PostGE2025 SAUTI YA MABADILIKO –Ujumbe kwa watanzania wote na Roma Mkatoliki

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

uhuruborn

Member
Joined
Sep 6, 2025
Posts
81
Reaction score
304
Katika safari ya kudai mabadiliko ya kweli nchini, kumekuwa na misimamo tofauti, shutuma, dhihaka na hata manyanyaso yanayowakumba wale wanaosimama kidete kutetea haki, uhuru na ustawi wa taifa. Wapo wanaotubeza, wanaotukejeli na hata wanaofurahia mateso ya wapigania mabadiliko. Lakini katika yote haya, jambo moja limesimama imara: mapambano haya si ya mtu binafsi ni ya vizazi vyote vya Watanzania.

1. Kutoona Umuhimu Leo, Lakini Kesho Itachelewa

Wapo wanaodharau harakati hizi kwa sababu ya nafasi walizo nazo leo. Labda wanahisi mifumo iliyopo inawanufaisha au angalau haiwasumbui. Lakini historia imeonyesha mara nyingi kwamba siku moja watu hao hao hujikuta wakitamani lau wangeunga mkono mapambano ya jana. Wakati huo huwa ni TOO LATE.

2. Ujumbe kwa Askari Wanaotumika Kuwatesa Wananchi

Askari wanaoshiriki kuwapiga, kuwatesa au kuua wananchi leo, wafahamu kuwa hatima yao ipo mitaani wakistaafu, wakazeeka, wakiwa wagonjwa, wakiwa na mzigo wa gharama za maisha na watoto wasio na ajira. Watagundua matatizo ambayo wapigania mabadiliko wanapiga kelele leo ndiyo yatakayokuwa yanawaumiza kesho.
Na hapo ndipo watakumbuka siku walizoshiriki kuzuia mabadiliko ambayo yangewasaidia wao wenyewe na familia zao. Wataona wazi kuwa walitumika vibaya na watawala, kutugombanisha sisi maskini huku wao wakichota na kugawana rasilimali za nchi.

3. Tunachopigania si Vyama – Ni Mabadiliko ya Mfumo

Mapambano haya hayalengi chama fulani kuingia madarakani. Hayalengi Chadema, ACT, Chauma au kingine chochote. Tunapigania mfumo sahihi wa kuongoza nchi mfumo unaowawajibisha viongozi, unaolinda raia, unaotupa haki, na unaohakikisha utawala wa sheria. Hata chama kikichukua nchi bila mabadiliko ya mfumo, kitafeli tu kama waliotangulia.
Ndiyo maana wasanii, wanaharakati na raia wengi wamelenga kwenye agenda:
Rushwa, ufisadi, utekaji, haki, ajira, elimu bora, afya bora—na siyo majina ya wagombea.

4. Kwa Nini Raia Wanataka “Mbadala wa Watawala”?

Kwa sababu walio madarakani wameshindwa kutekeleza mambo ya msingi ambayo wananchi wameyataka kwa muda mrefu. Wamepoteza lugha ya wananchi, wamepoteza uhalisia, na wamekuwa mbali na utesi wa wananchi. Ndiyo maana Watanzania wanatafuta viongozi wapya wanaoishi uhalisia wao na kuzungumza matatizo yao.

5. Lengo Kuu: MABADILIKO YA KIMFUMO

Hili ndilo lengo namba moja. Tuanzie kwenye:
  • Namna ya kuwapata viongozi
  • Utendaji wa serikali
  • Uwajibikaji wa mihimili
Hapo ndipo tunahitaji katiba mpya isiyoegemea chama tawala, uchaguzi huru na wa haki, uhuru wa vyombo vya dola, haki kwa kila raia, uwajibikaji wa viongozi na uhuru wa kutoa maoni bila vitisho.

6. Ni kwa Nini Watu wa Nje Ndio Wanaonekana “Too Vocal”?

Kwa sababu ndani ya nchi wengi wanaogopa. Sauti zao zimefungwa. Lakini Watanzania walioko nje wana uhuru wa kuongea, wanaona unyanyasaji unaofanyika, wanasikia kilio cha ndugu zao, wanajua jinsi mambo haya yanaweza kurekebishwa kwa sababu huko waliko hakuna mateso kama haya.
Ndiyo maana wanasema:
WE ARE THE VOICE OF THE VOICELESS.

Kuwatuhumu kuwa wanalipwa na wageni ni hoja dhaifu. Haiwezekani mzungu amlipa mtu kulaani mauaji au kudai maji Ubungo! Kama ingekuwa hivyo, basi huyo mzungu angekuwa mwema sana kuliko viongozi wetu.

7. Ukweli wa Hali Halisi Ndani ya Nchi

Maisha yamekuwa magumu:
  • Maji kukatika kwa mwezi mzima​
  • Ajira hakuna​
  • Kodi zimekuwa kero​
  • Bima ya afya haina tija​
  • NSSF inatesa wastaafu​
  • Utekwaji na ukandamizaji wa uhuru umeongezeka​
Haya ndiyo yanayowafanya Watanzania walioko nje kuwa sauti ya kulalamikia mfumo ulioshindwa.

8. Wasiowazimia na Kuwabeza Walioko Nje Watajuta

Wako watu wanaowadhihaki Watanzania walioko nje bila kujua kuwa hawa watu wanateseka pia. Wanawindwa, wanaishi kwa hofu, na mara nyingi wanabeba mzigo wa kukemea kwa niaba ya walio ndani.
Siku wakinyamaza ndipo taifa litajua thamani yao.

9. Watawala Wanaendelea Kutuchezea

Watawala wanatuzuga kwa maneno matamu na mbinu za kutugawanya. Wanawaalika wananchi kula, lakini chakula kiko mbali na hawana nia ya kukitoa. Ni mchezo wa madaraka na maslahi binafsi.
Hadi hapo, Watanzania wanapaswa kukaa kimasta, kutumia akili, kutafakari na kusimama kidete kwenye madai ya mabadiliko ya kimfumo.

HITIMISHO

Mabadiliko tunayoyapigania leo si kwa ajili ya kundi fulani ni kwa ajili ya taifa zima na vizazi vijavyo. Siku moja, kila Mtanzania ataona umuhimu wake. Wanaodharau leo, watatamani lau wangeunga mkono mapema.

Lakini wakati huo utakuwa tayari umeshachelewa.
 
Point namba 2 hapo, mifano tuanyo:-
1. Polepole.
2. Majaliwa.
3. Mpango.
4. Gwajima.
5. Mwambieni.
6. Jenister.
7. Tulia
 
Bwana Roma, kwanza poleni sana kwa yaliowapata. Mabadiliko na mageuzi ni harakati endelevu kamwe hazimaanishi kuhamasisha, kuchochea au kuunga mkono Mapinduzi yanayolenga kuihujumu na kuangusha serikali inayoongoza.

Mlikosea sana mlipokubali kulaghaiwa na kuungana na wale waliotaka kutumia njia zisizo rasmi na sahihi kupindua serikali. Iwapo mngefanikiwa hii nchi leo ingekuwa haikaliki tungehitaji walau miaka mingine walau 30 kurudisha serikali ya kiraia ni msaada upi huo mlikuwa mnatupa?

Mabadiliko haimaanishi kuwashambulia watu ama biashara zao au kufanya matukio yanayopelekea kuhatarisha maisha ya wengine, miundombinu au hata biashara zinazowapa mkate wao. Mliunga mkono mambo yanayolenga kulinda maslahi ya wachache huku wengi wakibaki wanatota kwenye jasho.

Nchi inabadilika na itaendelea kuwa hivyo suala litabaki wewe utakuwa upande upi. Wa wale wanaosaidia mabadiliko na mageuzi yatokee bila madhara, antagonist, anarchist au extremist ambaye kila kitu wewe ni kupinga tu so long as kimefanywa au kusema na yule unayetofautiana naye mtazamo!

Kazi kwako na kundi lako Mlitaka hii nchi iwake moto mkiwa mnafahamu sio kila Mtanzania ana uwezo kama wenu wa kupata green card au hata pasi ya kusafiria kukimbia nchi machafuko mliyokuwa mkiyachoche yakitamalaki.

Mmejiweka humu mtandaoni kutaka muabudiwe na kila mtu kwamba hamkosei na hampaswi kukosolewa. Hata hivyo nadharia hiyo siyo sahihi hivyo basi jirudini mtubu, mtasamehewa!
 
Back
Top Bottom