Sauti ya umauti masikioni mwangu

Daaah pole sana lakini umenikumbsha Mwaka 2022
Sisi mkubwa anaumwa mdgo wangu wa mwsho anaumwa na mm nnaumwa ila nlmficha bi mkubwa nilitoka msaada Kwa ssta ma dogo wakawa sawa mm.
Niko Hali mabya Sana, yaan nilfikia hatua ya kufa yaan Ile unakiona KIGo yaan unaona kabsa gari ya matiti inakuja kukufata afu ndugu zako wanalipa, usku ndo usiseme, kijoto chepesii, kibaridi, Ile kutetemka, Ile mavi yanatka kutka na roho inatka kuchomoka,
Yule binti nilikuwa nae na mtoto wangu mdgo, anasema jamn mm ndo nitaonekana muuaji usife baba flani, jamaniii.
Nashukuru Sana Mtumishi wa Mungu Mwamposa
Afya ilirudi maana yalikuwa mambo ya kishrikina Yale,
Pole mkuu! Nimeamini sisi binadamu tunapitia meng sana. Ukimtazama mtu usoni n kama yuko poa, kumbe yuko hoi, na anayeonekana anashida fulani kumbe ndiye afadhari hana shida kubwa. Shida zetu zingekuwa zinaonekana laivu au zinabebwa kama gunia la mahindi, bc wengine hapa tungekuwa hatuwezi kuzibeba.
 
N hatr aiseeh yaan ukiambiwa mtu kufikia hatua y kufa ndo Ile nilikuwa nmefikia Mimi. Hii Dunia Ina mengi sana
 
Habari ya usiku wana jf!

Leo ninayofuraha kuweka bando kwenye simu yangu baada ya siku nyingi bila kuweka bando!

Kwanini hiyo heading! Ipo hivi, mm kijana wa miaka 28.6, lakini nipo kama mtu mzima wa miaka 40. Sijaoa wala sina mtoto. Maisha nayoyaishi hiki kipindi sidhani kama Mungu ndiye aliyepanga niyaishi. Naishi maisha ya ovyo sanaa. Nimelelewa na mama tu na ndiye aliyenipambania hadi kupata haka kaelimu ka ovyo ambako hakana msaada na mm kabisa.

Ipo hivi, mwaka huu tangu uanze sina hamu nao tena maana ulikaribishwa kwa majanga ya kuanza kumwuguza mama yangu. Toka mwezi wa 11 hadi huu mwez wa tatu ndo bi mkubwa amerudishwa nyumbani. Nimempambania ili nisije kubaki na uchungu hapa duniani kama mama angefariki. Ningejiona sina maana kabisa ukizingatia mama aliza vitu vyake vyote ili anisomeshe mm akiamini nikipata ajira nitamtunza. Marehemu hasemwi vibaya ila utawala wa mwamba umeniharibia future yangu kwa 100%.

Tuachane huyo marehemu na utawala wake,. Baada ya mama kulazwa ilibidi nitoe hela yangu yote hadi hela iliyokuwa kwenye biashara nikatoa yote. Haikutosha ikabidi nianze kukopa hela kwa wakopeshaji wa mitaani maana walikuwa wananiamin kuwa nitawalipa maana nilikuwa nafanya biashara na wao wanaona. Nimeingiza deni kubwa sana saiz linasoma milion 6. Mimi sina ata mia mbovu, yan ata cha kuuza. Uwanja nilishauza muda. Sasa jana nimeambiwa na mmoja wa watu niliowakopa akaniambia "nitakudai kwa namna nyingine" hii kauli imenitisha sanaa, niliwaza nitakamatwa na police ila nahisi hapana ni uchawi utatumika na jana usiku nimelala vibaya sijui n wenge sijui ndo simu ya kifo yenyewe hiyo nilipigiwa ndotoni!

Mwisho mimi nina amani kuona nimemsaidia bi mkubwa. Lakini pia nina huzuni maana nahisi nakufa muda wowote na nawaza mama atasikiaje habari ya mimi kufa, nawaza mchumba niliyekaa nae miaka mitatu akinisubiri nimuoe atasikiaje habari ya mm kufariki. Kiufupi hicho ndo kinanitisha. Lakini acha iwe hivo tu maana sina uwezo wa kulipa hizo hela mimi.

Makala ni ndefu poleni ila nawaomba tuwapende mama zetu, usimtendee baya mama yeyote huendi ndiye mama yangu ambaye nitamwacha pekee yake hapa duniani bila uwepo wangu. Upendo ni amri kuu ya Mungu!
usjali bro,,,MUNGU yupo atakusaidia!!!!! sali sana utaishinda ROHO YA MAUTI"..........kama muislam mtafute sheikh atakusaidia,,kama mkristo mtafute mchungaji atakusaidia,,,,,usikate tamaa kabisa!!
 
usjali bro,,,MUNGU yupo atakusaidia!!!!! sali sana utaishinda ROHO YA MAUTI"..........kama muislam mtafute sheikh atakusaidia,,kama mkristo mtafute mchungaji atakusaidia,,,,,usikate tamaa kabisa!!
Asante Mkuu. Nam saiz nimeamua nitaishi . Hakika sitafariki. NITAISHI
 
Hii post imenipa picha Halisi jinsi Hili jukwaa lilivyojaa watu wabinafsi na Wasiojali Lolote kuhusu wengine.

Mtu anacomment utani na mzaha amekaa yuko baa anaendelea na Bia ya 12.. Ivi ukifia hapo utasema ni mapenzi ya nani? Sijui hii Jamii inakoelekea ila Kwa picha hii Mbele ni Giza Totoro.

N wale wanaopigia chapuo mifumo ya Kueneza ubinafsi wanazidi kujiona washindi.

Badilikeni kungali mapema. Bei na thamani ya Binadamu iko kwa kwa kuwajali wengine.

Usipozingatia hilo huna tofauti na mbwa anaepita hapo jalalani.
 
Umewaza mbali mkuu. Mm nilizipuuza maana naishi na huu msemo wa "Huwezi kuujua uchungu wa msiba ukiwa kwa jirani yako, mpaka ukufike miguuni kwako". Ukiufahamu vzr huu msemo hutahangaika kuhusu binadamu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom