Tz boy 4tino
JF-Expert Member
- Sep 14, 2014
- 1,598
- 1,816
Wataalamu wa magonjwa ya kuambikiza Duniani kwa umoja wao wakiri kutofahamu kwa nini nchi za Kiafrika hazijaathirika kwa kiwango sawa na nchi nyengine Duniani.
Wataalamu hao wamesema , “ Hali ya ugonjwa wa Corona katika nchi za Afrika hata wao zinawashangaza”. Wengi wamekiri kuwa wakati ugonjwa unaanza kusambaa Duniani walitegemea hali itakuwa mbaya zaidi katika bara la Afrika kutokana na msongamano wa watu, umasikini na uwezo wa mdogo wa serikali za kiafrika kupambana na magonjwa. Lakini hali imekuwa tofauti na walivyotegemea kwani Afrika ndiyo bara lililoathiriwa kidogo zaidi na ugonjwa huo.
Wanasayansi hao pia wamekiri kushangazwa zaidi kwani kuna baadhi ya nchi zilizomo nje ya Afrika kama Brazil na India pia zina masikini wengi na msongomano wa watu katika makazi tofauti na Afrika hizo nchi zimeathirika sana. Jambo ambalo linalozidi kuwachanganya, kwa nini Waafrika peke yao ndiyo wanaonekana kupona katika janga hil??.
Tafiti hii imefanywa na wanasayansi wa Marekani wakishirikiana na wale wa Afrika Kusini, Uingereza na India . Na kuripotiwa na New York Post ya Marekani.