Sasatel Iko Katika Hati Hati Ya Kufungwa...

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,605
6,080
Kampuni ya mawasiliano ya Sasatel iko katika hati hati ya kufungwa baada ya kushindwa kufanya vizuri katika soko la mawasiliano hapa Tanzania ikiwemo kushindwa kujitanua kwenda mikoa mingine huu ukiwa ni mwaka wa 3 sasa ila bado wako Dar es Salaam tu.

Kwa sasa ofisi zao zilizokuwa Uganda tayari zimeishafungwa kwa hapa Tanzania alikuwa anatafutwa mnunuzi bahati nzuri ikawa imejitokeza kampuni ya RAHA.COM ambayo ilitaka kuinunua Sasatel ila kiasi cha pesa walichokuwa nacho ni kidogo kwahiyo ikashindikana kufikiana makubaliano, kama hali itaendelea kuwa kama ilivyo sasa basi miezi michache ijayo wanaweza kusitisha operation hapa Tanzania pia..
 
We baba we, loh!

Mbona usiseme juzi wajamini, mwenzio ndio kwanza nimetoka kujitutumua kununua mo-demu yao juzi kati hapa? Lah, sijui inachakachulika
 
Prof Chitamu, mambo yamekuwaje tena?
Pro Chitamu sidhani kama anaweza kusaidia lolote kwa hali ilivyo sasa hivi nafikiri the only option iliyobaki ni kuiuza kama wanavyotaka kufanya, investor pia hawezi kuendelea kutoa hela kama kampuni haileti faida yoyote ile huu mwaka wa 3 sasa kampuni haija-expand kwenda mkoa wowote ule, ikumbukwe management ilikuwa ni ya wa Norway kabla ya kubadilishwa na kuwekwa wa South Africa
 
Kampuni ya mawasiliano ya Sasatel iko katika hati hati ya kufungwa baada ya kushindwa kufanya vizuri katika soko la mawasiliano hapa Tanzania ikiwemo kushindwa kujitanua kwenda mikoa mingine huu ukiwa ni mwaka wa 3 sasa ila bado wako Dar es Salaam tu.

Kwa sasa ofisi zao zilizokuwa Uganda tayari zimeishafungwa kwa hapa Tanzania alikuwa anatafutwa mnunuzi bahati nzuri ikawa imejitokeza kampuni ya RAHA.COM ambayo ilitaka kuinunua Sasatel ila kiasi cha pesa walichokuwa nacho ni kidogo kwahiyo ikashindikana kufikiana makubaliano, kama hali itaendelea kuwa kama ilivyo sasa basi miezi michache ijayo wanaweza kusitisha operation hapa Tanzania pia..

Wanaiuza bei gani Arif?....nataka niinunue iwe JAMBOTELL au JAMIITEL.
 
Wanaiuza bei gani Arif?....nataka niinunue iwe JAMBOTELL au JAMIITEL.
Mkuu sijajua kiasi gani lakini nafikiri mara nyingi kwenye ununuzi huwa wanaangalia value ya kampuni husika kwa wakati huo iko vipi na pia kwenye soko kama inafanya vizuri au lah..
 
Uwiii ki modem cha sasatel nimeklipia pesa kibao, Uwiii wataifunga lini, washushe gharama, pili watoe laini bureee ili watu wengi wasubscribe tatu walete michezo ya pesa ka ku motivate watu katika kampuni yao.
 
Sisi wachambuzi wa masuala ya biashara ya tekinolojia tulijua ni kampuni ambayo imeanzishwa ili ife na siyo kugrow.

Kwanza Sasatel kama new interant kwenye soko hawakua na competative advantage yoyote dhidi ya mahasimu wao. Pia techology waliyokuwa nayo ya cdma siyo flexible enough as compared to GSM.

Walikuja na pipe business bila ku focus on value adding services.

Chitamu is a tech guy, na hakuweza kusaidia kampuni kukua kibiashara. You need to be a biz guy to be able to focus and manupulate the market.

Hata hivyo wamejitahidi. Miaka 3 without making profit siyo mchezo. Hawakusoma alama za nyakati kama wenzao wa Benson online.
 
Back
Top Bottom