please guys kuna nafasi zilikua zimetangazwa za kazi UK, zile kazi ni scam na sio za kweli ni wanaigeria wanataka kutake advantage ya matatizo ya kazi kama mnavyojua sasa hivi tuna wanaigeria wengi sana bongo especial pale sinza hawana kazi cos hawana work permit kwa hio kazi yao ni kushinda kwenye ma internet cafe na kufanya ile kazi wanayo ifanya kule kwao ya kuiba kupitia mitandao wao wanaiita 419, sasa zile kazi ukiomba wanajifanya umepata then wanakutengenezea contracts harafu wanakupaa email wao wanaseme ni ya UK immigration which is not, then wanasema uwatumie hela ya visa, infact wako smart kidogo, so please msiingie kwenye mitego yao, hio kazi ilikua ya hotel ya five star inaitwa HOTELEDENPLAZA, UK. hizi kazi za nje inabidi tuwe makini kidogo na hawa watu wa mitandao ya kazi please wajaribu hata ku verify kidogo mtu akiwapa kazi wa post ili kuwasaidia watanzania wenzao wasiibiwe, si unajua kitaa kunachosha so mtu anaweza kuingia king kilaini sana cos of Desperation.