Scotland: 'No vote' haina maana 'No change'


Kwani wewe ndugu yangu unaichukuliaje Zanzibar Kama Zanzibar?

Zanzibar kuwa na watu 1.2 na udogo wa eneo lake sio sababu ya kuipotezea hadhi Zanzibar hadhi yake! Kama unaipima nchi kwa idadi ya watu wake, mapana na marefu yake basi kwanini hamkuungana na Sudani, Kongo Kinshasa au naijeria!!??

Hebu msikilize baba wa taifa lako kuhusu Zanzibar halafu uje na hii post yako.


Nyerere Hidden Speech:Zanzibar and Tanganyika are…: http://youtu.be/hyO1_ro_UDg
 

Hapa umesema kinyume chake! Kiuhalisia wanawake ni watanganyika maana ndio minyang'au "nimemnukuu odinga" inayoshindwa kuhoji kwa nini raslimali zote walizonazo hazina tija na wao? Na bado yamelala fofofo huku wazungu na viongozi wachache wakizifaidi vibaya mno.

Nenda kwa wazanzibar ukaangalie raslimali zao walizonazo kwa sasa za karafuu, utalii na mwani jee haziwafaidishi!!!??

Pamoja na hizi raslimali chache lakini huwezi kumkuta mzanzibari anaishi kwenye uchafu wa nyumba ambazo juu na kuta zake ni udongo a.k.a TEMBEEEEEEEEEEEE
 
Kama tungekuwa tunaongozwa na kufanya maamuzi kwa uzalendo,tungekuwa tumepiga hatua.
Naamini 100% kuwa haya uliyosema mleta mada yanajulikana tena sana na baadhi ya wafanya maamuzi.
Huu mkwamo na mchepuko sio kwa kuwa watu hajui wafanye nini ila ni kwa sababu hawataki kufanya wanachopaswa kufanya kwa makusudi kabisa.
Kama mtu mwenye hadhi ya professor wa sheria anasema uzalendo ni utii kwa serikali iliyoko madarakani bila kujali inavyofanya kazi,utasema prof.hajui maana ya uzalendo?
Tanzania tunamhitaji mtu wa aina ya Cameroon,mtu mkweli na muwazi kwa ajili ya kesho bora.Vinginevyo,if not we,our descendants will suffer the cost of transformation.
 

Kiongozi nilidhani Lengo lakuitaka znz huru nikujitegemea kumbe Mnadhani wenzenu watanganyika wanafaidi kwa kutembeza mabakuli huko Ughaibuni,,,,,,Nakuhusu kuipata znz huru tatizo ni Unafki wa watawala wenu mkikaa kwenye Gumzo mnapeana Moyo kuipata znz huru mkienda dodoma kimyaa Kwajinsi Tanganyika inavyowapendelea mngekuwa na Viongoz badala ya wasaka Tonge zamani mgeshaipata znz yenu Nacc huku baada yakuona huyu KUPE CCM anawafanya waTanganyika mandondocha tumeamua kwa dhati kabisa kuipata Tanganyika yetu pamoja na Mitutu ya Bunduki wanayotutisha nayo Tunachojua niwatu wachache sn wakikaribia Kifo wanakuwa kimya lkn wengi lazima walete Fujo kwahiyo tumeshajua tatizo letu ni ccm tunamtoa Mapema iwezakanavyo ili Tanganyika yetu ije,,,!!
 

Kiongozi nilidhani Lengo lakuitaka znz huru nikujitegemea kumbe Mnadhani wenzenu watanganyika wanafaidi kwa kutembeza mabakuli huko Ughaibuni,,,,,,Nakuhusu kuipata znz huru tatizo ni Unafki wa watawala wenu mkikaa kwenye Gumzo mnapeana Moyo kuipata znz huru mkienda dodoma kimyaa Kwajinsi Tanganyika inavyowapendelea mngekuwa na Viongoz badala ya wasaka Tonge zamani mgeshaipata znz yenu Nacc huku baada yakuona huyu KUPE CCM anawafanya waTanganyika mandondocha tumeamua kwa dhati kabisa kuipata Tanganyika yetu pamoja na Mitutu ya Bunduki wanayotutisha nayo Tunachojua niwatu wachache sn wakikaribia Kifo wanakuwa kimya lkn wengi lazima walete Fujo kwahiyo tumeshajua tatizo letu ni ccm tunamtoa Mapema iwezakanavyo ili Tanganyika yetu ije,,,!!
 

Mbona tayari wazanzibar tayari wana Zanzibar yao? Tatizo kwa bara ni mzigo wa ukupe. Yaani raslimali za bara kunufaisha wengine.
 
Mbona tayari wazanzibar tayari wana Zanzibar yao? Tatizo kwa bara ni mzigo wa ukupe. Yaani raslimali za bara kunufaisha wengine.

Ikiwa raslimali za bara haziwanufaishi wabara wenyewe jee zitawanufaisha wazanzibar kweli!!???

Labda raslimali zenu zinawanufaisha wazungu na viongozi wenu wachache kupitia 10%
 
 


Hata Tanganyika inategemea bakuli la wahisani kufanikisha bajeti yake.

Lukuki ya raslimali mlizonazo hazina msaada wowote kwa mtanganyika.

Zaidi tutakapopata mamlaka kamili tunampango Wa kuzigeuza bandari za Zanzibar kuwa free port, na hili watawala Tanganyika wanaliogopa maana hakuna meli ya mizigo itakayofika bandarini Dad es salaam vyenginevyo zitatulipa kwa kutumia bahari ya Zanzibar.
 
Tetty naungana na wewe sema pia kwa uwezo hawa jamaa walionao siku wakijiexpose bado maisha yao yatakuwa hatarini..

Tusisahau sisi hatuna viongozi ila tuna watawala.
Mtawala anaua na kuharibu yoyote asiyefuata matakwa yake! poor Tanzania.

Ni kweli,bado wenzetu wapo mbali kusaka pesa na kuua Taifa.
 
Mkuu mimi sipo hapa kuzungumzia maisha ya Mtanganyika na Mzanzibar sisi wote maskini kwa lugha ya kihuni naweza sema minyani tu, hata ukivikwa suti na kuwekwa zoo, nyani nyani tu kwa hiyo huna nafuu yoyote. Mtanisamehe waungwana kwa lugha hiyo maana kama lugha za kihuni sio kwamba hatuziwezi..

Anyway tuyaache hayo, hata kama Tanganyika ndiye mwanamke muhimu uelewe kwamba mwenye sheria mama ni huyu mwanamke na lazima wewe bwana uzifuate kwanza, na ndio mgogoro mkubwa wa madai ya mamlaka zaidi yanapokuja toka kwenu mabwana. Hivyo muhimu weka akili zako sawa kujua kwa nini serikali yako inataka mamlaka zaidi juu ya mambo ambayo inaweza kuwapelekea wananchi wake huduma na maendeleo. Kinachozungumzwa hapa ni decentralization yaani kugawa mamlaka toka juu kwenda chini sio kugawana umaskini. Kama ungekuwa na maisha bora zaidi msingefikia kuyataka mamlaka zaidi wala kujitenga. Lini mume akamuacha mkewe wakati maisha yake ni bora zaidi? na wasemavyo wahenga kila penye mume mwenye mafanikio kuna mwanamke nyuma yake.

Na kwa bahati mbaya sana watu wengi wameutumia muungano wetu kama JUMUIYA yaani shirikisho tuloungana kwa baadhi ya mambo tu wakasahau kwamba huu ni Muungano (UNITARY) ambapo serikali kuu lazima iwe na mamlaka juu ya serikali ndogo na kuacha mamlaka madogo chini yao kuyasimamia ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli za serikali. Sasa yaonyesha kwamba imejengwa imani kwamba yale mambo ya Muungano ndiyo pekee yalotuunganisha laa sivyo kila mtu ana chake, mfumo huu sii wa kimuungano bali ni wa Kijumuiya kama ilivyo EAC (a trade union) na yaonyesha kuna watu kwa makusudi kabisa wanataka wananchi waamini hivyo. Mtazamo huu ndio ulowapotosha wengi na kama viongozi wetu wa leo wanafikiria hivyo basi hii nchi imefikia mahala pabaya sana kutokana na hulka ya Kimaskini kuupoteza UTU wake, akiona chakula mezani hufikiria tumbo lake kwanza.
 
Hakuna tatizo lolote kuirudisha Tanganyika.
Na hakuna tatizo lolote tukiamua kujiita Tanganyika badala ya Tanzania bara, haya ni majina ambayo hayakutoka kwa wananchi wa "Tanganyika". yametoka kwa wakoloni, kwa hiyo sioni mantiki ya kushabikia sana.
Is Tanganyika a "Nation"? So why do you wanna kill somebody just because huitwi mtanganyika? Is that necessary.

England ipo kama jina lakini hakuna kitu kinaitwa "Government of England".

Na wala nisingependa tujifananishe nao kwa sababu sisi tuna malengo yetu tofauti nao kimaisha.
All I'm saying is, this Tanganyika thing is too overrated, it's just politics ... it's actually weird/kinda stupid if you ask me.
 
Mkuu nashindwa kabisa kuelewa hawa watu wanataka nini. Mimi nimewashauri hivi. Toka leo wajiite Watanganyika kila wanapokwenda, waanzishe timu za Tanganyika ktk michezo, mbona zamani wakati wa Nyerere hadi 1984 ilikuwepo timu ya Tanzania bara na ya Zanzibar kama hawalitaki jina hilo wajiite Tanganyika uwe ndio mwanzo mpya.

Tukienda Olimpiki au michezo ya Commonwealth tuwe na timu zetu tofauti na Zanzibar na hata World cup tuombe nafasi hizi zitenganishwe. haitachukua Muda Tanganyika itajulikana japo mimi kama wewe sii mshabiki wa jina la Tanganyika hata kidogo. Hili Jina la wakoloni sijui Mjarumani ambaye hadi leo amekataa kuwalipa wazee wetu fidia baada ya kupigana vita wakapoteza maisha yao kwa ajili yao. Yaani hata sielewi kuwepo kwa Tanganyika kutaleta Uzalendo gani zaidi ya Tanzania.
 
Mkuu, umenikuna hapo kwa makamu. Ni hawa hawa wanaosema S3 ni gharama, leo wanakauwa na utitiri wa makamu. Ukiweka na wale wa znz tunaishia kuwa na viongozi wa kitaifa 5 katika ngazi ya Urais na Umakamu.
Halafu wanasema S3 ni mzigo.

Kuna mwenzetu kasema rasimu ya Warioba ilikuwa kukusanya maoni tu. Nadhani ndicho Warioba alichokifanya.
Amekusanya maoni kisayansi, sasa sijui bunge la katiba la Sitta lilipata wapi ridhaa ya kukusanya maoni;
1. Kuunda tume ya Sitta na Shibuda kwa njia ya kujiteua
2. Kukusanya maoni ya wafugaji 17 na wakulima 23

Hao hao wanaosema tume ya warioba imekusanya takwimu za watu wachache katika maelefu leo wamekaa kimya wakitetea takwimu za Sitta za watu 40.

Hili la katiba ya Sitta ni hatari na naogopa kama taifa sijui tunaelekea wapi.
 
Mwaka 1965 Mwalimu alipiga marufuku vyama vingi. Mwaka 1995 Mwalimu alikuwepo Jangwani katika mfumo wa vyama vingi.
Mwalimu alikuwa 'progressive'' na kwamba, wakati aliweza kuusoma vizuri sana.

Uingereza imekuwa chini ya Monarchy kwa miaka 300.
Mfumo wao ulikuwa Unitary. Ni mfumo uliokuwa na nguvu sana kwasababu ya Monarchy ambayo ni final say kwa mambo mengi tu.
Mabadiliko ya dunia yameupitisha mfumo huo katika hatua mbali mbali kama tulivyoeleza, na bado inaendelea

Mfumo wa Uingereza ndio umeigwa na makoloni na mataifa mengi duniani.

Leo waziri mkuu Cameron anasimama na kueleza jinsi Unitary system inavyobadilika kukidhi haja ya mazingira mapya duniani.
Kasema, Scotland wamesikilizwa, sasa ni wakati wa washirika kusikilizwa sambamba na Sotland

Tena kasisitiza England ambayo mfumo wake haupo (kwa maana haina fiscal autonomy) katika mambo mengi ukilinagnisha na washirika sasa isikilizwe. Kasisitiza sauti za mamilioni ya England zisikilizwe kama tunavyosisitiza sauti za Watanganyika zisikilizwe

Mfumo wetu ambao Nyerere aliwahi kukiri tumeuchukua kutoka Uingereza kwa sehemu kubwa, umekuwa na malalamiko hasa kwa wazanzibar. Kila mara wamesikilizwa na sasa wamegeuza muungano kama mradi.

Mfano, mwaka huu wamezawadiwa nafasi asilimi 21 za ajira za muungano.

Ni hao hao wanaosema kwanini wafanyakazi wa halmashauri wawe wa muungano, lakini sasa hivi wanamegewa pande kutoka katika 'nyama' ile ile wanayosema ni haramu.

Wamedai PAYE, wamepewa ingawa mapato ya PAYE ni ya wafanyakazi wa Tanganyika.

Hivi Karibuni wamezusha madai, wanataka bidhaa ziingie znz halafu zije bara bure.

Maana yake ni kuwa ule utamaduni wa kutoa misamaha wanauendeleza hata kama ni maumivu kwa Mtanganyika.

Yaani, bidahaa ziingie znz, wachukue kodi kama wanataka au watoe misamaha halafu Tanganyika ikose mapato.

Wakati wakitenda hayo, ni Tanganyika hiyo hiyo inayolipia gharama za bajeti na Serikali yao.

Kwa kutokuwa na uchungu kama ule wa kutoa misamaha ya kodi, sasa wameamua kuweka lundo la viongozi.

Ka nchi kadogo na fakiri kama znz hakawezi kuwa na Rais, Makamu wawili! wote hao ni wa nini?

Fikiria kuwa mbunge wa Ilala au mkuu wa Wilaya ya Ilala hana makamu, vipi znz wamudu utitiri wa viongozi?

Jibu ni rahisi, gharama za kuhudumia hao viongozi zinatoka hazina Dar kwa jina la muungano Tanzania.

Tanzania inayosemwa ni kodi za Mtanganyika. Hivyo zigo la makamu wa rais znz analibeba mkulima wa Malinyi, Kidogobasi na Mtimbira. Kwanini?

Hapa hatuna maana wasiwe na viongozi wanotaka, tunachotaka ni wao wawajibike si kwa mambo yao tu hata katika muungano.

Katika muungano watakapoacha kudai na kuja kuomba hilo ni msaada kwetu.

Watakapopunguza utitiri wa viongozi kama wale watalii 84 wanaokuja Dodoma kwa gharama zetu, watakuwa wametusaidia.

Azma ya kuwa na Tanganyika ni kutoa fursa kwa Tanganyika kuhudumia watu wake bila kufungwa mikono na jina la Tanzania ambalo limeigeuza Tanganyika shamba la bibi.

Huwezi kuwa na mznz Mtanzania wakati anakuja Hazina na TRA Dar, halafu mtu huyo akawa na kitambulisho cha uzanzibar ukaazi akishachukua fungu Dar na kupanda meli.

Hivyo hoja ya kutoa mamlaka kwa washirika ambao ni znz na Tanganyika haina maana kuua muungano.

Ina maana kuimarisha kwa maridhiano, vinginevyo Tanganyika itaamua asubuhi moja kuzinduka na ndicho kifo cha muungano.

Swali linabaki, katika hali hiyo nani atakuwa kwenye hasara?
 
Kwanza niseme afadhali umeliona hilo la kufananisha mazingira yetu na Uingereza.
Hoja hiyo ndiyo imetumika katika kupotosha kuwa Scotland wamekataa kundoka katika muungano wa Uingereza na hivyo Tanzania ijifunze kwa wenzetu.

Sisi tunasema huo ni upotoshaji. Na ndio hasa tunaupiga vita hapa.
UK ina mataifa 4 yaliyoungana, na Scotland ilitaka kuwa huru.
Sisi,sehemu kubwa ya wznz wanataka muungano, kusema tuwaangalie Scotland kama mfano ndio upotoshaji tunao ukataa.
Hatuhitaji Tanganyika kuvunja muungano, bali kuimarisha kama Uingereza wanavyofanya sasa

Lakini pia usishau kuna kufanana kwa baadhi ya mambo, na hilo hatuwezi kulipuuza.
Tumeonyesha wapi tunafanana na tunaweza kujifunza nini.

Pili, umedai Taganyika ni jina la mkoloni.
Sijui ni kitu gani unachozungumzia hapa ikiwa muungano na mfumo wa tawala zetu ni wa Westminster ya Uingereza.
Kwanini hukuliona hilo kwanza.

Halafu, sheria tunazotumia leo hii nyingine ni za mkoloni, kwanini hujalizungumzia hilo.

Mfano, sheria za makazi( local) ni za mwaka 1930 n.k nab ado tunazitumia.
Sisi ni wanachama wa Commonwelath chini ya malkia, kwanini hujaona ukoloni huo.

Leo unapopata tatizo katika nchi tusiyokuwa na ubalozi, unashauriwa kwenda ubalozi wa Uingereza, na hilo lipo katika hati yako ya kusafiria. Kwanini hujaona ukoloni hapo.

Tatu, unaposema tunaweza kujiita Tanganyika, hilo halina shida.
Shida na tatizo letu ni kupewa haki ya kuamua mambo yetu kama Tanganyika bila kufungwa mikono na wazanzibar.
Mfano, wao wanasheria zao za ardhi, sisi ardhi yetu ni yao pia. Kwanini.

Tunachokitaka hapa ni fiscal autonomy ya Tanganyika, ili kuepuka ‘kuwanyonya' wznz na wao kututegemea hadi kutubebesha mizigo inayotokana na uzembe wao.

Hawawezi kutoa misamaha ya kodi halafu Mtanganyika afidie uzembewao.
Kila mmoja abeba mzigo wake.

Nne, tunataka kuwe na mshirika wa muungano ili kila mmoja apate uchungu wa muungano.

Mfano, leo kama wangekuwa wanahudumia watalii wanaokuja Dodoma kwa jina la wabunge, wasingeweza kuwa na watu 84.
Mbona BLW lina watu 50.

Hapa ni kuwa Tanganyika inabeba mzigo wa watu wanaokuja kuwakilisha nchi yao kwa jina la Tanzania. Hapana ! sasa basi

Na mwisho kama unadhani Tanganyika is overrated, kuna tatizo gani la kuzindua ili ifanye kazi? Nini mnachokwepa katika hilo?

Na hadi lini Tanganyika itabaki kuwa Tanzania ikibeba znz , Tanganyika na muungano peke yake? Lini wznz watasikia uchungu wa muungano kama hawawajibiki?
 
Hoja dhaifu sana, tunataka fiscal autonomy na sijui kama unaelewa maana ya neno hilo.
Sitafananua kwa ushahidi kuwa hukumuelewa Cameron it is unlikely unaweza kunielewa.

Cameron aliposema wanatoa mamlaka, mwenzangu ukasema amesema wanahodhi mamlaka. Hata palipokuwa na video hukuweza kumwelewa Cameron.

Kama ni suala la jina, mbona znz wanalo lao? Vipi ile katiba yao ya 2010 ni ya nini?
Wapi katiba ya Tanganyika kwa mambo ya Tanganyika?
Lini na vipi tutakuwa Tanganyika na wakati huo huo tukibeba mzigo wa znz kwa jina la Tanzania?

Ni wewe Mkandara unayesema tumeavaa koti, leo tunataka kuvua koti, hutaki.

Kwako wewe watu wanafahamu usichokitaka ni uwepo wa Tanganyika kwa ile kauli yako '' Nawasikitikia wazanzibar, watapata taabu sana'' ambayo ukitaka nukuu omba niianike hapa.

Hatuwezi kubeba mzigo wa znz bila sababu za maana.
Muungano ni lazima uwe wa kiuchumi ambao sasa ni ulinzi.

Hatuwezi kuwa na Tanzania ambayo Mtanganyika ni raia haramu na daraja la pili kule znz kuliko Mkenya, Mnigeria n.k.

Wakati wznz wanachoma moto Watanganyika, mlikuwa kimya. Leo watanganyika wanadai nchi yao halali mnatoka povu

Tunataka fiscal autonomy tu, na kama jina la wakoloni linwaudhi tutaita Azania. The bottomline lazima tuwe na uwezo wa kuamua na kupanga mipango yetu kama Tanganyika na si kubeba mzigo wa znz.

Leo kwa kutumia jina la Tanzania tunagharamia bajeti, ulinzi na usalama, mambo ya nje na sasa wameongeza utitiri wa makamu wa rais ambao hawana maana yoyote Tanganyika ingawa ndege za JMT wanatumia kubeba mikaa kutoka Pemba

Leo kuna wanafunzi 28,000(Mwigulu Nchemba) waliokosa MIKOPO. Wapo wanafunzi 1,700 kutoka znz waliopewa zawadi, siyo mikopo. Kodi za Mikopo ya wanafunzi wa Tanganyika wanalipa watanganyika.
Zawadi za wanafunzi wa znz wanalipa Watanganyika.

Huko znz wana bodi yao iliyodhamini wanafunzi 800 mwaka huu. Hakuna mwanafunzi hata mmoja kutoka Tanganyika.
Maana yake, wanatumia chao kupanga mipango yetu, wanatumia chetu kufanikisha mipango yao wakiwa nchi jirani ya znz isiyotambua Tanzania (ref katiba 2010)

Leo wanaajiri hovyo, wakijua mishahara inatoka hazina Dar.
Hawakusanyi kodi wakijua tutafidia bajeti na wanatoa misamaha wakijua kuna Watanganyika wanamenyeka kuwalipia kodi.
Huu uzembe, wizi na uvivu sasa baasi.

Tunataka Tanganyika tuwe na mamlaka ya kuamua mambo yetu

Kama haitarudi mezani, itarudi mitaani na huko ndiko mtasikia jina la Tanganyika kwa kishindo.

Mkuu Mkandara, hatuwahitaji wznz kwa lolote kwa chochote. Ni mzigo mzito wa samadi mgongoni.
 
Na sasa hivi hakuna mzanzibar anayesema tean.
Keissy kawaambia ukweli bungeni, hoja zao ni ngumi.

Hawa ni wanafiki, wanasubiri wakirudi znz wanaanza tararira.

Ni mzigo mzito sana tumebeba. Zigo hasa, maana wenzetu hoja zao ni kwa IGP na mkuu wa majeshi na mabalozi baasi.

Uchumi hawana habari, mjomba Tanganyika yupo, watakuja kuchota. Zigo zito sana mgongoni mwa Mtanganyika.

Wameondoka znz wakiwa na msimamo, wanafika Dodoma wameufyata wao ndio wenyeviti wa kamati.
Mwakani utawasikia Nyerere laanatulah, leo wapo katika mfumo ule ule wanaoulaani.

Tanganyika is the way forward.
 
Ni kweli tusiishie hapo kwenye timu za mpira na olympic, tunataka pia tuwe na bunge letu kitakalopanga mipangao ya tmu zetu, tunataka serikali yetu itakayopanga mipango ya timu zetu.

Unachokisema ni kitu kizuri sana kwamba Tanganyika iruhusiwe kuwepo kutumia jina, iwe na bunge na serikali yake , mahakama zake n.k. Hakika ndicho tunachotaka.

Tena znz walikataa ligi tumebaki ya yetu, ile ya znz mamelod wa FIFA kasema haifai hata kusema.
Leo Malindi wapi, Small simba wapi. Hivyo bana timu ya taifa ipo zanzaibr heroes n.k.

Msifiche ukweli, sisi hatutaki jina kama wendawazimu, tunataka fiscal autonomy ya Tanganyika na hapo ndipo jina linaanza.

Hilo litatokea tu kama si kwenye mfumo wa sheria, litatokea mitaani.

Tanganyika haizuliki, ninyi hamuitaki si kwasababu ya jina la kikoloni, mnachotaka ni jina Tanzania litumike ili litumiwe na wezi kupora rasilimali za Tanganyika. Hilo linafika mwisho.

Mnasema ni jina la Kikoloni, Dar es Slaam ni jina la wazawa hilo?

Mkuu Mknadara, znz ni kasehemu kasiko na manufaa kwetu hilo ukae ukijua.
Huu muungano ni wa kuwasadia si wa manufaa kwa Mtanganyika.
Wenye muungano ambao ni Tanganyika sasa wamechoka

Mtatafuta kila hila ili Tanzania ibaki ili kujenga utegemezi wa znz, kwasasa Watanganyika wameshaamka.
 

Hili blanket term wazanzibar ni misleading. Tatizo siyo wazanzibar tatizo ccm zanzibar. Wanzanzibari wanawaunga mkono in your struggle to be free.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…