Sasa vijana wa CCM na CHADEMA watalazikika kuhamisha magoli!

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,996
2,000
Mods nawaomba huu uzi msiunganishe.

Kabla ya 2015 tulikuwa tukisikia chadema wakimwita Lowasa ni fisadi na wale wa ccm wakisema siyo fisadi.

Baada ya Lowasa kuhamia chadema, ccm wakanza kusema chadema imepokea mafisadi, huku chadema wakisema mwenye ushahidi alete au apeleke mahakamani

Leo Lowasa karudi ccm, atapokea matusi ya kila aina kutoka chadema huku ccm wakisema ni mtu safi.

Inakera sana kuwa na siasa za aina hii!

Wa kuwaonea huruma ni chadema maana wao huwa ni fungu la kukosa.
Sasa itawabidi waanze kumshangilia Lisu, kwa ajili ya urais 2020, mtu ambae hata mizizi yeyote zaidi ya kubebwa na ubwatukaji. Chadema inaenda kulingana na mdundo wa umaarufu wa mtu mmoja katika chama.

Upinzani Tanzania bado sana! Siyo kwamba watu hawajaichoka ccm, lkn wataitoa wamweke nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,022
2,000
Sema sababu Ccm ni Mali ya MTU binafsi ingekuwa ya wana chama wangempa lowasa 2020 ataungwa mkono na nusu ya ukawa japo wabunge watawachagua wa upinzani Lkn kwa nafasi ya uraisi watampa Lowasa.
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,332
2,000
Sina chama lakini kuna mambo yananishangaza kuhusiana na CCM na Chadema. Kwa CCM Lowassa alikuwa mmoja wa mafisadi na akalazimika kujiuzulu. Kisha akajiondoa CCM na kuhamia Chadema. Akatukanwa sana wakati wa kampeni na akawa mmoja wa watu wa kwanza waliosemwa kushughulikiwa na mahakama maalumu ya ufisadi.

Kwa Chadema alikuwa mtaji coz alipata kura 6m, kukawa na idadi ya wabunge na madiwani kubwa kuliko kipindi chochote kile.

Sasa amerejea CCM - sijui atakoma kuitwa fisadi au Chadema watamuita liability kama Dr. Slaa alivokwisha sema na kujiondoa katika uongozi (sijui kama ni mwanachama wa Chadema).

Ninaanza kupata picha halisi - siasa ni sehemu mtu huangalia maslahi binafsi ya wakati huo zaidi. Ndio maana watu wenye maslahi ya umma ktk siasa ni wachache sana; Muamar Ghaddafi, Patrice Lumumba, Kwameh Krumah, Amr Saadat, Nelson Mandela, Julius Nyerere - walikuwa unselfish!!!
 

TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,022
2,000
Lowasa kamkimbia Lissu upepo si wake heri arudi ccm kuokoa chama kisife 2020.
 

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
952
1,000
Sema sababu Ccm ni Mali ya MTU binafsi ingekuwa ya wana chama wangempa lowasa 2020 ataungwa mkono na nusu ya ukawa japo wabunge watawachagua wa upinzani Lkn kwa nafasi ya uraisi watampa Lowasa.
Sema sababu Ccm ni Mali ya MTU binafsi ingekuwa ya wana chama wangempa lowasa 2020 ataungwa mkono na nusu ya ukawa japo wabunge watawachagua wa upinzani Lkn kwa nafasi ya uraisi watampa Lowasa.
haya maneno umeamua kuongea kinyume makusudi ili usifutwe uanachama?
 

Trillion

JF-Expert Member
Apr 24, 2018
1,330
2,000
Lowasa, Magufuli na "upotevu" wa trillion zetu ndio CCM hiyo.., chama cha MAFISADI PAPA .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom