Satelite ya nasa itaanguka muda wowote

Mr.Toyo

JF-Expert Member
Feb 9, 2007
433
117Setalaiti 'chakavu' yenye ukubwa unaolingana na basi la abiria inatarajiwa kuanguka duniani kutoka angani muda wowote hivi sasa.Awali setalaiti hiyo ya Shirika la Mambo na Anga la Marekani (NASA) ilitarajiwa kuanguka duniani usiku huu (kwa saa za hapa Uingereza ambazo ni masaa mawili mbele huko nyumbani Tanzania) lakini inaelekea itachelewa kutokana na kasi mwendo wake kupungua.


Inaonekana kuwa vumbi linalotoka kwenye setalaiti hiyo linatarajia kuangukia Amerika ya Kaskazini japokuwa bado uwezekano huo ni mdogo.Setalaiti hiyo 'chakavu' ina uzito wa zaidi ya nusu tani (tani moja ni kilo 1000).Awali NASA walieleza kuwa setalaiti hiyo isingeweza kuangukia Amerika ya Kaskazini lakini taarifa zilizopatikana baadaye zimeonyesha kuwa hadi sasa haifahamiki chombo hicho kitaangukia sehemu gani duniani.


"Kuingia (kwa chombo hicho) duniani kunatarajiwa kutokea Ijumaa ya tarehe 23 Septemba (jana kwa saa za hapa), au mapema Jumamosi tarehe 24,mchana kwa saa za Mashariki ya Marekani (masaa matano mbele kwa saa za hapa au masaa saba mbele kwa saa za huko nyumbani)" ilieleza taarifa ya NASA.


NASA inatarajia vipande 26 vya chombo hicho,vyenye jumla ya kilo 532 vitabaki vimefungamana na kuanguka duniani.Vipande vidogo vidogo vya chombo hicho vinatarajiwa kusambaa kwa umbali wa maili 500 katika uso wa dunia.Kutegemea ukubwa wake,vipande hivyo vinatajiwa kuanguka duniani kwa kasi ya kati ya maili 55 (kilometa 90) kwa saa na maili 240 (kilometa 385) kwa saa.


Vituo vya rada sehemu mbalimbali duniani vinafuatilia safari ya chombo hicho lakini kuna uwezekano mdogo wa kutabiri vipande vipande vyake vitaangukia wapi.Matarajio ya wanaanga ni kuona vipande vipande vya chombo hicho vikiangukia baharini (na hivyo kuepusha madhara yoyote kwa wanadamu na mali zao).


Habari njema ni kwamba uwezekano wa vipande vipande vya chombo hicho kukuangukia ni takriban 1 kwa trilioni 20 (1:20,000,000,000,000)


NASA wanashauri mtu yeyote atakayeona vipande kutoka katika chombo hicho kutovigusa bali awasiliane na mamlaka husika (polisi kwa Marekani).Kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa,kila kipande kitakachoanguka popote pale kinapaswa kurekjeshwa kwa mmiliki wake,yaani NASA.


Sasa kwa wale wanaofanya biashara za chuma chakavu wakiona vipande hivyo na kuvifanya dili watakuwa wanajitafutia kesi za bure na NASA na Wamarekani kwa ujumla.Well,hiyo ni changamsha-baraza,lakini ni matumaini yetu sote kuwa kuanguka kwa setalaiti hiyo hakutakuwa na madhara yeyote kwa wanadamu popote pale walipo.


Habari hii imetafsiriwa kwa ufupi kutoka gazeti la Guardian la hapa Uingereza
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,666
2,179
Mpaka kinaanguka ni kwamba wameshindwa kukicontrol au ndo utaratibu kikichakaa kinaanguka chenyewe?
 

WIZARD

Member
Sep 18, 2011
72
9
Mbona kile cha mwanzo walikidungua kabla hakija leta madhara, ina maana hiki wameshindwa. Natamani kidondokee hapohapo NASA senta.
 

Glue

Senior Member
Jan 14, 2011
156
49
Sasa hao wamarekani wanaojifanya wanajua kila kitu, wameshindwa kuzuia hyo satelite isianguke na wakaitoa juu kwa juu ili isilete madhara!
 

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,448
8,283
Labda ilishakatika vipande zamani wanazuga wamekuta ilisha anza safari ya kurudi wakawa hawana lakufanya.
 

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
23,436
44,990
waanze kutembea wanaangalia juu.hiyo lazima iondoke na uhai wa watu.huko baharini hakuna wavuvi,meli?
 

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,895
3,393
natamani idondokee juu ya nyumba yangu wamarekani waje kunijengea nyingine
 

vivian

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,749
998
kwa wale wanaujua mahesabu watakubaliana na mimi hii habari ni kwaajili ya kuchangamsha jukwaaa.

Probability of hapening 1:20,000,000,000,000.

Hivi ukaambiwa Probality yako ya Kupata kazi ndio hiyo utakaa chini uanze Kusherekea? Au ukiambiwa probality yako ya kufa leo ndio hiyo utakaa chini uanze kulia?

No way.
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
49,307
69,595
Si itakua dili sana kwa sisi tunaofanya biashara ya chuma chakavu, ngoja nikivizie mwanangu
 

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,901
3,091
Mimi nikipata kipande chochote siwapi ng'o. Nitahifadhi nije kuwadanganya wajukuu wangu kuwa nilikuwa astronaunt...
 

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
13,377
13,109
osama kama angekuwa na akili hii biashara ya kulipua satellite zote angani ndio ingempa heshima zaidi, maana tungeweza kurudi zama za stone age!
 

Nzowa Godat

JF-Expert Member
Jun 15, 2011
2,762
796
kwa wale wanaujua mahesabu watakubaliana na mimi hii habari ni kwaajili ya kuchangamsha jukwaaa.

Probability of hapening 1:20,000,000,000,000.

Hivi ukaambiwa Probality yako ya Kupata kazi ndio hiyo utakaa chini uanze Kusherekea? Au ukiambiwa probality yako ya kufa leo ndio hiyo utakaa chini uanze kulia?

No way.

You are so intelligent teaching aids user.
 

Mr.Professional

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,582
258
kwa wale wanaujua mahesabu watakubaliana na mimi hii habari ni kwaajili ya kuchangamsha jukwaaa.

Probability of hapening 1:20,000,000,000,000.

Hivi ukaambiwa Probality yako ya Kupata kazi ndio hiyo utakaa chini uanze Kusherekea? Au ukiambiwa probality yako ya kufa leo ndio hiyo utakaa chini uanze kulia?

No way.

Hyo ni probability ya vipande kumwangukia mtu sio probabillity ya yenyewe kuanguka kama nitakuwa sahihi ktk usomaji wangu otherwise dada vivian rudia habari mwanzo mwisho ndo unaweza kuicriticise vizuri. Ama ndo zile za wabongo kuzoea kubisha hata kwenye ukweli coz tunabisha hata wikileaks wanapotoa siri zetu tunasema huwa ni uongo
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom