SoC01 Sauti moja ya vijana ni suluhu ya changamoto zote za vijana

Stories of Change - 2021 Competition

kadizy

New Member
May 5, 2019
1
1
UMUHIMU WA KUWEPO KWA BARAZA LA VIJANA LA TAIFA KAMA NJIA BORA ZAIDI YA USHIRIKISWAJI WA VIJANA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO NA KULIJENGA TAIFA.

Habari za wakati huu ndugu msomaji, IKO WAZI KUWA TUTAKUBALIANA kwamba vijana ndio nguvu kazi ya taifa, lakini pia vijana hawahawa ndio wanakumbana na changamoto ya ukosefu wa ajira, swali la kujiuliza je, Nguvu kazi hiyo inatumika wapi kama vijana hawana ajira? Kupitia swali hili utajua taifa letu linashindwa kwenda kasi kwakua vijana wanaopaswa kufanya kazi na wao wamekua tegemezi licha ya kuwa na viwango vikubwa vya elimu, hivyo utagundua kupitia ukosefu wa ajira rasilimali watu kubwa haitumiki vile ipasavyo na vijana wanashindwa kushiriki au kushirikishwa vizuri kuijenga nchi yao kiuchumi.

PIA TUTAKUBALIANA KWAMBA Uchumi wa jamii au nchi huendeshwa na mifumo mbalimbali ya kisiasa na kijamii, hivyo kama ushirikishwaji au ushiriki wa vijana katika mifumo hii ya kisiasa na kijamii ni mdogo basi nguvu kazi hii itaendelea kupotea na kubaki kuwa kero kwani vijana wasio na kazi wanaongezeka siku hadi siku..

Sasa tusihangaike kumtafuta mchawi ni nani, tazama kwanza hizi sifa za vijana. Vijana wanasifa ya kuwa na utimamu wa mwili na akili, wachapaka kazi na wabunifu, wavumilivu na wastahimilivu n.k. kama hizi ndizo sifa zao basi jiulize maswali yafuatayo:-

(i) Kwanini watu ambao sio vijana wazungumze, wapange na watoe maamuzi kwa niaba ya vijana ambao wanaweza kuzungumza, kupanga na kufanya maamuzi mwenyewe juu ya mambo yenye maslahi kwao na kwa taifa?

(ii) Je, wanauhakika wanachokisema au kukizungumza, wanachokipanga na hata maamuzi wanayoyafanya ndio hayo hayo vijana wangefanya au wanavyotaka yafanywe?

Ndugu msomaji nafikiri tutakubaliana kuwa SIO SAWA kutenda jambo kwaniaba ya mtu ambaye anaweza kutenda mwenyewe kwakua anayelala na mgonjwa ataishia tu kusikia sauti za kuugulia kwa mgonjwa lakini maumivu ya ugonjwa anayajua vizuri mgonjwa. KWAHIYO ikitokea mgonjwa anauwezo wa kuelezea hali yake basi apewe nafasi ya kufanya hivyo na sio muuguzi kupambana kueleza kwaniaba yake kwasababu itachelewesha kupata suluhu ya ugonjwa wake.

Ninachojaribu kukuonesha ni chimbuko la matatizo yanayowakabili vijana ya kwamba vijana ndio wanaoujua uchungu wa kukosa ajira pamoja na matatizo mengine, hivyo naamini vichwani mwao zipo njia bora na zenye matokeo chanya na endelevu kwaajili ya kutatua matatizo hayo LAKINI HAWAJASHIRIKISHWA KWA NAMNA BORA ZAIDI katika kutatua, isipokuwa wapo wanaouvaa ujana nakujaribu kutafuta suluhu jambo ambalo ni zuri lakini haliwezi kuwa zuri Zaidi ya vijana wenyewe kupewa jukumu hilo.

KOSA KUBWA tunaloendelea kulifanya vijana ni KUWATEGEMEA waliojivika ukijana kututafutia suluhu ya changamoto zetu wakati huohuo tunajua kabsa mtegemea cha ndugu hufa maskini. Kinachonipa nguvu ya kuendelea kuandika Makala hii ni kwamba jambo hili linaepukika na kabla sijakueleza njia yakuliepuka nikupitishe katika SABABU KUU 3 ZA KUTOWATEGEMEA WASIOKUWA VIJANA KUTUTAFUTIA SULUHU YA MATATIZO YETU:-

(1) Wao wanamchango mkubwa wa sisi vijana kuwemo na kuendelea kuwemo katika matatizo hayo hususani ukosefu wa ajira. Hii nikupitia mifumo mbalimbali ya kiutawala inayoongoza nchi hususani mfumo wa elimu ambao kwa Zaidi ya miaka 17 mfumo unamuandaa kijana kuajiriwa, kwa zamani ulifaa sana lakini kwasasa unahitaji kufanyiwa marekebisho kutokana nakuwa zama zimebadilika wasomi ni wengi tofauti na zamani. Lakini wale tunaowategemea watuboreshee mfumo uendane na matakwa ya dunia ya sasa bado wanaung’ang’ania. Hivyo sio wakuwategemea kwani wanaendelea kutuweka kwenye matatizo.

(2) Vijana wanaoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali serikalini bado haitoshi kuitegemea kama njia ya kutatua kero za vijana, vijana kupewa madaraka ni jambo zuri na njia nzuri pia kuwashirikisha vijana kujenga taifa lao lakini sio yakukaa na kuitegemea kwani vijana wakuteuliwa wakati mwingine huulazimika kufanya kazi yake kwa matakwa ya aliyemteua na sio matakwa ya vijana ilikupata teuzi nyingine.

(3) Serikali inamatatizo mengi ya kutatua ili kuhakikisha nchi inaenda vyema kama vile kufikisha huduma kwajamii, serikali inawaza na kupambana jinsi ya kupata fedha kuendesha miradi yake ndio maana bunifu mbalimbali za upataji kodi zinafanyika. Changamoto za vijana kama kero ya ajira ni sehemu ya matatizo serikali inapambana kuyatatua lakini si busara kuendelea kuitegemea kwani kumtegemea mtu mwenye matatizo akutatulie yakwako inachua muda sana hivyo jambo la busara ni sisi vijana kuisaidia serikali kutatua changamoto hizi.

Ndugu msomaji, kwa sababu hizi tatu na kwa kauli kwamba ni muda wa vijana kuisaidia serikali namaanisha kuwa ni wakati sahihi sasa kwa vijana kuamka na kusema matatizo yao na ya nchi kwa ujumla, kupanga mbinu na mikakati ya kutatua na kisha kupata kibali na Baraka za wasiokua vijana kutatua changamoto hizo. Kwakuwa ninachotaka ni vijana kama nguvu kazi ya taifa washiriki kikamilifu na sio kukaa tu mitaani basi kwamimi napendekeza na kusisitiza UUNDWAJI WA BARAZA LA VIJANA KAMA MSINGI BORA WA USHIRIKISHWAJI WA VIJANA KUFANYA KAZI YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA NCHI NA KUENZI MAZURI YA NCHI.

Ndugu msomaji, BARAZA ni chombo cha majadiliano ambacho hukusudia kukusanya mawazo kutoka kwa washiriki wake juu ya mambo yanayowasibu kisha kukubaliana na kupanga mikakati na kubwa Zaidi washiriki hutoka na SAUTI MOJA yakutatua changamoto zinazowakabili. Yapo mabaraza mengi sana yanayohusisha vijana yakiwemo yale yanayoendeshwa na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali mchango wake kwa taifa ni mzuri lakini bado sauti zao hazisikiki vizuri ndio maana kuna uhitaji mkubwa wa BARAZA LA VIJANA LA TAIFA. Baraza hili litakusanya mawazo ya kila kijana wa taifa letu bila ubaguzi wa kielimu, kikabila, kijinsia au uhitaji maalum kisha kutoa sauti moja inayotambulika kisheria kwamba hii ndio sauti yapamoja ya vijana hivyo kwa nguvu waliyonayo vijana na uzito wa sauti hio hapana budi kutekelezwa. BARAZA HILI LITAKUA NA UMUHIMU UFUATAO:-

(i) Baraza litakua mshauri mzuri kwa serikali hususani katika masuala ya kisera na kisheria, mambo haya yatamuwezesha kijana kupata nafasi ya kujengwa kikamilifu nakutumika kwa maslahi ya taifa kwakua sera na sharia zitagusa kumuinua kijana katika Nyanja zote za kiuchumi kwa maswala kama namna bora ya upatikanaji wa mitaji, uanzishwaji wa biashara na mashirika ya kibiashara ya vijana. Kijamii kwa maswala kama mfumo wa elimu bora kuendana na mahitaji ya soko na kisiasa kwa masuala mazima uongozi na utawala.

(ii) Baraza litajenga vijana wazalendo kwa taifa, serikali kupitia baraza hili itaweza kupitisha mahitaji yake kirahisi kwa vijana na utiifu kwa sharia na mamlaka zilizopo utakua wa hali ya juu kwa vijana katika kuziendea haki zao.

(iii) Baraza litakuwa sehemu sahihi ya kudai haki za vijana endapo itabidi, hii kama zitazuiwa au kunyimwa na baraza litakuwa mtetezi kwa wanyonge.

(iv) Baraza litapiga vita matendo yote yakikatili, haya ni yale yanayoweza kuwadhuru na hata kukatisha ndoto za vijana kama rushwa.
Ndugu msomaji kiujumla kuyaleta mawazo ya vijana pamoja ndio umuhimu mkubwa kwani zitafanyika bunifu nyingi na zenye maslahi sana kwa vijana na taifa. Vilevile niongeze msisitizo katika kazi za baraza la vijana kwa serikali na kwajamii ambapo ni KUISHAURI SERIKALI, KUFANYA UTETEZI, KUBUNI NA KUIBUA MIRADI MBALIMBALI.

Pengine unamaswali unajiuliza vijana wengi wasomi wapo kwenye vyama watawezaje kuendesha baraza bila kuingiza itikadi zao, pengine wakashindwa kuyasemea mambo Fulani Fulani iliwasionekane wabaya kwenye vyama vyao. Je baraza litaundwaje? shughuli zake zitaendeshwaje? Na maswali mengine kama hayo. Nikutoe tu hofu kwamba muswada umeshaandikwa unaoeleza mambo yote haya kilichobaki ni Raisi kuridhia na kuidhinisha kuanzishwa kwa chombo hiki.

Nihitimishe kwakutoa masikitiko kwamba ni Zaidi yamiaka miwili tangu muswada uandaliwe kwanini wasiokua vijana na serikali kwaujumla wanashindwa kuunga mkono agenda hii ya vijana? Je wanapenda kuona nguvukazi ya taifa ikiwa haifanyi kazi? Naombeni mawazo yenu katika hili. Ombi langu kwa vijana ni kwamba tujifunze kuhusu baraza kwa nchi za wenzetu wenye baraza, kisha tulisemee, tulipambanie na kuliunga mkono hili kwani jambo linalopewa uzito na vijana lazima lifanikiwe na kama faida ni kubwa kwanini lisipitishwe ilitupate nafasi ya kupaza sauti moja. Raisi ni msikivu tumuambie.

Naomba kuwasilisha JINA LANGU NI YASINI JUMA. NAOMBA NA KURA YAKO PIA.
 
Back
Top Bottom