Sasa huyo Lowasa angekuwa 'visionary' kama unavyomuita wewe, asingefanya ufisadi na kuitumbukiza nchi kwenye mkenge wa Richmond na Dowans.
Au labda katika hilo swala la Richmond na Dowans, alikuwa bado hajawa 'visionary'??
Machafuko yanayotokea sasa sio matokeo ya vijana kukosa kazi, ila ni matokeo ya Kikwete kupandikiza udini na kuupalilia.
Hebu angalia, maandamano na vurugu hizi zinazoendelea sasa, zinafanywa na vijana wanaodai ajira ??
Vurugu hizi zilipangwa rasmi kabisa ili zitokee, na kwa bahati mbaya sana zikapata kisingizio cha 'mtoto kukojolea quran'.
Vurugu hizi ni za kidini, na sio za kiuchumi. Watu kuchoma makanisa sio vurugu za kiuchumi.
Au wewe na Lowasa mnadhani kuwa watu wakichoma makanisa ni ishara ya kukosa ajira ??
Au wewe ukikosa ajira utaenda kuchoma kanisa ??
Ushauri kwako na kwa Lowasa ni huu:-
- Acheni ufisadi ili nchi ineemeke kwa utajiri iliyonao, na hakutakuwa na ukosefu wa ajira.
- Mshaurini mwenzenu Kikwete akemee na kuchkua hatua za kukomesha udini hapa Tanzania, badala ya kukimbilia Oman wakati nchi yake inaingia kwenye machafuko ya kidini.