Sasa wezi wa mabwana kukiona

Sasa wezi wa mabwana kukiona

ameline

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
2,292
Reaction score
1,152
Jamani wezi wa mabwana za watu mmesababisha kuwepo vikundi kama hivi.

Kwa Arusha sijasikia wala kuona labda mikoani.

TANGAZO TANGAZO TANGAZO
LAURAPETTIE a.k.a LP MSUTORING THEATRE GROUP

Hiki ni kikundi cha kukodi kwa ajili ya shughuli za msuto. Tuko akina dada watano tu na tuna vifaa stahiki hakiki kwa ajili ya shughuli zetu za msuto. Tunapatikana kuanzia asubuhi saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni. Usafiri wa kutufikisha alipo msutwaji ni juu yetu. Tunachaji kulingana na aina ya usutaji na vifaa unavyotaka vitumike. Bei zetu ni nafuu!!

Laura Msutoring inakuondolea hali ya kununa, hali ya kuishi na visasi au stress za kufikia kujiua kwa maneno ya umbeya au kuibiwa mpenzi wako na mtu wako wa karibu....hali ya kuandika mafumbo kwenye status za whatsapp au mitandaoni humu...why mafumbo...tupe kazi tumalize!!.... Tupo kukupa raha mjini, tupo kukusaidia kufikisha ujumbe, tupo kukukomeshea wanafiki, tupo kukuondolea kero za umbeya.

1. MSUTO WA JIKO LA MKAA…msuto huu unajumuisha sare ya khanga yenye maneno stahiki… jiko la mkaa la kumbebesha kichwani mtuhumiwa…. Majivu ya kuchovywa wakati wa kumtia masingi mtuhumiwa pamoja na kumsomea mashtaka yake huku akiweka mtu kati.. ukitaka tumsute kwa maneno hadi azimie ni wewe tu na hela yako… msuto huu ni TSHs. 650,000/= tu

2. MSUTO WA KEKI…. Msuto huu unaambatana na sare ya dera… bendi ya tarumbeta… na MC wa kuutangazia umma mita mia kabla ya kumfikia mtuhumiwa… Msuto huu unakuja na ofa ya kumsuta mtuhumiwa staili ya kucheza ngoma ya mganda…Msuto huu ni TSHs. 550,000/= tu

3. MSUTO WA BARUA/SHAIRI… msuto huu unafanywa kwa mic na spika…. Mtuhumiwa anasomewa barua yenye maneno ya msuto kwa mtindo wa kuimbiwa shairi au barua mbele ya kadamnasi pale alipo… atapewa vipande vyake barabara… huku spika zikiunguruma!!... bei ni TSHs. 400,000/= tu

4. MSUTO WA KILUGHA mixer mixer…. Hapa tunavaa suti za rangi moja… msuto huu unawafaa wadada au wakaka wanaojiona matawi…. Msuto hujumuisha mchanganyo wa lugha kiingereza, lugha mama yake iwe kihehe kigogo kikwere, etc , kizungu chochote ikiwemo kifaransa… utakavyoamua wewe… Msuto huu huambatana na muziki wa minaj au Beyonce… vyovyote utakavyochagua…. beo ni TSHs 700,000/= tu.

TUNA AINA NYINGI ZA MISUTO wasiliana nasi tukupe catalog la misuto!!…. Tunasuta kulingana na haiba ya msutwaji… jinsia ya msutwaji...eneo la msutwaji… historia ya msutwaji…kosa la msutwaji… tunasuta jumatatu mpaka ijumaa…wikendi tuna mapumziko. Tunasuta kwa masaa tatu mfululizo! Na nusu saa ya ziada kama ofa... Hatupigi mtu ila tunavyosuta ni sawa na kumtandika ngumi 60 za uso hahahahahahaaa.

MOTTO WETU: STRESS ZA UMBEYA MWISHO MPAKAN, HUKU TUNASUTA TU!! Wa MIKOANI tunapokea oda wiki moja kabla ya shughuli.
 
Mh! Hii kali.Nnavohitaji hela hivi alafu nimpe mtu kwa kazi ya kunisutia flani.
 
Dunia ina mengi, wazungu wavumbua technologies waswahili misuto haya kazaneni mvumbue pia ant-misutoring.
 
Weka namba ya simu na anwani ya ofisi ikiwezekana na gharama ya bima ili niweze kukata msije mkamtoa raha kipoza roho wangu?
 
u made my day
nimependa huo msuto wanaovaa suti tehe tehe tehe tehe tehe tehe
msuto tu ni sawa kapigwa ngumi ngapi?uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii mbavu zangu
 
Kufa kufaana mabwana wasipoibiwa wangepata wapi hiyo ajira?
 
kazi ipo,nitawakodi mje mumsute bosi wangu ili aniongeze mshahara,malipo ni baada ya mshahara kuongezwa
 
Mmhh kazi ipo... Misuto, wazaramo nini sababu nasikia wanasuta hadi unazimia

Dunia ina mengi, wazungu wavumbua technologies waswahili misuto haya kazaneni mvumbue pia ant-misutoring.
 
Back
Top Bottom