Scopolamine/ Burundanga: Madawa ya kulevya hatari duniani

orangutan

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
757
773
scopolamine_butyl_bromide_cas_149_64_4_plant_extract.jpg

vice-world-scariest-drug-Scopolamine-devils-breath.jpg

Scopolamine ni madawa ya kulevya yanayotengenezwa kutokana na ungaunga wa mbegu za matunda ya mti unaoitwa kitaalamu "borachero tree". Miti hii inapatikana kwa wingi huko Bogota, Columbia. Baada ya hapo huo ungaunga hufanyiwa chemical processing kama ile inayofanyika kwenye cocaine, na ndipo scopolamine inapopatikana (density yake na muonekano wake unawiana kwa karibu sana na cocaine). Madawa haya yanafahamika kwa jina la "burundanga" huko Columbia na madawa ambayo kwa mujibu wa tafiti za wataalamu wa madawa wameyathibitisha kuwa ndio madawa ya kulevya hatari duniani.

Madawa haya mara zote huwa hayatumiki kwa ajili ya starehe, bali hutumika kwa ajili ya uhalifu ambao mara nyingi hufanywa na makahaba, wezi, majambazi na 'gang members' kwa ajili ya kuwadhuru wabaya wao.(Unaweza kupewa haya madawa kwa njia ya kupuliziwa, au kuwekewa kwenye kinywaji au chakula, kupewa kitu kilichopakwa huo unga-kama cards, au hata makahaba kumkisi muhusika kwa lipsi zenye madawa hayo huku wao wakiwa wamejikinga kwa kuchomeka pamba ndani ya pua).
Sifa kubwa ya haya madawa ni kwamba pindi mtu akipuliziwa tu unga wake (ndani ya sekunde tu!) basi ubongo wake hupoteza uwezo wa kutambua kile anachokifanya na muhusika atafanya kila kitu anachoamriwa na huyo aliempulizia (Mhusika nakuwa kama Zombie).

Watu wengi waliopuliziwa haya madawa wamejikuta wakiamriwa kwenda kutoa fedha kutoka kwenye bank accounts zao, kukabidhi mali zao bila kujielewa, kujikuta wakisaini documents bila kujielewa, au hata kukubali kufanywa vitendo vibaya na hao wabaya wao. -Lakini punde nguvu ya hayo madawa ikiisha muhusika huwa hakumbuki chochote alichokifanya tangu apuliziwe huu unga hatari. (Labda asimuliwe na mashuhuda).
Hatari nyingine kuhusu huu unga hatari ni kwamba ukimpulizia muhusika unga mwingi (over-dose) chance ya kupoteza maisha ni kubwa sana. Gramu moja ya scopolamine ina uwezo wa kuua watu wazima 10-15.
Haya madawa yamepachikwa jina la utani kama"devil's breath", kwasababu pindi tu ukipuliziwa huu unga, muhusika anaonekana yupo kawaida kabisa wala haonekani kuonyesha dalili yoyote ya kulewa kama kuyumbayumba au kusinziasinzia lakini muhusika hufanya kila kitu kama vileanavyoamriwa na wabaya wake (loss of freewill) nayeye anakuwa hana uwezo wa kutambua kile anachokifanya . Pindi nguvu ya madawa inapoisha muhusika hujikuta kajifanyia uhalifu kwa mikono yake mwenyewe lakini huwa hana kumbukumbu ya kile akichokifanya au watu waliomfanyia hicho kitendo hadi siku anaingia kaburini!
2_world%E2%80%99s-dangerous-drug.jpg


kWA hisani ya vyanzo mbalimbali.
 
Hayasaidii mtu kukurupuka!!!! maana naona kuna dalili zote za ingredients.

Na Colombia na Jamaica siyo mbali kiivyo.
 
dahh!! wataalamu embu watufafanulie yanafanyaje kazi haya makitu asee??
 
Mkuu huu unga kibongobongo ni ngumu sana kupata. Yanapatikana kwa ugumu sana huko Bogotá na medellin , Columbia
 
Back
Top Bottom