Scotland: 'No vote' haina maana 'No change'

Rasimu ya Warioba imetupwa. Iliyopo ni ya CCM na Samwel Sitta.

Wakati bunge linaanza Sitta alisema kuna mambo mengi mazuri ya kushughulikia kama kuwapa wazanzibar nafasi zaidi katika muungano, kuwapa wafugaji na wakulima fursa zaidi ndani ya katiba.

Ukisoma rasimu ya Chenge, kila jambo alilosema Sitta ndilo limefanyika. Kuwapa wazanzibar pipi na peremende.
Wakati huo huo kuhakikisha Tanganyika inafutika.

Njia ya kuhalalisha katiba ya CCM ya mafichoni ni Sitta kukusanya maoni kwa wakulima 17 na wafugaji 23 halafu kutengeneza katiba waliyosoma jana.

Hawa watu wanatufanya majuha kama ulivyosema. Hata hivyo huu ndio mwanzo wa mwisho.

D.Cameron kasema anashughulikia matatizo ya Wales, northern Irelanda.
Cameron akasema, England imeachwa katika mjadala wa kitaifa na ni wakati nao wasipuuzwe kama wanavyopuuzwa Watanganyika.

Kwa kadri CCM inavyowafanya wananchi majuha, muungano unakaribia sana kuvunjika.
Kwasasa hoja si Zanzibar, ni kurejea kwa Tanganyika katika hadhi yenye mamlaka, utamaduni na value zake kama ambavyo Cameron ameonyesha njia kwa Wales, England na N.Ireland.

Kinyume cha uwepo wa Tanganyika ni kuvunjika muungano.Hilo si mjadala tena ni suala la wakati.
 
Mkuu wangu hiyo rasimu ya warioba haikuwapa Zanzibar mamlaka zaidi? kilichotofauti na Sitta niu kuwepo tu kwa Tanganyika lakini hadi leo hii tanganyika ina mamlaka yote yalokuwa ya Muungano na yasokuwa ya Muungano. hakuna swala lolote lilotakiwa na wananchi wa tanganyika lilizimwa kwa sababu ya kutokuwepo Tanganyika - HAKUNA. KIla kinachopita kwa serikali kuu ni cha tanganyika ina maana hata hao wabunge wa Zanzibar wanapelekeshwa tu pale Bungeni maaa nguvu kubwa bado ipo ktk serikali kuu.

Maneo ya Cameron juu ya England ni kuonyesha watu jinsi gani serikali yake inavyotaka kuweka usawa lakini anajua nguvu yote wanayo Westminster na hivyo kuyaondfdoa mamlaka hayo hapo inabidi England nayo kama nchi iyadai unajua kwa sababu gani?.

Scotland watakapo kuwa na mamlaka juu ya kodi na kuchangia mfuko wa Ufalme ina maana Scotland inakuwa na mamlaka juu ya mapato yao wakati England na nchi nyingine zinakuwa bado hazina mamlaka hayo hivyo kuna umuhimuu wa kila nchi iwe na mamlaka hayo. Ni hoja inayokubalika kuisikiliza na pengine watafikia maridhiano. Sisi kwetu Zanzibar tayari wanayo mamlaka hayo na huku Bara (England yetu) TRA wanayo mamlaka sasa unachotaka kusema wewe Tanganyika idai nini zaidi ya hapo? devolution on social welfare sisi bara tuna TAMISEMI (chini ya CCM) japo haifanyi kazi inavyotakiwa lakini tunacho chombo hicho kabla ya hao England, Unachofananisha ni kipi? Je kwa kufanya hivyo tumeongeza ufanisi wa huduma za serikali kwa wananchi ama kuongeza pato la nchi - sidhani..

Mkuu wangu rasimu ya Warioba haina tofauti kabisa na maamuzi ya kina Sitta (sii ya wananchi) isipokuwa katika mambo mengineyo labda na hilo swala lenu kubwa la kuifufua Tanganyika ambayo ni jina tu limekosekana lakini mamlaka yote yapo chini ya Tanganyika. Bunge la Dodoma halina tofauti na Westminster.
 
Mkuu hujajibu hoja za Cameron kuhusu aliyosema. Hapa unajaribu kubadilisha mjadala.
Halafu unadai tunapotosha, wakati tumetumia hoja za Cameron na yaliyotokea.

Tunataka devolution yenye kutoa haki na usawa kwa Tanganyika kama ambavyo Wales, England na Ireland zinavyokwenda kupewa haki sawa na Scotland.

Usichokijua kutoka Scotland ni sawa na kinachotokea Zanzibar. Kwamba, mafuta yamewatia kiwewe.
Hata hivyo, bado wanahitaji ulinzi wa kiuchumi na usalama na hilo ndilo limepelekea wengi kuogopa kujitoa.
Na znz ni hivyo hivyo, kwamba wanahitaji kubaki na jina la Tanzania ili wapate ulinzi wa kiuchumi na Uslama.

Tatizo ni kuwa znz wanadai hayo kwa gharama za Mtanganyika.
Ni upuuzi wa hali ya juu sana kudai devolution za mikoa wakati kuna wznz 84 wanaochukua rasilimali zaidi ya mikoa 10 hadi 20 ya Tanganyika.

Ni upuuzi kudai devolution wakati znz yenye watu 1.2 inachukua kiasi cha takribani bilioni 500 kutoka Tanganyika kwa jina la Tanzania. Wewe unaficha unyonyaji unaofanywa kwa jina la Tanzania na ili kufikia lengo hilo hutaki kusikia Tanganyika.
Tanganyika inahitajika kwa utambulisho na fiscal autonomy yake na si vinginevyo

Mkandara, hatuwezi kuishi na Tanzania ambayo ni mzigo mkubwa sana kwa Watanganyika.
Tunataka fiscal autonomy kama wznz ili kuondoa kama si kukomesha upuuzi wa kupora kwa kutumia jina la Tanzania.

Leo tumeshaeleza mchango zero wa znz, na muungano kubebwa na Tanganyika kwa jina la Tanzania.
Hiyo TRA ya Tanganyika inakusanya kodi na kuzipeleka znz, wakati huko znz ZRB haina mchango kwa Mtanganyika.
Huwezi kuzuia hilo kwasababu jina la Tanzania linawahusu wznz, la waznz ni lao. Huu upuuzi tunaukomesha sasa.

Devolution lazima ianze na nchi na hapa uwepo wa Tanganyika. Halafu tutaangalia maeneo ya kusaidia wazanzibar
Nasisitiza kuwasaidia wznz kwasababu sisi hatuwahitaji.

Unachopigania wewe kama ulivyowahi kusema huko nyuma ni kutorudi kwa Tanganyika.

Ulisema Tanganyika ikirudi Wazanzibar watapata taabu sana(nukuu ipo kama unaitaka)
Hivyo usilaghai watu kwa kujifanya ni Mtanzania kuliko Mtanganyika. As long as znz ipo, Tanganyika inahitaji haki yake

Lazima tukubaliane kuwa znz ni mzigo na tatizo kubwa, na kwamba wao ndio wanapaswa kuji-adjust kuishi na sisi kwasababu wanatuhitaji kuliko tunavyowwahitaji.
Ndivyo Scotland ilivyoamua, kwamba itabaki katika muungano lakini washirika wengine wapewe haki kama wao.

Niseme kuwa hujaweza kujibu au kufafanua hoja za Cameron kama nilivyokuuliza.
Hiyo maana yake ni kukubaliana na aliyosema. hatuoni kwanini unaendelea kubabaisha watu.

Jibu hoja si kutuondoa katika mada kwa vioja.
 
Cameron kaniuliza swali? ni hoja gani hiyo ambayo sikuijibu. Nimekuonyesha tu wazi kwamba hayo yanayodaiwa na Scotland sisi tayari tulikwisha yafanya na tumeona matokeo yake. kama ni kodi zanzibar tayari wana mamlaka hayo na Tanganyika tunayo hatuna nchi nyingine kama wales ama North Areland. kama ni social welfare tayari tumeisha peana mamlaka hayo tunayo Tamisemi tena zaidi ya happo tuna vyombo vingine vingi vya kimamlaka ya maendeleo MKUKUTA na MKUZA.

hao Wazanzibar 84 ni wabunge wa zanzibar katika bunge la Muungano hata huko Uingereza wabunge wa Scotland bado watakuwepo bunge la Westminster, kuwa na malaka juu ya uendeshaji shughuli za serikali haina maana unapoteza uwakilishi ktk bunge la taifa - hapana isipokuwa unapewa mamlaka ya kusimamia. Wee vipi mkuu wangu. Unataka Bunge la Tanganyika? well wasome waingereza wenyewe wanasema nini kuhusu hilo wazo..England

Nikikupa Mamlaka ya kuendesha kitengo cha biashara yangu ina maana huna kiti ktk kikao cha maendeleo ya kampuni. Mkuu kutoa mamlaka chini haina maana mtu anapoteza kiti hata wizara zetu zina Idara na mkuu wa idara ana mamlaka fuani alopewa juu ya uendeshaji wa idara hiyo. haina maana anapoteza kiti chake kama mtumishi wa Umma.
 
Tumemuuliza kwanini England, Wales, North Ireland bado zipo katika muungano kwa utambulisho, tamaduni na value, hana jibu.

England haijapotea na kuwa Britain, bali ipo ndani ya Britain. Vipi Tanganyika ifutike ndani ya Tanzania.

Tumemuuliza kwanini Camaeron ameahidi kufanyia kazi maeneo ya England na Wales, hana jibu.

Ukimuuliza Mkandara, kwanini Tanganyika isiwepo kwa utambulisho na fiscal autonomy, hana jibu.

Asichokitaka ni kuwepo kwa Tanganyika, anajua hilo litamaliza uhuni na wizi wa wazanzibar kwa kutumia jina Tanzania.

Kila wanapohitaji kupora huja kwa jina Tanzania, wakipata wao ni wznz ambao Mtanganyika ni kama Mnigeria tu hana hadhi yoyote. Well, hatuhitaji kuwa wznz tunahitaji kubaki na Utanganyika wetu.

Mkandara ni mbabaishaji kama CCM, amebadili position mara zaidi ya 50.
Huko nyuma kasema hakatai serikali 3, leo anasema hataki serikali 3.

Leo anasema kuna taifa la bara, anajitia ujuha tu akijua haujawahi kuwa na kitu kama hicho tangu dunia iumbwe

Hana hoja kwanini tusiwe Tanzania wote, kwanini iwepo znz na Tanzania na si znz na Tanganyika. Hana hoja.

Sasa hivi anabadili mjadala, tumempa vidonge vya Cameron hajaweza kuandika hata mstari mmoja, bado anataka tuendelee kuishi zama za mawe kwasababu tu anataka wznz waendelee kupora na wizi.

Leo anasema znz si tatizo, hivi kweli watu 84 wanaokuja kutoka nchi jirani ya znz kama watalii kupiga soga Dodoma wanalipwa bilioni 126 wakati tunapeleka bilioni 100 Muhimbili kwa miezi 3 halafu tuseme hawa si tatizo.

Hivi kweli, wznz wasiokusanya kodi wanapewa nusu ya bajeti kwa pesa za Mtanganyika halafu tuseme si tatizo.

Hivi wznz wanaotoa misamaha halafu wanalipia huduma za elimu na nishati kama umeme bure si tatizo kwa mlipa kodi wa Tanganyika.

Hakuna njia ya mkato lazima tufuate model ya Cameron. Yes, ya Cameron kwasababu yeye ni kiongozi sisi tuna watwala wa FFU na Polisi.

Lazima tuondoke katika ujima wa unitary system twende katika federation kwa kurudisha hadhi ya Tanganyika, kuipa mamlaka ya kumiliki, kupanga, na kuendesha uchumi, utamaduni na value zake bila kufungwa na mikono ya wznz.

Ndio maana tunasema hoja ya Scotland imepotoshwa na tupo hapa kupambana na wapotoshaji.
Ukweli wanaouona na tutaendele kutoa elimu dhidi ya ubabaishaji na upotoshaji

UK wametaka muungano, hawajakataa mabadiliko.

Mabadiliko ni haya ya kuondokana na mfumo wa Unitary na kwenda katika devolution zaidi.

Hatuwezi kuanza na devolution bila kuwa na taifa la Tanganyika. Hilo sasa ni suala la muda na halizuuiliki tena.
 
Ok, maswali yanayotokana na hoja za Cameron ambaye ni mwingereza zaidi yako wewe ni haya hapa.
Anaendelea
Fafanua alimaanisha nini na kwasababu zipi.

 
Hujauliza vizuri kwa sababu UK ina nchi NNE ktk muungano wake wakati sisi tuna nchi mbili. Unapouliza kuhusu Ireland na Wales nashindwa kukuelewa. Cameron anazungumzia nguvu watakazo pewa Scotland itaiacha England ndani ya mambo ya pamoja na Wales na Ireland wakati sisi tunapoipa nguvu Zanzibar na Tanganyika moja kwa moja inapata mamlaka hayo haina mchangiaji mwinginewe na nimekupa mifano. Kwani TRA tunachangia na nani ktk mambo ya Tanganyika? TAMISEMI ipo Rwanda au Kenya pia? Tulipofika sisi ndiko Uingereza wanafikiria kwenda sasa inakuwaje unawachukulia wao kuwa mfano badala ya wao kutusoma sisi tulo mbele yao.
 
Mchambuzi #56

Leo Warioba na Cameron wanasimama upande wa viongozi
Upande wa pili kuna CCM, JK, Sitta katika kundi la watawala.

Ahsante sana kwa bandiko lilosheheni hoja za kutitia na nzito.
Huko wababaishaji hawatagusa maana ni misumari mwanzo hadi mwisho
 
Last edited by a moderator:

ndugu yangu mbona unakuwa kama unasahau?/
ivi unajua tulishafanywa kama midoli kwamba tunahadaika ata kwa sahani ya pilau na maji ya baresa??

ivi unajua leo hii serikal ikiongelea maendeleo inaongelea watu kuvaa madela na ndala za kimasai??

leo hii rais yuko kwenye climate change forum cha ajabu kabisa anaongopea hadi ulimwengu wa wenzetu kwamba tanzania tunakabiliana na changa moto hii af akasahau kwamba ndo nchi inayoongoza kwa kuwa na magari chakavu tena yasiyo na smog check?
akasahau kwamba tanzania ndo nchim pekee ambayo hadi leo bado ina dispose taka zake kwa mtindo wa open combustion ambao unachafua hewa na maji??

af utaskia akirudi hizo mbwe mbwe zake, nenda mwenyewe kajionee ofc inayohusika na utupaji taka pale katibu na kamata ofc ni uchafu kuliuko uchafu wenyewe af mtu anavaa tai mbele za watu anasema??

kwaheri nitarudi baada ya saa 2 usiku
 
Kwa tafsiri isiyo rasmi '' kwahiyo, kama ilivyo kwa Scotland kupiga kura katika bunge la Scotland kwa masuala ya kodi, matumizi na huduma za jamii. vivyo hivyo England, pamoja na Wales na Ireland kaskazini, zinapaswa kupiga kura kweny masuala yao''
"And I want Wales to be at the heart of thedebate on how to make our United Kingdom work for all our nations.
Ningependa Wales iwe kitovu katika mjadala wa namna tunavyoweza kuifanya muungano wa falme zetu(United Kingdom) zifanya kazi kwa mayaifa yetu

Ireland kaskazini ni lazima tuhakikishe mamlaka zinafanya kazi kwa ufanisi

Nina amini kuwa sehemu muhimu inayoachwa katika mjadala wa kitaifa ni England

Tumesikia kauli za Waskoti na sasa mamilioni ya sauti za England hazipaswi kupuuzwa''

My take
Unamwekea Cameron maneno yako. Hakuna mahali aliposema nguvu za England zitaachwa ndani ya mambo ya pamoja ya Wales na Ireland.

Hakuna mahali Cameron kasema hayo, kinyume chake nimekuonyesha amesema wazi kuhusu kutoa mamlaka kwa Wales, kuhakikisha mamlaka zinafanya kazi kama inavyopaswa Ireland, na England ambayo imeachwa katika mjadla wa kitaifa lazima sauti za mamilioni ya watu wake zisipuuzwe.

Mkandara, video ipo, tumeweka mameno ya Cameron kwa kiingereza, na sasa tafsiri.
Sielewi nini tatizo lako, kutoelewa mada, maana au ni tafsiri. Sielewi. Kuna nyakati unajitoa ufahamu bila sababu.

Kuhusu TRA, tumekueleza kuwa ile unayosema ni ya Tanganyika kwa jina la Tanzania inatumika vibaya. Endapo unaamini TRA ni ya Tanganyika, iweje Zanzibar waje kuchota mishahara ya SMZ kwa jina la Tanzania na si kuomba msaada kutoka Tanganyika?

Iweje znz ipate 4.5% ya pato linalokusanywa na TRA ya Tanganyika kama haki yao na si msaada kwavile ni ya Tanganyika?

Iweje znz ihukue pesa za kufidia bajeti yake kutoka hazina ya Tanganyika

Iweje TRA unayosema ni ya Tanganyika itoe bilioni 11 kwa umeme wa kwenda Pemba kama haki na wala si msaada?

Inakuwaje wanafunzi wa znz waje kusoma bure kwa pesa za TRA Tanganyika kwa kutumia jina la Tanzania na si kuomba Tanganyika. Tena wazazi wa wanafunzi wa Tanganyika wanalipa kodi huku watoto wao wakupewa mikopo na si zawadi. Nani alipaswa kupewa bure, Mtanganyika au hawa madowezi kutoka nchi ya Zanzibar

Iweje wale watalii 84 wachote bilioni 126 kutoka hazina inayopata mapato ya TRA ambaypo unakiri ni ya Tanganyika? Wana haki gani na kwanini wasihudumiwe na ZRB

The main point ni kuwa jina Tanzania linahalalisha na kuwapa haki Wazanzibar kuiba, na kupora kutoka Tanganyika kwavile tu nao ni sehemu ya Tanzania.

Hicho ndicho Cameron amesema kinapaswa kijadiliwe kwasababu England itaumia kwa kuendelea kubeba muungano huku washirika wakiwa na fiscal autonomy

Jaji Warioba na tume yake waliliona hilo kabla ya Cameron. Wakasema ili kupunguza mvutano lazima kila mshirika awe na fiscal autonomy ya kuamua masuala yake.

Wewe unakubaliana na Waeioba na Cameron kwa kuiita Tanganyika kama nchi ya bara.
Katika ubabaishaji tumekuuliza kama Tanganyika ipo na ndio yenye mambo yote, haki ya wazanzibar kuja kudai kama ni chao wanaipata wapi? Hapa ndipo unatakiwa ueleze, uhalali wa ZNZ kuja kudai na si kuomba wanaupata kwa kutumia haki ipi ikiwe mwenyewe umekiri kuwa rasilimaliza za muungano ni za Tanganyika.


Na mwisho, lazima utambue kuwa hatuna sababu za kuwashikilia wazanzibar.
Hatuwahitaji, na hivyo kudhani wao ni sehemu muhimu ya kutuzuia kuizundua Tanganyika ni kujidanganya mwenyewe.

In short, znz ni irrelevant kwetu na wala usiilinganishe na Scotland, Wales au England.

 
Nguruvi3,
Wewe una wabunge zaidi ya 300 ktk bunge la Muungano dhidi ya 83 kuna jambo gani ambalo halijawahi kupitishwa na bunge hilo kwa manufaa ya Tanganyika?. Kuna muswada gani ulotolewa kwa matumizi ya mambo yasokuwa ya Muungano kwa Tanganyika yalokwamishwa kuwepo wabunge wa Zanzibar?
Nitajie moja tu ambalo tanganyika haina mamlaka nayo iwe bungeni ama serikalini. Taja jambo moja Pleeease..
Ukisha kuwa wewe ndiye mwenye sheria mama unataka nini zaidi kama sii kujitafuna? Tanganyika ndiyo yenye sheria mama, Tanganyika ndiyo Westminster kwenye mabwanyenye na haina mshirika zaidi ya Zanzibar tunaowagawia tunachotaka. Bado huoni tofauti iliyopo?
- Kifupi kwa kumalizia England ina wake watatu, sisi tuna mke mmoja unafikiri mpango wa maisha yetu utakuwa sawa!
 
Kutoka Duru za Siasa: Kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

March 21 2014
 
Katika bunge la JMT lenye hao 300 unaosema, wapo watalii 84 ambao nguvu yao ni sawa na wa Tanganyika. Wao wana 2/3 kumbuka, hivyo wanajadili katika uzani sawa.

2. Katika kupitisha au kuamua mambo ya Tanganyika, hao Watalii 84 wanapiga kura kwa mambo yasiyowahusu na hivyo kubadilisha kabisa uamuzi. Leo wabunge 150 wakikataa jambo, na 150 wakikubali wale watalii 84 ndio watakaoamua nini kifanyike, wana nguvu ya kura kama mbunge wa Tanganyika.

Mfano, katika wabunge 300, miongoni mwao, 125 wakagoma zisijengwe maternity waodi na 175 zijengwe, wale watalii 84 wakipiga kura kusema zisijengwe jambo hilo halipiti.

Swali, wazanzibar wanakuja kujadili mambo ya Tanganyika yanawahusu nini.
Ni kutokana na kutokuwa na umuhimu wala thamani kila siku hudai vyeo na znz ni nchi au si nchi.
Fikiria mbunge wa znz anataka kuwe na IGP mzanzibar, na tunamlipia gharama! real

3. Wabunge wa znz wanaowakilisha watu 2,500 kwa ajili ya znz na si Tanzania.
Kumbuka mbunge wa Kigoma yupo pale kwa ajili ya Tanzania, hawa wapo kwa ajili ya znz.
Wanapaswa kuhudumiwa na SMZ na si kodi za Watanganyika.

4. Mbunge wa znz anazungumzia maendeleo au matatizo ya Muheza kwa lipi na yanamhusu vipi.
Yeye ana BLW huku bara anakuja kujadili nini, na kwanini sisi tusiwe ndani ya BLW ambayo ni sehemu ya Tanzania.

5. Gharama zimetushinda, bilioni 126 kwa ajili ya watu 84 wanaowakilishi kata ni hasara kubwa.

Japo basi wangekuja na substance, no! hoja zao ni kutaka vyeo tu hakuna hoja ya uchumi wala nini.
Wakimaliza hapo usingizi.Hatuwezi kubeba gharama za wawakilishi wa kata kwa jina la Tanzania.

6. Hawa watalii wanapewa mamilioni ya mfuko wa jimbo.
Leo umesema TRA ni ya Tanganyika, sasa hizo milioni 30 kwa watu 84 kwenda kuhudumia znz zina uhalali gani?
Lini ZRB imechangia katika Tanganyika.

Gavana kathibitisha znz haina lolote wala chochote, sisi tunabeba mzigo wa kuhudumia watu 84 na wake zao wakienda kuondoa chunusi India na London.

Hatuwezi kuwawajibisha kwasababu wamekuja kwa Uzanzibar ndani ya Tanzania.

No way, huu wizi na uporoaji, udowezi na uvivu lazima ukomeshwe.

Tanganyika inataka fiscal autonomy, hatuhitaji kunyonya znz wala hatuwahitaji kwa maendeleo yetu

Nadhani umeelewa nilipoatafsiri hoja za Cameron, usimwekee maneno mdomoni kuhalalisha hoja zako potofu na dhaifu
 

Tatizo lipo wapi Zanzibar kudai chake, hata kama mafuta hayadhibitika kuwepo?
Uzembe wa Watanganyika kudai haki zao isiwe sababu ya kusema legitimate demands za Wanzibari ni za kitoto When UN comes knocking to map out the maritime boundaries of Tanganyika and Zanzibar will no longer be in doubt then who has the last laugh.
 
Mkuu kama hujui how the system works uliza. hao wabunge 83 wanapiga kura 2/3 kwa mambo ya 22 ya Muungano hawaingilii mambo ya Tanganyika isipokuwa penye sheria mama, na ndio maana wakati mwingine unaliona Bunge tupu halina watu. Inapofika kujadili bajeti ya Tanzania wabunge wanaelewa msimamo wa kila jambo hilo jifunze kabla hujaenda Bungeni.

Ila inapofikia maswal ya Zanzibar kudai mamlaka zaidi ndipo wabunge wote hujadili kwa sababu ni swala linalomhusu kila mtu. Kazi ya bunge ni kupitisha muswada tu hakuna muswada wa Tanganyika ulowahi kutopitishwa kwa sababu ya Zanzibar ila ipo miswada ya Zanzibar ktk muungano ilokataliwa. Sasa wewe ulitaka hata sheria mama inapofanyiwa marekebisho wasizungumzie ama kupiga kura?

Nimekuomba nitajie muswada, sheria ama kuisimamia serikali ya tanganyika ambako Zanzibar imekuwa mwiba kwa hao wajumbe wake kuingilia mambo ya Tanganyika kama sio kutushtua sisi zaidi. Zanzibar hawahitaji kuwa sawa na sisi wao wako Mil 1.3 nasi mil. 45 wanaingia mara ngapi? Tukiwa na Tsh Trillioni 45 wao na Trillioni 1.3 tuko sawa tu usitazame namba mkuu..

Gavana anasoma maandishi, ni takwimu alizonazo, kama Zanzibar haichangii, muulize yeye mfuko wa muungano una kiasi gani na wa Tanganyika una kiasi gani? Akiweza kujibu nitakuwa upande wako wakati wowote..
 
Nadhani hukumuelewa Bongolander
Alichosema ni kuwa wznz walichagizwa sana kujitoa katika muungano baada ya kusikia kuna mafuta.
Ndipo akatokea mtu mwenye PhD na kusema yanaonekana majini ukipita na mtumbwi.

Haya yangesemwa na mvuvi tusingejali, huyu ni mtu mwenye elimu ya juu sana na bado anaamini unaweza kuona mafuta ukipita na mtumbwi.

Pili, hatuna sababu za kuwazuia kuondoa mafuta katika mambo ya muungano.

Tusichotaka ni wao kudai gesi na pengine mafuta ya Tanganyika kama mambo ya muungano.
Huu wizi kwa kutumia jina ndio tunaupiga vita.

Tatu, znz wanaweza kuondoka tu na UN wakaja, hilo haliwezi kuzuilika.

Swali ni kuwa pale Dodoma wao ndio wenyeviti wa kamati za bunge, wanafanya nini kama boundaries zina umuhimu sana kwao? Bunge la CCM na Sitta wao ndio vinara sasa tuwaeleweje

Nne, tunataka Tanganyika kwa faida za Tanganyika. Tumegundua wznz ni wenzetu wakaielekea hazina Dar, baada ya hapo ni wznz.

Tukutane katika mambo 7 ya kuwasidia. Vinginevyo hatuna sababu za kuwazuia hata kidogo.

Na mwisho, kuhusu uzembe wa Watanganyika hilo nakubaliana nawe
 
Well done, kama ni hivyo waje siku za mambo ya muungano kwa gharama zao na si za Watanganyika
Hakuna sababu ya wao kukaa 60 na kuzungumzia mambo yasiyowahusu, ni umbe tu ili wapate nafasi ya wizi.

Pili, hivi mbunge wa znz anapokuwa katika kamati za bunge za serikali za mitaa , hizo zinamhusu nini.

Tatu, mbunge wa znz anapojadili wizara ya afya hiyo inamhusu nini.

Tena umethibitisha kuwa wanapokuja ni kulala tu, maana mambo wanayojadili ni chini ya 4. Kwanini tuwalipe mabilioni ya pesa ikiwa umesema ipo siku hawaingii bungeni, you mean wanakuja kulala Dodoma.

Gavana aanasema hawa wanachingia sifuri, period. Mfuko wa muungano haupo uliopo ni ule wa Tanganyika ambao znz imeugeza shamba la bibi. Kama hawawezi kuchangia kwvile hakuna mfuko, mishahara wanachukua kutoka wapi?
Watoto wao wanaosoma bure wanasomeshwa na mjomba gani? Hao watalii 84 wanalipwa na mfuko gani.
Bajeti yao ambayo nusu inatoka Tanganyika, inatoka mfuko gani.
 
Unaelewa nini kuhusu Mambo ya Muungano? ebu tupe list yake hayo mambo 22 kisha tazama maneno yako hapo juu halafu twambie inahusiana vipi na mapato yake..
 
Mkuu wangu wee mbunge ni mwakilishi wa sera za chama ktk utekelezaji wa kazi zake bungeni. Hili ni taifa moja huo Uzanzibar unauweka wewe na akili yako ya kibaguzi. Hata wewe unaweza kuwa mbunge wa kamati za Zanzibar. Karume, Mwinyi, Salim, Jumbe hawa wote walikuwa wabara kwa makazi na wengine asili zao na bado walitawala siasa za zanzibar - Chaa ajabu kipi?
 
kila siku tumekuwa tukizungumza hapa juu ya hatima yetu ya muungano. Mie nasemai kwann uwepo ugumu katika kuirudisha tanganyika ambayo iliuwawa kimazingira?

sawa mwl kwa nafasi yake alifikia hapo alipofika katika kuutengeneza Muungano. na ukweli ni kwamba yeye na mzee wetu Karume tutawasifu kwa hilo. Lakin nafikir kazi ya kuurekebisha huu Muungano mbona sasa ni kazi ya wengine tuliopo kwa sasa?

unless kama watu tumesahau yaliyotokea wakati wa kuanzishwa kwa vyama vingi, watu tulihofia machafuko mpaka mwl aliposema wapeni watu kile wakitakacho baada ya kura maoni kuonyesha hilo. Naamini hata mwl angekuwepo lazima angeridhia leo hii mawazo/maoni ya wanachi yapewe kipaumbele.

hata hii england tunayoisemea miaka 300 sio midogo, na huenda ile misingi iliyoasisi Muungano wao haipo tena baada ya kuonekana kwamba aipapply na hivyo wamekuwa wakirekebisha kila mara hadi kufikia leo.

ilichokifanya scotland ni mfano mzuri kwa sisi tulio leo ambao pengine tu wadogo sana since mara ya mwisho walipofanya marekebisho.

sisi hatuupingi muungano na wala hatujawah kusema tunataka uvunjike ila tunataka marekebisho kwamba kila nchi ibaki kuwa tawala binafsi ila iwepo serikali ya muungano ambayo itatukutanisha.

lakin kwenye mambo ya nchi binafsi yabaki kuwa ya nchi binafsi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…