Saudia inaitaka Ujerumani kuendelea kuwauzia silaha

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Saudia yaitaka Ujerumani iendelee kurundika silaha nchini humo

Feb 18, 2020 08:08 UTC

[https://media]

Utawala wa Aal-Saud ambao unaendelea kumwaga damu za Wayemen umeiomba Ujerumani iondoe katazo la kutuma silaha nchini Saudi Arabia.

Katika mahojiano na shirika la habari la Ujerumani la DPA jana Jumatatu, Faisal bin Farhan Aal Saud, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia alidai utawala wa Riyadh unahitaji silaha hizo kwa ajili ya kujilinda.

Bin Farhan ameashiria kuhusu mashambulizi ya mwaka jana ya harakati ya Ansarullah ya Yemen dhidi ya vituo viwili vikubwa vya mafuta nchini Saudia na kudai kuwa, "Natumai Ujerumani inafahamu umuhimu wa silaha hizo kwa ajili ya kulilinda taifa letu."

Ombi la Saudia kwa Ujerumani linakuja wiki sita kabla ya Ujerumani kutafakari iwapo itarefusha muda wa kusitisha mauzo ya silaha kwa Saudia na karibu waitifaki wenzake wote wanaoshiriki katika jinai dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Yemen au la.

[https://media]Marekani na nchi za Ulaya zinaendelea kurundika silaha Saudia licha ya mauaji ya Wayamen

Marufuku ya Ujerumani ya kuizuia silaha Saudia inatazamiwa kumalizika Machi 31 mwaka huu. Ujerumani ilisitisha mauzo ya silaha zake kwa watawala wa Riyadh mwishoni mwa mwaka 2018, kufuatia mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji wa utawala wa Aal- Saud ndani ya ubalozi wa Saudia nchini Uturuki.

Ukoo wa Aal Saud na wavamizi wenzake wa Yemen wanatumia silaha za nchi za Magharibi kufanya jinai za kuchupa mipaka dhidi ya Waislamu wa Yemen.

4bprd19d8942a1181xm_800C450.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah wapumbavu.. kuwa imara kijeshi kunategemea Sana kutengeneza silaha zako za ndani zenye uwezo mkubwa wa uharibifu ..
Ukinunua makombora kutoka ujerumani, ufaransa, na marekani ni Sawa na kujiweka uchi kwa mbwa mwitu wenye njaa.. mwisho wa siku ukiwa against hawawazi coz takwimu wanazo wanskutegea ukimaliza wsnajua.
Huyo waziri anatia aibu kulilia silaha kutoka west..
Wajifunze kutengeneza..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saud Arabia wanazalisha silaha. Ila ukizingatia Saud is the 3rd biggest spender on military in the world, they can't produce much themselves inabidi waagize.

Hiyo inawafanya wawe Germany's 2nd-best weapons customer. Kuna swali lingine Proved?
Mi nafikiri si kwa sababu production inazidiwa na mahitaji lakini ni akili zilizobana.. vichwa vikubwa na bongo lala..
Mwaka juzi nilishangaa eti ndege zao ziliiacha kushambulia kisa makombora ya air to ground yamekwisha.. aibu..
Inabidi wajifunze hata kukopi basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah wapumbavu.. kuwa imara kijeshi kunategemea Sana kutengeneza silaha zako za ndani zenye uwezo mkubwa wa uharibifu ..
Ukinunua makombora kutoka ujerumani, ufaransa, na marekani ni Sawa na kujiweka uchi kwa mbwa mwitu wenye njaa.. mwisho wa siku ukiwa against hawawazi coz takwimu wanazo wanskutegea ukimaliza wsnajua.
Huyo waziri anatia aibu kulilia silaha kutoka west..
Wajifunze kutengeneza..

Sent using Jamii Forums mobile app
Sema ni vile kuna uaminifu kwenye kuuziana silaha, kwa sababu nchi inayouza ikiuza feki inachafuliwa sifa na faini za kutosha.

Ingekuwa sio hivo unawauzia baadhi ya batches zilizo fail au hazifanyi kazi. Watunguliwe mpaka akili ziwakae sawa.
 
Watuige sisi na silaha zetu kutoka kiwanda cha Silaha Mzinga, Moro
Dah wapumbavu.. kuwa imara kijeshi kunategemea Sana kutengeneza silaha zako za ndani zenye uwezo mkubwa wa uharibifu ..
Ukinunua makombora kutoka ujerumani, ufaransa, na marekani ni Sawa na kujiweka uchi kwa mbwa mwitu wenye njaa.. mwisho wa siku ukiwa against hawawazi coz takwimu wanazo wanskutegea ukimaliza wsnajua.
Huyo waziri anatia aibu kulilia silaha kutoka west..
Wajifunze kutengeneza..

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nafikiri si kwa sababu production inazidiwa na mahitaji lakini ni akili zilizobana.. vichwa vikubwa na bongo lala..
Mwaka juzi nilishangaa eti ndege zao ziliiacha kushambulia kisa makombora ya air to ground yamekwisha.. aibu..
Inabidi wajifunze hata kukopi basi

Sent using Jamii Forums mobile app

Hawa si huwa wananunua silaha zaidi ya wanazozihitaji. Yaani wanakuwa na stocks za kutosha. Hii ya mwaka juzi ilikuwaje?
 
Wasaudi wazembe katika kusoma wakilinganisha na Qatar, U.A.E na matajiri wenzao. Tuachane na Wairan ambao wako mbali sana kielimu kuliko hawa.
Yawezekana lakini
Wanachojua ni kununua silaha za kisasa na kuziuza au kuzigawa kwenye vikundi vya kigaidi.
 
Ndo hiyohiyo pesa inatumika kununua silaha zilizotengenezwa na sayansi. Alafu nchi gani iko tiyari kukuuzia kila teknolojia ya maana ya kutengeneza silaha. Marekani ambao ndo washirika wakubwa wa Saudi hawataki hivo.
True Marekani anamuuzia silaha ambazo ana "uhakika " kabisa kwamba hatakaa aweze kutengeneza/kuzalisha wenyewe hata apewe miaka 100, licha ya kumuuzia teknolojia.

Ila nao Saud wana minimal domestic military production.
 
Nchi zote wauzaji wa silaha wanakuwa na mkataba wa kuzuia reverse engineering ya silaha hizo. Na mikataba inahusu package nzima ya marekebisho, modernization na spare parts. Na mpaka training uhusika inategemeana na package ya mkataba. China alireverse Su-35 fighter jet za Urusi na kutengeneza J-15 zake wakakosana baadae Urusi akakataa kumuuzia modern jet nyingine. Hawa ni marafiki wakubwa, sembuse Marekani na Saudi Arabia.
 
Yawezekana lakini
Wanachojua ni kununua silaha za kisasa na kuziuza au kuzigawa kwenye vikundi vya kigaidi.
Silaha nyingi zinazopatikana Middle East sio direct from the source. Wanakwepa kukamatwa na kuonekana nani katengeneza kama ilivotokea kwa silaha za Iran kwenda kwa Houthi wiki jana.
Mfano wanachofanya U.S na hawa Saudi Arabia wananunua silaha kutoka iliyokuwa Yugoslavia maana kule kuna lundo la silaha. Sera za nchi hiyo ilikuwa ni kuamini muda wowote USSR atawavamia hivo wakawa wana maghala makubwa sana ya silaha kila kona ya nchi kwamba nchi ikivamia silaha zote zinafunguliwa kila mwanaume anayejua kutembea anaingia uwanja wa mapambano. Ndo maana NATO ilipata taabu sana ilipoingia nao vitani hasa upande wa Serbia.
Kule Libya vilevile kuna silaha zinazunguka kutoka uku kwenda uku. Zikikamatwa silaha na jeshi la Syria utaambiwa na mainstream media kuwa magaidi waliimport kutoka Libya.
 
Back
Top Bottom