Sauti Kubwa: Magufuli anatumia uwanja wa ndege Chato “kupiga dili”?

Tazama,Maxence uko wapi,habari kama hizi za Kishamba kabisa....Hapa hakuna uchunguzi bali ni ushabiki na uwongo

Mwandishi hatuambii mtuhumiwa amekiuka maadili yepi...na ufisadi anaouzungumzia chimbuko lake ni nini?

Watu hawa watasababisha mtandao huu ufungwe,wala usilalamike maana unaruhusu mwenyewe. ....
Usiruhusu madonda kushika kalamu.
hoja ujibiwa kwa hoja si kwa watu wasiojulikana
 
Tatizo la mh anataka kupiga yeye tu kila kitu wakipiga wenzake utasikia pesa ya awamu ya tano hailiwi mtaitapika, wakati yeye anapiga kimya kimya kama hivi akiulizwa anakuwa mkali
 
IMBA NA MIMI: Magufuli akifaa, mimi siwezi kuliaaa

"Nitamtupa Kagera, awe chakula cha Mamba"
 
Gharama za ukimbizi siyo mchezo!
Sasa umeamua kuwa toilet paper ,ngoja utumike!
Ila kumbuka Magufuri ni ccm, jiandae kufia ukouko ugaibuni!
 
IMBA NA MIMI: Magufuli akifaa, mimi siwezi kuliaaa

"Nitamtupa Kagera, awe chakula cha Mamba"
Dah....kama mmefika hadi huku...Pasipo na shaka yoyote ni wazi mmeshikwa pabaya na hamna tena Hoja za maana kwa watanzania....na watanzania tunawaona mjue...
 
Shauri yako mungu anakuona ujue.
Hata akiniona hawezi kunifanya kitu, ndio maana mtumishi wake ibilisi katili Magu anatamani damu yangu kama alivyochukua za kina AZORY, BEN SAANANE, AKWILINI, na wengine lakini Mungu wangu ananipigania na kumuumbua kila leo !
 
RAIS John Magufuli amekamatika. Sababu za yeye kutopenda kukosolewa, na bidii yake kudhibiti wapinzani wake zimeanza kujulikana. Anaogopa wapinzani na vyombo vya habari wasiibue ufisadi wake au wa rafiki zake.

Katika siku za hivi karibuni, mbali na “upotevu” wa Sh. 1.5 trilioni ambazo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) amesema hakuona zilipo, huku serikali ikijitahidi kufunika sakata hili kwa maelezo yasiyoeleweka, na bila mafanikio, kuna wizi mwingine wa kimfumo unaohusisha Rais Magufuli na watu wake wa karibu.

Rais Magufuli anatajwa katika dili la Uwanja wa Ndege wa Chato, ambao ulipangiwa kujengwa kwa Sh. 39 bilioni, lakini hadi sasa umetumia Sh. 42 bilioni, ambazo zimepitishwa bila idhini ya bunge. Wanaojua kinachondelea wanasema fedha hizo nazo “zimepigwa.” Wanachosikitikia ni kwamba rais anajua na anahusika, hata kama mkono wake hauonekani moja kwa moja.

Kampuni iliyopewa zabuni ya kujenga uwanja huo, Mbutu Bridge JV, inasimamiwa na Steven Makigo, mmoja wa maswahiba wakubwa wa Rais Magufuli. Urafiki wa Makigo na Magufuli ulianzia katika Shule ya Sekondari Lake, ya Mwanza, tangu miaka ya sabini. Makigo alisomea pale 1975-1978, wakati Magufuli alisomea pale 1977-78. Makigo ni mhandisi aliyehitimu shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Magufuli ni mwalimu wa kemia, hisabati na elimu, mhitimu wa chuo hicho.

Makigo ndiye anaonekana, katika video fupi ya watu watatu iliyosambaa mitandaoni, akimshauri Magufuli agombee urais; na Magufuli akimjibu, “nikigombea, watalimia meno.” Mtu wa tatu katika video hiyo ni Charles Kitwanga, swahiba mwingine wa Magufuli ambaye ni mbunge wa Misungwi, Mwanza. Makigo ndiye alikuwa mshika fedha za kampeni za urais wa Magufuli mwaka 2015. Taarifa zinasema Makigo na Magufuli wawili hao ndio wamiliki halisi wa kampuni hiyo, ingawa mmoja amemtanguliza mwenzake kwa sababu za kisiasa.

Mbali na kusimamia kampuni ya Mbutu Bridge, Makigo amekuwa mkurugenzi mtendaji wa Mayanga Construction Co. Ltd, iliyosajiliwa mara ya kwanza kama kampuni ya “CIVIL” mwaka mwaka 2007, ikapewa namba ya usajili C1/0056/12/2007; halafu ikasajiliwa tena mwaka 2016 kwa namba ya usajili B1/154/04/2016 ikiwa kampuni aina ya “BUILDING.”

Mwaka 2012 Kampuni ya Mayanga iliungana na kampuni nyingine 12 za wazalendo kuunda Mbutu Bridge Joint Venture kwa ajili ya kutengeneza daraja la Mbutu, Igunga, lenye urefu wa mita 46.1. Ilizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete, Januari 2013. Mradi huo uligharimu Sh.12.34 bilioni. Shabaha ya kuunda kampuni hiyo ilikuwa kuwezesha kampuni za wazawa kupewa zabuni za miradi minono ambayo imekuwa inachukuliwa na wageni, hasa Wachina, kwa sababu ya uwezo mdogo wa kampuni moja moja za kitanzania.

Hata hivyo, kashfa za kampuni hiyo zimeibuka baada ya kampuni kupendelewa na kupewa mradi mnono wa kujenga uwanja wa ndege wa Chato, huku haina sifa wala uzoefu wowote. Katika kuonyesha kuwa serikali ililenga kuipa fedha kampuni hiyo, tangazo la zabuni namba AE-027/2016-2017/CHT/w/07 ya ujenzi wa uwanja huo lilisisitiza kuwa lazima kampuni inayoomba iwe inatoka katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Kagera, na Simiyu.

Wakandarasi wengine walilalamika kuwa sharti hilo lililenga kuwatenda ili kuipa zabuni “kampuni ya rais” ambayo inaendeshwa kwa mgongo wa rafiki yake. Hata hivyo, licha ya kampui hiyo kupewa zabuni hiyo, kampuni yenyewe haijawahi kujenga uwanja wa ndege popote duniani, jambo ambalo limeongeza wasiwasi juu ya vigezo vilivyotumika kuipa zabuni.

Zaidi ya hayo, inatuhumiwa kwa “upiga dili” na kushindwa kazi katika miradi mingine midogo iliyowahi kupewa. Miongoni mwa tuhuma za awali ni zile zioizotajwa na wabunge kadhaa wakiwemo Zitto Kabwe, John Heche na Marwa Chacha Marwa wa Serengeti katika mjadala makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mwaka 2016/2017. Alisema:

“Mheshimiwa Mwenyekiti, …sasa naomba niseme kuhusu barabara ya Makutano – Nata – Mugumu – Loliondo – Mto wa Mbu. Aliyeanza kuwa na maono ya kujenga barabara hii ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wakati huo ikiitwa Makutano – Nata – Ikoma Gate. Mheshimiwa Mwenyekiti, baadaye alipokuja Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ndipo wakaanza kuiweka kwenye Ilani ya CCM. Mkapa akaondoka, katika miaka yake kumi hakujenga barabara hii. Akaja Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ikawekwa kwenye Ilani ya CCM, wakati huo Mheshimiwa John Pombe Magufuli akiwa ndiye Waziri wa Wizara ya Ujenzi. Ikapita miaka kumi wala hakuna chochote kilichofanyika. Sasa amekuja ambaye alikuwa Waziri wa wizara hiyo, Mheshimiwa John Pombe Magufuli.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu sana, barabara hii mwaka 2013 ilitengewa fedha kwenye bajeti ili ianze kujengwa na mwezi wa tatu mwaka 2013 ujenzi wa barabara ukaanza, ambapo wakandarasi wa ndani ndio waliokuwa awarded tender ya kujenga barabara hii. Na bahati nzuri mmoja wa wakandarasi anaitwa Steven Makigo, rafiki yake sana Magufuli, akapewa kazi ya kujenga barabara hii. Yeye na wenzake contractors kumi, tangu mwaka 2013 mwezi wa tatu mpaka leo ninavyoongea wamepewa shilingi bilioni 14 hawajajenga hata mita moja ya lami. (Makofi)

“Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia; waliopewa kujenga barabara hii ya lami, Makutano – Nata – Mto wa Mbu ni contractors wa ndani wakiongozwa na Kampuni ya Mayanga ambayo Mkurugenzi wake ni huyu Steven Makigo, wako contractors kumi. Wakaisajili kwa jina moja wanasema Mbutu Bridge Contractors; ni wa kwetu ni wazawa. Tangu 2013 wamepewa shilingi bilioni 14 hata mita moja ya lami hakuna halafu mnasema hapa kazi tu, hapa kazi kwa issue gani? Kama mmewapa bilioni 14 wameshindwa wanyang‟anyeni, watumbueni majipu wale, anzeni na huyu mkandarasi, yaani hakuna chochote anachofanya lakini mnampa mahela tu.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, siku moja nimeuliza swali hapa Mheshimiwa Waziri hakulijibu na hiyo wamepewa kujenga 50 kilometers kuanzia Makutano mpaka Sanzate. Sasa hivi ninavyoongea mkataba wa kujenga barabara ile uliisha mwaka 2015 mwezi wa tano, baadaye wakaomba extension wakaongezewa mpaka Machi 2016, hivi huu ni mwezi gani? Mpaka leo bado hawajajenga hata mita moja, bado tunaendelea ku-entertain watu wa namna hii, si afadhali mtuwekee pale Mchina ajenge ile barabara ikamilike haraka.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu, kama watu wamepewa shilingi bilioni 14 hata mita moja ya lami hawajajenga halafu unaniambia nisiongee, I have to talk. Nimeletwa hapa kama Mbunge wa Jimbo la Serengeti niongee kwa niaba ya wananchi wa Serengeti. Tunachokiongea hapa si mambo ya chama, hata kama ingelikuwa kwako wewe wametumia shilingi bilioni 14 hawajajenga kilometa moja ya lami utasikia vizuri, au huyo malaika akiguswa mnasikiaje? Tulia. (Makofi)

“Mheshimiwa Mwenyekiti, kampuni yenyewe sasa hivi wanajenga daraja la Mto Kiarano, hata structural engineer hawana, material engineer hayupo! Hivi hii Wizara ikoje hii?

Na kama kweli Rais, Mheshimiwa John Pombe Magufuli anaipenda nchi hii, anawapenda wananchi wa Mkoa wa Mara, anawapenda wananchi wa Serengeti, aanze ku-deal na huyu mkandarasi. Kama mtu anaweza kutumia shilingi bilioni 14 halafu hakuna chochote alichofanya halafu watu wanaona sawa tu eti usimguse nitakugusa tu. (Makofi)”

Heche, mbunge wa Tarime Vijijini, katika ukurasa wake wa Twitter, tarehe 10 Novemba 2017, aliandika:

“Uwanja wa ndege wa Chato unajengwa kwa billion 41 haukua kwenye mpango wala bajeti ya mwaka huu!!Nini faida za kiuchumi kujenga uwanja mkubwa wenye runway ya 3km na upana 43m Chato? Je, uwanja huu ni muhimu kwa taifa kwasasa kiasi hicho? Sheria ya bajeti inavunjwa na serikali!!”

Ukubwa halisi wa uwanja huo, kwa mujibu wa zabuni hiyo, ni urefu wa mita 3000 (km3), na upana wa mita 45.

Zitto naye, tarehe 11, Novemba 2017, alijadili suala hilo katika ukurasa wake wa Twitter, akichangia hoja ya Heche, akaandika:

“Hii ni hoja ya kuundia Kamati Teule ya Bunge kwani ina viashiria vya upendeleo kinyume na Katiba na pia mkandarasi wa uwanja huu, hiki ni kiwanja chake cha kwanza kujenga na ana mahusiano ya karibu sana na Rais. John hebu lishike hili kwa kina.”.

Mbali na “kupiga bilioni 14” na kutokuwa na sifa za ujenzi wa uwanja wa ndege wa zaidi ya Sh. 40 bilioni, kampuni hiyo imeshindwa pia kujenga barabara ya Makutano – Nata (km 50), mkoani Mara. Na taarifa ya CAG ya 2016/17 imeonyesha kuwa kampuni hiyo imelipwa na TANROADS fedha zaidi ya kiwango ilichostahili. Imelipwa Sh. 951,815,664.

Kifua ambacho kampuni hii imekuwa inakingiwa na upendeleo inaopewa katika mazingira haya ya kifisadi, huku Rais Magufuli akijitutumua kukema na “kutumbua” wengine anaoita mafisadi, huku akikingia kifua kampuni inayochota hela kijanja janja na kushindwa kutiiza kazi inazopewa, ni baadhi ya masuala yanayomomonyoa uadilifu wa rais katika vita dhidi ya mafisadi.

Baadhi ya watu waliofanya naye kazi kwa karibu akiwa waziri na sasa akiwa rais, wanasema kuwa hatua nyingi anazochukua rais kuadhibu watu anaowataja kama mafisadi, zinawalenga watu ambao ama aliwahi kukosana nao huko nyuma au ana maslahi ambayo anataka kulinda, na anahisi kuwa wasipoondoka katika nyadhifa zao hawatamlinda.

Katika hali isiyo ya kaiwada, hata CAG katika ripoti ya mwaka 2016/2017 hakuonyesha upungufu wa fedha za uwanja wa ndege Chato ambazo kisheria zimechotwa na kupelekwa nyumbani kwa rais bila idhini ya Bunge. Alipoulizwa kwanini hajazikagua alisukumia wabunge mzigo huo akisema ndio wanapaswa kuhoji kwanini fedha hizo zimetukika bila idhini yao.

Hata hivyo, wabunge walishtuka muda mrefu, na wamekuwa anahoji kwa nyakati mbalimbali, hata wengine kufananisha mradi huo na ufisadi wa dikteta Mobutu Seseseko wa Zaire aliyechota fedha za umma na kujenga uwanja wa ndege kijijini kwake Gbadolite. Uwanja huo ulitumika hadi alipoondolewa maradakani, akakimbilia na kufia uhamishoni Morocco mwaka 1997. Sasa hivi umegeuka pori.

Baadhi ya wachambuzi wanasema ufisadi huu wa Chato ni moja ya sababu zinazomfanya Rais Magufuli kutisha wakosoaji na wapinzani, na kufungia vyombo vya habari vya uchunguzi.

Chanzo: Sauti Kubwa

Hakuna hoja hapa....
 
Anzia nyumbani kwenu hapo unyumbuni, bilioni 7 zilipigwa na mbowe
Siyo nyumbani kwangu kwasababu siko kwenye siasa. Wengine tunasikia tu mnavyotafuna nchi na wengine wanaona. Kuna wenye uelewa kiduchu sana ambao mnatumika tu kama tissues. Adui wetu mkubwa kwa Taifa ni ujinga wenu. At the same token, huo ujinga ndo mtaji wa watawala ambao nao wajanja katika wajinga. Maana wenye akili hawawezi kufanya mnayofanya, na ambayo mmekuwa mkifanya ever since we gained our independence from Britain.

Bado ninaamini hatujawahi kupata viongozi wa kweli. Wengi wenu ni vilaza tu na walafi sana. Endelezeni ujinga wenu tu maana ndo mmezoea.
[HASHTAG]#hovyokabisa[/HASHTAG]
 
Mnaotumiwa ba mabwanyenye mmeshikwa pabaya awamu hii. Mnaleta habari za kufikirika zisizo na ushahidi halisi. Vumilieni tu kasindano kaingie wajameni

We kwa akili zako unaona sawa kujengwa kwa uwanja wa ndege wenye hadhi ya kimataifa kijijini Chato.. Atautumia nani?
 
duh mbona majuzi tu nilimsikia mwenyewe anaelezea historia yake alipotembelea pale mkwawa university kwamba 1977_1978 alisoma pale A'level we unatwambia alisoma Lake sec i smell fishy here
 
Dah....kama mmefika hadi huku...Pasipo na shaka yoyote ni wazi mmeshikwa pabaya na hamna tena Hoja za maana kwa watanzania....na watanzania tunawaona mjue...
Ni kweli KUPIGWA 2.6 Trillion si mchezo plus kupigwa risasi 38 mchana wa jua kali
 
Back
Top Bottom