Sasa Tucta yataka Sh750,000 kima cha chini

Sasa Tucta yataka Sh750,000 kima cha chini

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Mbeya.

kazi.jpg

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Mkoani Mbeya, limetangaza kiwango kipya cha mishahara inayotakiwa kuwa kima cha chini ni Sh 750,000.

Mwenyekiti wa Tucta mkoani hapa, Alinanuswe Mwakapala alisema kwa maisha ya sasa kima cha chini lazima kiwe Sh750,000 na kwamba, pendekezo hilo la mkoa litawasilishwa kwenye ngazi za juu za Tucta ili kulibariki.
Mwakapala alisema hayo kwenye hafla ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kukabidhiwa jengo la ghorofa tano lililojengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
“Wafanyakazi nchini sasa wamechoshwa na mishahara midogo, hivyo wakati umefika kwa wafanyakazi kutoogopa maandamano na migomo kudai haki,” alisema huku akishangiliwa.
Hata hivyo, Rais wa CWT, Gratius Mukoba alisema madai ya wafanyakazi yaliyowasilishwa Serikalini ni kutaka nyongeza ya mishahara kwa asilimia 100.
Mkoba alisema CWT hivi sasa wanasubiru ndani ya miezi mwili hadi Desemba kupata majibu.
hayatapatikana basi Serikali ijue imejipalia mkaa.
‘’Hatuwezi kuendelea kuwaona watu wasiofanyakazi wanapata mishahara mikubwa wakati wafanyakazi wanasota. Mwisho wa matatizo hayo ni sasa’’ alisema huku akiwataka wafanyakazi hususan walimu kuachana na njama za kutaka kuwatenganisha.
Alisema Serikali inatakiwa kuwalipa walimu Sh49 bilioni wanazodai zikiwamo Sh30 bilioni walizopunjwa katika mishahara na kwamba pia lazima ipunguze kodi kwa wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi.

Chanzo: Tucta yataka Sh750,000 kima cha chini - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
eh... kutoka katika serikali hii ya sisiem au ingine baada ya uchaguzi 2015!?
 
Tucta nao michosho tu. Hakuna lolote la maana.
 
...maccm hatari kweli,yameingiza mamluki kwenye chama cha walimu ili kuvunja nguvu yao,kweli kwa staili hii ya kukandamiza haki za wanyonge kuna maisha bora...?
 
Nimeacha kuwaamini hawa TUCTA
kipindi kile MGAYA alituaminisha mambo
makubwa na mazuri lakini alipoitwa IKULU

Sijui alipewa nini mpaka leo yuko kimya
unawezafikiri jamaa kahama Nchini hizi
zote kwasasa ni porojo tu hakuna jipya.
 
Ndugu zangu tuelewe tu kuwa hivi vyama vipo kwa maslahi ya ma ccm na wala haitawahi ikatokea hata siku moja wakawatetea wafanyakazi wao wamakuja na mapendekezo siku zote ambayo wanajua hayatekelezeki kwa maelekezo maalum kutoka kwa maccm.Hapo utasikia serikali inajitokesa na kusema hayo madai hayawezi kutekelezeka huku wakiorodhesha mambo kibao ambayo yanaikabili serikali nakuonekana kuwa ni ndoto kufanya hivyo kisha hao Tucta hutawasikia tena kwani jazi yao watakuwa wamemaliza.
 
Angezungumzia kupunguza mfumuko wa bei ningemuelewa mshahara ukipanda tu kila kitu kinapanda haina maana kabisa
 
Vyama vyote vimenunuliwa na CCM ikiwemo na CHADEMA
 
tangu mwaka mpya wa fedha unaanza na serikali kuongeza mshahara kiduchu walikuwa wapi,mbona hawakutoa kauli yoyote. au wanaona wafanyakazi ni wajinga wa kupokea matamko ya kipuuzo namna hii. tucta hawana lolote wapuuzi ,kwanza hakuna vyama vya wafanyakazi tz,bali kuna vyama vya kunyonya wafanyakazi.
 
eh... kutoka katika serikali hii ya sisiem au ingine baada ya uchaguzi 2015!?
Viongozi wa TUCTA watakuwa wanataka kugombea ubunge 2015 hivyo wanaosha jina mapema, nchi hii imeoza
 
hakuna jipya hapo kila kitu siasa tuuuuuuuuuuuuuuu
i hate TUCTA !!
 
Back
Top Bottom