Nimesoma article yako mkuu kuhusu vazi la taifa kuna mantiki ndani yake
Kwanza kabisa shukurani kwa kuona mantiki. Mara nyingine habari inaweza kuwa na kina kinachozamisha wengine kiasi cha kukosa hewa na uelewa.
Haya ya Saudi kwa kiasi fulani, ukifikiri kwa kina, ndiyo hayo hayo ya kuweka kamati kwa wananchi kuhusu vazi la taifa. Ruhusu majina yote, wazazi wajinga wawape watoto wao majina ya kijinga. Tujue hawa wazazi wajinga, hawa wakatoliki, hawa wanspenda Segere Matata, hawa wanajeshi, hawa Waingereza weusi. I Ruhusu hata kubadilisha majina kuwe rahisi, kama mtu hapendi jina lake abadilishe tu.
Mfalme anaogopa mtoto akiitwa "Mfalme" anaweza kuwa mfalme kweli? Mfalme yuko so insecure asingeweza kym face Mzee Kawawa kwenye rabsha za trade union, after all Mzee Rashid middle name yake "Mfaume"!
Hiyo habari nimeandika January 2012, leo March 2014. Hatujafikia tamati ya hii kamati bado. Na watu washaisahau.
Katika somo la uongozi, umangimeza unavyojitanda, hususan ukifuatilia Parkinson's Law, utaona kazi itaweza kumalizika katika muda wowote mrefu zaidi iliyopangiwa kumalizika.
Kama tume hizi hazijapangiwa muda wa kumaliza kazi, hilo linaweza kumaanisha kazi haimaliziki, au inaweza kumalizika kwa kuchelewa sana kiasi tamati yake isiwe na maana tena.
Kumetokea mengine, tume na kamati nyingine zimeundwa, zitasahauliwa hivyo hivyo.
Mpaka hapo yatakapotokea mengine na kui choke serikali nzima kwa kamati ziso tamati wala hati yenye chati ya dhati, Tandahimba mpaka Babati.
Talk about a short attention span and penchant for pretentious politics purely perpetrating power pushes for people's propositions.