VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Hatimaye kada wa CCM aliyetimkia huko baada ya kuwa CHADEMA Makao Makuu, Saumu Malungu ameomba ulinzi CCM. Hii inafuatia kutajwa kwake na Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA,Wakili Msomi Tundu Lissu kuwa ndiye anayeratibu mipango ya kupika ushahidi na kuandaa ushahidi dhidi ya Winfred Lwakatare.
Ni leo tu ambapo Saumu aliripotiwa na gazeti la Tanzania Daima kuwa alinaswa akiwasiliana na kiongozi mwandamizi wa CCM ambaye ni mratibu wa mpango wa Lwakatare kichama. Saumu anatumiwa kwakuwa alikuwa Idara ya Usalama ya CHADEMA na kwakuwa anajua kila linaloendelea CHADEMA Makao Makuu.
Mnamo majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni hii, Saumu alifika hapa Ofisi Ndogo za CCM Lumumba ili kuwasilisha ombi lake la kuomba ulinzi na haraka akakabidhiwa kwetu kama Kitengo cha Ulinzi cha CCM. Niko hatarini. Inadaiwa kuwa nimeshtukiwa. Kuna wenzangu wamenisaliti ndani ya CHADEMA. Wamevujisha siri za mipango yetu alisema Saumu akionekana kuwa na shaka kuu.
Nilindwe. Mwigulu Nchemba kwasasa hanipi msaada wa kutosha. Nilianzia UVCCM pale ambapo wamenielekeza nije hapa. Tafadhali nilindwe ilinimalizie kazi yangu aliongeza Saumu Mulungu.
Baadhi ya vigogo hapa Lumumba wameonesha hofu kuu katika kuharibiu taswira ya chama juu ya suala hili. Wameapa kuwatenga wote wanaohusika na mpango huu haramu,kama kweli upo. Kuna sintofahamu kubwa hapa Lumumba.
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.