Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Tazama!
Mwaka 1971 mkulima mmoja aitwae Said Mwamwindi alimuuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa marehemu Dr Kleruu kwa kumpiga risasi.
Kwa wanaokumbuka kesi ile Alhaji Mwamuhindi alinyongwa mpaka kufa.
Miaka 36 baadaye, yaani mwaka 2006, Mungu aliruhusu tukio kama hilo litukie lakini sasa iwe kinyume chake!
Hapa alikuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora kumuuwa dereva wa daladala kwa kumpiga risasi mpaka kufa!
Sote tunaelewa kilichoendelea kuhusiana na ile kesi; kiasi cha kugeuzwa na kuwa ya kuuwa bila kukusudia!
Ona haki ya hapa kwetu ilivyo!
Katika utetezi wake marehemu Mkuu wa mkoa alidai kuwa yule Dereva wa daladala alimtuka kwa kutumia kidole cha kati, hali iliyopelekea kupandwa na hasira na kumuua bila kukusudia!
Yule mkulima Mwamuindi naye katika utetezi wake alidai kuwa; Mkuu wa mkoa alimpiga kibao mbele ya wakeze, huku akimuuliza swali kwanini hataki kuhama? Hali iliyopelekea Mwamwindi kukasirika na kuchukua bunduki kisha kumuuwa Mkuu wa mkoa!
Matokeo kwa hawa wawili yalikuwaje?
Mwamuhindi alinyongwa kwa kuuwa kwa makusudi ila Mkuu wa mkoa alipewa dhamana kwa kuuwa bila kukusudia!!
Hukumuni ninyi wenyewe hapo!
Tukiachana na matukio hayo mawili yanayorandana ni juzijuzi tu wafanyakazi wengi wa kada ya chini waliondolewa kazini kwa sababu ya udanganyifu katika elimu zao.
Na hapa serikali ilisimamia haki kweli kweli.
Lakini sasa jambo lile lile lililowaondoa maskini wale linapokuja kuwagusa wakubwa wetu; sisi tunaambiwa tuna wivu!
Tena eti tunaunga mkono madawa ya kulevya!!
Hivi siku hizi mtu ukiwa ni mpinga madawa ya kulevya, ukitenda kosa lingine unakuwa huna hatia?
Mimi bado najaribu kuwaza tu!
Iwapo kama tukio la juzi la kuvamiwa kwa Stesheni ya Tv angelifanya mtu wa kada ya chini hivi leo mambo yangekuwaje?
Ndiyo maana mimi nadhani kuwa; katika nchi hii, sisi ni wazuri kuinyoosha sheria kwa wadogo ila kwa wakubwa tunaipindisha!!