Science is the Savior of Humanity

Science is the Savior of Humanity

Spinozist

Senior Member
Joined
Feb 26, 2025
Posts
120
Reaction score
161
Science is the Savior of Humanity

Imekuwa ni jambo la kawaida sana kukutana na maandiko ya watu wakisifu miungu yao na imani zao. Lakini ni mara chache sana kukutana na maandiko yanayoeleza mambo makuu na ya kishujaa yaliyofanywa na binadamu wachache waliojitolea kwa dhati kuisaidia jamii kupitia gunduzi na tafiti mbalimbali za kisayansi.

Ufuatao ni uchambuzi mfupi unaoeleza kwa nini sayansi inapaswa kutazamwa kama mkombozi wa kweli wa binadamu katika kutatua matatizo ya maisha ya kila siku.

1. Sayansi imeongeza umri wa kuishi wa binadamu

Sayansi imeweza na itaendelea kuwezesha binadamu kuishi maisha marefu zaidi ukilinganisha na karne zilizopita. Leo hii kuna chanjo nyingi dhidi ya magonjwa ambayo zamani yalikuwa tishio kubwa kwa maisha ya watu.

Bila ugunduzi wa “germ theory of disease”, hakuna ambaye angeelewa chanzo cha magonjwa mengi wala namna ya kuyatibu. Thibitisha hili kwa kulinganisha idadi ya watu (population) ya miaka ya 1990 na ya mwaka 2022 – utaona ongezeko kubwa sana la watu duniani.
Sasa jiulize: kama watu wangelitegemea tu maombi, ibada, kufunga, au hija, je magonjwa kama polio, tetekuwanga, surua na mengine yangeweza kutokomezwa kupitia chanjo?

2. Kupungua kwa vifo vinavyoweza kuzuilika

Vifo vilivyokuwa vinaepukika vimepungua kwa kiwango kikubwa. Mfano mzuri ni kupungua kwa kiwango cha vifo vya watoto wachanga (Infant Mortality Rate). Haya yote ni matokeo ya maendeleo ya sayansi na huduma za afya.
Leo hii mama mjamzito anaweza kuchagua kujifungua kwa njia ya kawaida au kwa upasuaji salama. Jiulize bibi zetu wa miaka ya 1500 walipitia changamoto kiasi gani wakati wa kujifungua, na ni watoto wangapi walipoteza maisha kutokana na kukosekana kwa tiba na teknolojia ya kitabibu?
Je, matatizo hayo yangetatuliwa kwa maombi peke yake, mafuta ya upako, au dua?

3. Nishati ya umeme – zao la fikra za kisayansi
Nishati ya umeme kwa sasa ni hitaji muhimu sana kwa binadamu. Maisha ya kisasa hayawezi kuendelea bila umeme: mawasiliano, hospitali, elimu, viwanda, usafiri na hata shughuli ndogo kama kupasi nguo au kuhifadhi chakula.
Haya yote ni matokeo ya kazi za watu waliotumia akili na utafiti wa kisayansi hadi kugundua misingi ya umeme kama “Direct Current (DC)” na “Alternating Current (AC)”.
Jiulize: kama Nikola Tesla na wanasayansi wenzake wangesubiri maono ya kimiujiza badala ya kufanya utafiti, je leo tungekuwa na umeme wa maji (Hydroelectric Power) au mitambo ya kisasa?

4. Mapinduzi katika sekta ya usafiri
Usafiri ni nguzo muhimu ya maisha ya binadamu, hasa mijini. Biashara, elimu, afya na shughuli za kijamii zote hutegemea usafiri.
Magari, meli na ndege havikutokea tu kwa bahati mbaya. Ni matokeo ya tafiti, majaribio na ubunifu wa kisayansi. Leo mabilioni ya watu wanatumia vyombo vya moto bila hata kufahamu kwa undani jinsi injini zinavyofanya kazi.
Kama ndugu Wright (Wright Brothers) wangelisubiri maono badala ya kufanya majaribio ya kisayansi, je leo tungekuwa na kitu kinachoitwa ndege?

5. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Tunatumia simu na intaneti kila siku, lakini wengi hatujui namna mawimbi yanavyosafiri na kubadilishwa kuwa sauti au maandishi kwa umbali wa maelfu ya kilomita.
Leo mtu aliyeko Tanzania anaweza kuzungumza na mtu aliyeko Marekani, au hata kuwasiliana na chombo kilicho angani. Haya yote ni matokeo ya sayansi na teknolojia, si miujiza.
Maendeleo ya hivi karibuni kama Akili Unde (Artificial Intelligence) yanaonesha wazi kuwa mustakabali wa binadamu unategemea zaidi sayansi kuliko chochote kingine – hasa kwenye afya, elimu na biashara.

Hitimisho
Hayo ni machache tu kati ya maelfu ya mafanikio ya sayansi.
Maarifa ya kisayansi hayahitaji kuabudiwa wala kusifiwa kama dini. Yanahitaji kusherehekewa, kujadiliwa na kufundishwa kwa uhuru kwa ajili ya kujenga kesho iliyo bora zaidi.

Not by Almighty
But by Rationality
Not by Grace
But by Effort
Embrace Reality
 
Naomba unisaidie hayo maandiko yana maana gani Ndugu
Ukosoma 1 Petro 21:3 vizuri;
Petro hakuwa akizungumzia jehanum wala wokovu. Alikuwa akizungumzia namna Mkristo anavyopaswa kuishi kwenye jamii.

Petro alikuwa anaandikia Wakristo waliokuwa wanaishi chini ya utawala wa Kirumi ,waliokuwa wanasingiziwa uasi, vurugu, na machafuko
“Tiini kila amri ya kibinadamu kwa ajili ya Bwana…”
Tunafanya vitu kwaajiri ya Bwana, kufuata mafundisho ya kikristo utajifunza mambo mengi nje ya kuw ana imani tu, utaje ga tabia nzuri na kuepuka mambo maovu! Hivuo Petro alifundisha kwa kulenga watu washi kwa nidhamu na kuheshimu mamlaka zilizopo.

Usitumie uhuru wa Kikristo kama kisingizio cha uasi na lengo la Petro halikuwa hofu ya jehanum

“Kwa maana kufanya mema ndivyo kumpendeza Mungu, mkiziba vinywa vya watu wajinga.” (1 Petro 2:15)
lego lake halikiwa la namna hiyo unalojaribu kuliekezea hapo juu
“Imempasa Mungu kutiiwa kuliko wanadamu.”(Matendo 5:29)
Kwahiyo Utii wa mamlaka una mipaka Ukipingana na mapenzi ya Mungu, Mkristo anachagua Mungu

kwa kifupi, Alimaanisha tutii sheria zilizowekwa na mamlaka na sio kila kilichokatazwa ndio dhambi ya milele
Kwanza sio kila kosa hukumu yake ni ya jehanum

Mafundisho ya 1 Petro 2:13 ni mafundisho ya nidhamu na ushuhuda,
sio andiko la kutisha wokovu.

Kaangalie warumi 13:1 pia hili somo lipo wazi tu.
 
Okay mkuu nashukuru kwa maelezo hayo.
Mimi nina swali: Ikiwa serikali ya Tanzania imefungia mtandao wa jamiiforums kutumiwa, halafu wewe ukaamua kutumia ujanja wa VPN ili uweze kuutumia, Je hapo wewe unakuwa umekiuka mamlaka ya raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Halafu pia, nitaomba unipe maelezo ya nini maana ya kukiuka/kutotii mamlaka?
Ukosoma 1 Petro 21:3 vizuri;
Petro hakuwa akizungumzia jehanum wala wokovu. Alikuwa akizungumzia namna Mkristo anavyopaswa kuishi kwenye jamii.

Petro alikuwa anaandikia Wakristo waliokuwa wanaishi chini ya utawala wa Kirumi ,waliokuwa wanasingiziwa uasi, vurugu, na machafuko

Tunafanya vitu kwaajiri ya Bwana, kufuata mafundisho ya kikristo utajifunza mambo mengi nje ya kuw ana imani tu, utaje ga tabia nzuri na kuepuka mambo maovu! Hivuo Petro alifundisha kwa kulenga watu washi kwa nidhamu na kuheshimu mamlaka zilizopo.

Usitumie uhuru wa Kikristo kama kisingizio cha uasi na lengo la Petro halikuwa hofu ya jehanum

lego lake halikiwa la namna hiyo unalojaribu kuliekezea hapo juu

Kwahiyo Utii wa mamlaka una mipaka Ukipingana na mapenzi ya Mungu, Mkristo anachagua Mungu

kwa kifupi, Alimaanisha tutii sheria zilizowekwa na mamlaka na sio kila kilichokatazwa ndio dhambi ya milele
Kwanza sio kila kosa hukumu yake ni ya jehanum

Mafundisho ya 1 Petro 2:13 ni mafundisho ya nidhamu na ushuhuda,
sio andiko la kutisha wokovu.

Kaangalie warumi 13:1 pia hili somo lipo wazi tu.
Okay mkuu nashukuru kwa maelezo hayo.
Mimi nina swali: Ikiwa serikali ya Tanzania imefungia mtandao wa jamiiforums kutumiwa, halafu wewe ukaamua kutumia ujanja wa VPN ili uweze kuutumia, Je hapo wewe unakuwa umekiuka mamlaka ya raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Halafu pia, nitaomba unipe maelezo ya nini maana ya kukiuka/kutotii mamlaka?
 
Okay mkuu nashukuru kwa maelezo hayo.
Mimi nina swali: Ikiwa serikali ya Tanzania imefungia mtandao wa jamiiforums kutumiwa, halafu wewe ukaamua kutumia ujanja wa VPN ili uweze kuutumia, Je hapo wewe unakuwa umekiuka mamlaka ya raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?
Sababu za kuifungia forum zina mashiko? Nikiingia kwenye forum nafanya kosa lipi? Kama simvunjii heshima kiongozi au mtu yoyote sioni sababu ya kufuata hiyo sheria! Nimekiuka mamlaka kwa na sababu zionajulikana ninz akishenzi siweiz kufuata na hilo halinipeleki mimi motoni! Kwani nyumbani kwenu ukiambiwa usipende kula kwa watu ukienda kula wanakuua? Ndiomaana kuna neno linasema lifunguliwalo duniani na mbinguni limefunguliwa, kwani hakuna viongozi washenzi? Hakuna ndoa za ajabu? Hakuna institutes na makundi ya kishenzi?
Halafu pia, nitaomba unipe maelezo ya nini maana ya kukiuka/kutotii mamlaka?
Kukiuka ni kwenda kinyuma na matakwa ya mamlaka.
 
Waiting for science to disprove God is like waiting for a map to erase the land: the more accurate the map becomes, the more real the world appears.

Its like expecting a mirror to hide the face: the clearer the reflection, the more undeniable the presence.

It's like searching for darkness in the heart of the sun: the deeper you look, the more light you find.
 
Back
Top Bottom