90% basi ni 70% or 90% za KWELI KWELI,NADHANI UNANIELEWA.
  Seminari ni nzuri kwa malezi ya kiimani na vilevile wanaenda kwa WASTANI ,upo below huendi form 2 kama upo from 1.
  Kwa level ya msingi kusoma ndani ya kata,kunasaidia kupambana na shida wanazopata watoto wetu za usafiri.
   
Loading...